Majeshi yaungana kuukabili ugaidi

Lilambalyakwilole

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
1,095
632
Majeshi yaungana kuukabili ugaidi



jwtz+pic.jpg



Kwa ufupi
Akifungua mafunzo hayo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi ameeleza kuwa kutokana na mabadiliko ya vyanzo vya migogoro katika jamii ya kimataifa, majeshi ya ulinzi nayo hayana budi kuwaendeleza askari wake uwezo wa kukabiliana nayo ili kudumisha amani.

ADVERTISEMENT
Dar es salaam.Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) limeungana na majeshi ya mataifa mengine manane kufanya mazoezi ya kukabiliana na uhalifu wa kimtandao ukiwamo ugaidi, dawa za kulevya na uharamia.

Akifungua mafunzo hayo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi ameeleza kuwa kutokana na mabadiliko ya vyanzo vya migogoro katika jamii ya kimataifa, majeshi ya ulinzi nayo hayana budi kuwaendeleza askari wake uwezo wa kukabiliana nayo ili kudumisha amani.

“Zamani tulikuwa tunajipanga kulinda mipaka yetu na kufanya maandalizi ya vita na yeyote atakayetushambulia. Hali imebadilika sasa hivi. Uharamia, ugaidi na dawa za kulevya ndiyo tishio la usalama kwa nchi nyingi duniani,” amesema waziri huyo.

Amesema kutokana na makosa hayo kutekelezwa kwa mitandao mikubwa duniani yanahitaji ushirikiano baina ya wadau mbalimbali ndani ya jamii ambao wataunganisha nguvu, ujuzi na uzoefu ili kupunguza kama si kutokomeza kabisa athari zake.

Dk Mwinyi amesema juhudi za Serikali nyingi duniani kukabiliana na uhamishaji wa binadamu pamoja na uharamia umesababisha hasara kubwa ambazo zinahitaji mikakati imara itakayohakikisha biashara na maisha kwa ujumla yanastawi pasipo kikwazo chochote kutoka kwa watu wachache.

Amesema hayo mbele ya maofisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na Umoja wa Afrika (AU).

Majeshi yaungana kuukabili ugaidi

 
Back
Top Bottom