Majeruhi nane ajali ya moto Morogoro waruhusiwa kutoka wodini

Kisiwa Cha Harishi

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2019
Messages
1,020
Points
2,000

Kisiwa Cha Harishi

JF-Expert Member
Joined Jun 15, 2019
1,020 2,000
Morogoro. Majeruhi nane kati ya 18 waliokuwa wamelazwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro nchini Tanzania ambao walitokana na ajali ya lori la mafuta ya petroli wameruhusiwa kutoka wodini.
Ajali hiyo ilitokea asubuhi ya Jumamosi Agosti 10, 2019 baada ya gari hilo kuanguka kisha kuwaka moto eneo la Msamvu mkoani Morogoro.
Akizungumza na Mwananchi jana Jumapili Septemba 1,2019 Mganga Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kusirye Ukio alisema majeruhi hao wameruhusiwa baada ya maendeleo yao kurudisha.
Dk Ukio alisema wagonjwa hao majeruhi walianza kuruhusiwa Jumatatu hadi Alhamisi iliyopita huku akieleza 10 waliobaki bado wanaendelea kupatiwa matibabu chini ya uangalizi wa wauguzi na madaktari.
Pia, Dk Ukio alisema awali walikuwa na majeruhi 16 waliobaki baada ya wengine kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam lakini waliongezeka wawili waliotoka majumbani na kufikia 18.
Tangu kutokea kwa ajali hiyo hadi jana Jumapili, jumla ya watu 104 wamefariki huku majeruhi 29 wakiendelea kupatiwa matibabu. Kati ya majeruhi hao 18 wapo Morogoro na 11 Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

CREDIT : Gazeti la Mwananchi
 

Forum statistics

Threads 1,381,484
Members 526,110
Posts 33,801,867
Top