Majeruhi wa Lucky Vicent: Doreen apata hisia, wenzake waruhusiwa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Hiyo ni ishara kuwa upasuaji mkubwa wa uti wa mgongo aliofanyiwa,umefanikiwa.

Wenzake Wilson Tarimo na Saidia Ismael wameruhusiwa baada ya kupata matibabu na sasa wanaendelea na mazoezi ya viungo katika nyumba maalum kwa wagonjwa waliovunjika viungo jijini Sioux.

Mbunge wa Singida Kaskazini(CCM) Lazaro Nyalandu, ameandika kwatika ukurasa wake wa facebook akisema Doreen ameweza kuisogeza miguu yake miwili kwa mara ya kwanza tangu apate ajali hiyo. “Tuendelee kumuombea , huu ni uponyaji wa uti wake wa mgongo.” aliandika Nyalandu

Pia watoto Saidia na Wilson, pamoja na wazazi wao, walikwenda Hospitali kumuangalia Doreen leo ambaye bado amelazwa akiendelea na matibabu.


Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom