Majengo ya TBA hayana ulinzi wa polisi - Kangi Lugola

Sheria hazitambui Skype zinatambua mahojiano ya ana kwa ana.Peleka mswada wa marekebisho bungeni utakaotambua Skype kuwa njia mojawapo inayokubalika kisheria za Tanzania kwa mahojiano.Sheria zilitungwa kabla ya Skype kuwepo na hazijabadilishwa.Tundu Lisu na dereva wafike tu Tanzania wahojiwe
Kama hazitambui zilizindua mahakama inayotembea kwann? Kama hazitambui kwa nini kuna ushahidi wa sauti na video?

Acha kupotosha kitu usichokijua Chief
 
Kama hazitambui zilizindua mahakama inayotembea kwann? Kama hazitambui kwa nini kuna ushahidi wa sauti na video?

Acha kupotosha kitu usichokijua Chief
Hiyo ni
Mobile court sio mobile police investigation or interrogation.Naongelea Sheria za mahojiano ya kipolisi siongelei mobile court.Hivi wewe sheria za mahakama na polisi unaona ziko sawa.police hawajazindua police mobile interrogation!!!!..
 
Kama nyumba tu ya mkuu wa wilaya/mkoa inalindwa na police unadhani sehemu yenye nyumba za Mawaziri/naibu spika etc itakua haina police wa kulinda?

Kweli nimeamini common sense isn't so common.
Eneo kama lime milikishwa kwa Bunge basi Bunge linawajibika kuomba kwa serikali ulinzi wa Polisi au Bunge likaamua kutafuta Kampuni binafsi kwa masharti ya Masaa 24 au Usiku tu.Ukumbuke Bunge ni taasisi inayo jitegemea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elewa hayo makazi yapo ndani ya security complex,na viongozi waandamizi wa kiserikali wanaishi hapo,sasa wewe unataka kutuaminisha hapa kuwa cctv hazipo?,je unataka kutuaminisha hapa kuwa kwenye security gate ya kuingia na kutoka kwenye complex hii haina cctv?wala walinzi wenye log book?;ninachokiona mimi ni ujinga wa jeshi letu la polisi wa kushindwa to protect hiyo crime scene,hamana hata police tapes kuzunguka eneo hilo,je unaelewa hiyo gari ipo wapi hadi leo?hadi leo hatujui kama silaha zilizotumika na za aina gani wala hatujui kama polisi walifanukiwa kukamata hizo silaha na kuzifanyia ballistic tests;usituletee uongo hapa ili uwe ukweli wa kitaifa.
Unatakiwa kwanza ujue eneolile kama lilikua likilindwa ba kampuni je! Nani aliingia mkataba na Kampuni iyo, Bunge au Serikali . je! Mkataba wa ulinzi ni Usiku au masaa 24. Je iyokampuni ilikua inausisha CCTV CAMERA katika ulinzi au ilitumia askari pekeyake? Kama kweli camera ilikuwepo ilikua chini ya uangalizi wa kampuni, anayeishi ndani ya jengo polisi au Mwenye jengo. Alafu kama wahusika awajakamatwa sasaizo silaha utazipataje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TL akirudi atakua na wakati mgumu sana. Ikumbukwe kufikia maamuzi ya kumshambulia, ilitokana na ukweli kwamba kisheria ilikua ngumu sana kumshinda, ikapelekea hayo yaliyotokea yamkute. Bahati akapina.

Akirudi ataundiwa zengwe la kesi za uhaini au kushambuliwa kikamilifu warekebishe kosa walilofanya awali. Ndito za kugombea urais azisahau tu, vinginevyo utokee muujiza.

