Majeshi ya majini ya Iran na Urusi kufanya mazoezi Ghuba ya Uajemi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,890
Majeshi ya majini ya Iran na Russia kufanya mazoezi Ghuba ya Uajemi
Apr 29, 2019 10:12 UTC
Majeshi ya majini ya Iran na Russia yanapanga mazoezi ya pamoja na ya kipekee katika Ghuba ya Uajemi baadaye mwaka huu.

Hayo yametangazwa na Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Admeri Hossein Khanzadi ambaye ameyadokeza hayo alipozungumza na waandishi habari mapema leo hapa mjini Tehran baada ya kurejea kutoka safari muhimu nchini China ambapo amekutana na makamanda wenzake kutoka kote duniani.

Admeri Khanzadi ameongeza kuwa, tayari mazungumzo yameshaanza na Russia kuhushu maozeozi hayo ya pamoja.
Majeshi ya majini ya Iran na Russia hufanya mazoezi ya pamoja mara kwa mara katika Bahari ya Kaspi na kwa msingi huo mazoezi yajayo katika Ghuba ya Uajemi yatainua kiwango cha uhusiano wa pande mbili.

Admeri Khanzadi aidha ameashiria mpango wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kuimarisha uhusiano wa mafunzo na majeshi ya majini ya nchi zingine na kusema: "Iran inachunguza mwaliko kutoka nchi kama vile India, China, Pakistan na Italia ambazo zimetaka ushirikiano katika mafunzo kwa maafisa wa kijeshi."

Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria matamshi ya hivi karibuni ya waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel ambaye alitishia kuzishambulia meli za mafuta za Iran na kusema "maji ya kimataifa ni ya nchi zote, na hivyo jeshi la majini lina jukumu la kulinda maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran." Admeri Khanzadi amesisitiza kuwa, meli za mafuta za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni sehemu ya ardhi ya nchi hii na zitalindwa kikamilifu.
Tags
RUSSIA
4bpw5022b892421bd9y_800C450.jpg
 
Hiyo inaitwa 'military provocation' to Trump and NATO Russia na Irani pamoja na Uturuki, nitishio kubwa kwa jeshi la NATO
 
Back
Top Bottom