Kwa hizi kauli za viongozi, bora abaki huko huko.
Mungu ndiye mlinzi wa watu usikae na kufikiri kuwa nia ya adui lazima itimie, ni ujinga kuamini kuwa kila apangacho adui yako kitafanikiwa
Kumbuka Sauli alishindwa kumwua Daudi kijana mdogo kabisa wakati yeye alikuwa ni mfalme
 
Mungu ndiye mlinzi wa watu usikae na kufikiri kuwa nia ya adui lazima itimie, ni ujinga kuamini kuwa kila apangacho adui yako kitafanikiwa
Kumbuka Sauli alishindwa kumwua Daudi kijana mdogo kabisa wakati yeye alikuwa ni mfalme

Mie nimetoa maoni yangu binafsi.
Kumbuka Daudi alikuwa amepakwa mafuta kuwa mfalme.

Yesu alilisha watu maelfu mikate na wana wa Israel walikula Manna jangwani, mbona sie tubahangaikia chakula?
 
*on top of that ni kwamba baada ya tukio zilichomolewa zile CCTV camera na hiyo picha ni baada ya tukio means zilishapelekwa kusiko julikana*

Unapiga picha angle moja halafu unaanza pelepete leta picha Multi Angle Halafu ziwe na date and Time.
 
Hiyo ni
Mobile court sio mobile police investigation or interrogation.Naongelea Sheria za mahojiano ya kipolisi siongelei mobile court.Hivi wewe sheria za mahakama na polisi unaona ziko sawa.police hawajazindua police mobile interrogation!!!!..
Kwani hapo Lisu ndie anaeshitaki au jamhuri ndio inashitaki na T ni kama shahidi tu? Au ikoje hiyo!!

Je ni kweli kwamba idara ya polisi bado iko nyuma hadi isitumie mobile ivestgation ikiwa mahakama yenyewe imepiga hiyo hatua?

Eti kama ushahidi wa kimobile hautumiki kwa nini huwa wapelelezi wanapeleka ushahidi wa videos ama audio kama ushahidi muhimu waliopata?
.
Yawezekana nimekwelewa ila nijuze na hilo tafadhali
 
Kama nyumba hazina Polisi so what?

Ni hivi kwa utaratibu wa serikali wakati ule mpaka sasa hivi. Makampuni Binafsi ya ulinzi ndiyo yanalinda ofisi nyeti za serikali na mashirika ya Umma.

Ukifika Dodoma Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Inalindwa na Kampuni Binafsi. Jengo la Wizara ya Fedha Linalindwa na Makampuni Binafisi na Ma CCTV camera kila kona, Ofisi ya Wizara ya Serikali za Mitaa inalindwa na Kampuni Binafsi.

Kwa hiyo kutokuwepo Askali sio tija.


Ni upuuuzi fulani hivi Naibu speaker akiwa na eskoti ya magari mawili popote anapokwenda na akifika nyumbani wale askali waondoke na wamuuache peke yake bila ya ulinzi.

Hizi kauli nina mashaka nazo ni vizuri zikawa zimefanyiwa utafiti kidogo.

Maana Mh Lugola ndiyo amezidi kuchanganya wananchi kwamba kuna uzembe mkubwa wa ulinzi na usalama wa Viongozi wetu.
Yeah umesema ukweli kwa asilimia nyingi samahani kama nitatofautiana kwa lengo la kusema nijuacho hapo.
1. Ni Ukweli kuwa kampuni binafsi zilikuwa zinalinda main gate. Hadi 2010 nilipotoka hapo Area D maana niliwahi kukaa
2. Ni ukweli kuwa wakati wa session za bunge askari huja kufanya ulinzi ila ilijuwa kuanzia jioni saa 12 na si mchana
3. Kama cctv ziliwekwa ni baada ya 2010 .
Lkn hili halizuii kufanya uchunguzi wa kipolisi.
4. Ni ukweli upo uzembe ambao polisi wanaleta kuwepo mashaka kwa kutowajibika tangu shambulizi lilipofanyika kwa kuwashika au kuwahoji wahusika wowote tangu Dereva au yoyote hata kama ni walinzi wa kampuni binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom