Majengo ya TBA hayana ulinzi wa polisi - Kangi Lugola

Nelson Masaduki

JF-Expert Member
Oct 27, 2017
341
500
Nimemsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola akifafanua baadhi ya mambo yanayohusu kesi ya Tundu Lissu. Pamoja na mambo mengine, amemuomba Lissu aje ayaeleze hayo mambo mengi waliyonayo kuhusu kesi yake. Ninachokiona ni umuhimu wa maelezo ya mlalamikaji katika hatua za awali za upelekaji wa kesi za jinai mahakamani.

Nelson,
Dodoma
 
redio

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
2,182
2,000

Itakua jambo jema kurudi atueleze izo Camera zilifungwa sehemu gani, na authibitishie umma kama kweli polisi uwa wanalinda eneo ilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
26,506

Kama nyumba tu ya mkuu wa wilaya/mkoa inalindwa na police unadhani sehemu yenye nyumba za Mawaziri/naibu spika etc itakua haina police wa kulinda?

Kweli nimeamini common sense isn't so common.
 
Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
9,112
2,000
Itakua jambo jema kurudi atueleze izo Camera zilifungwa sehemu gani, na authibitishie umma kama kweli polisi uwa wanalinda eneo ilo.
Yaani anasubiliwa aliyepigwa risasi ndio arudi authibitishie Umma kama kweli pale kulikuwa na CCTV camera na kama kweli lile gate huwa lina(paswa) kuwa na walinzi 24/7?

Well, kwa akili hizi bila shaka tutamtaka auhakikishie Umma wa Watanzania kama ni kweli na yeye ana apartment eneo lile, kama kweli akina Kalemani na Tulia ni majirani zake na kama kweli alikula shaba 16.
 
The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
15,034
2,000
TL akirudi atakua na wakati mgumu sana. Ikumbukwe kufikia maamuzi ya kumshambulia, ilitokana na ukweli kwamba kisheria ilikua ngumu sana kumshinda, ikapelekea hayo yaliyotokea yamkute. Bahati akapina.

Akirudi ataundiwa zengwe la kesi za uhaini au kushambuliwa kikamilifu warekebishe kosa walilofanya awali. Ndito za kugombea urais azisahau tu, vinginevyo utokee muujiza.

Kwa hizi kauli za viongozi, bora abaki huko huko.
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
1,884
2,000
Ukitazama picha hiyo nimeikuta sehemu naona kamera haionekani kweli View attachment 1022094
Elewa hayo makazi yapo ndani ya security complex,na viongozi waandamizi wa kiserikali wanaishi hapo,sasa wewe unataka kutuaminisha hapa kuwa cctv hazipo?,je unataka kutuaminisha hapa kuwa kwenye security gate ya kuingia na kutoka kwenye complex hii haina cctv?wala walinzi wenye log book?;ninachokiona mimi ni ujinga wa jeshi letu la polisi wa kushindwa to protect hiyo crime scene,hamana hata police tapes kuzunguka eneo hilo,je unaelewa hiyo gari ipo wapi hadi leo?hadi leo hatujui kama silaha zilizotumika na za aina gani wala hatujui kama polisi walifanukiwa kukamata hizo silaha na kuzifanyia ballistic tests;usituletee uongo hapa ili uwe ukweli wa kitaifa.
 
malisoka

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
1,863
2,000
Kama nyumba hazina Polisi so what?

Ni hivi kwa utaratibu wa serikali wakati ule mpaka sasa hivi. Makampuni Binafsi ya ulinzi ndiyo yanalinda ofisi nyeti za serikali na mashirika ya Umma.

Ukifika Dodoma Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Inalindwa na Kampuni Binafsi. Jengo la Wizara ya Fedha Linalindwa na Makampuni Binafisi na Ma CCTV camera kila kona, Ofisi ya Wizara ya Serikali za Mitaa inalindwa na Kampuni Binafsi.

Kwa hiyo kutokuwepo Askali sio tija.

Ni upuuuzi fulani hivi Naibu speaker akiwa na eskoti ya magari mawili popote anapokwenda na akifika nyumbani wale askali waondoke na wamuuache peke yake bila ya ulinzi.

Hizi kauli nina mashaka nazo ni vizuri zikawa zimefanyiwa utafiti kidogo.

Maana Mh Lugola ndiyo amezidi kuchanganya wananchi kwamba kuna uzembe mkubwa wa ulinzi na usalama wa Viongozi wetu.
 
mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
26,506
2,000
TL akirudi atakua na wakati mgumu sana. Ikumbukwe kufikia maamuzi ya kumshambulia, ilitokana na ukweli kwamba kisheria ilikua ngumu sana kumshinda, ikapelekea hayo yaliyotokea yamkute. Bahati akapina.

Akirudi ataundiwa zengwe la kesi za uhaini au kushambuliwa kikamilifu warekebishe kosa walilofanya awali. Ndito za kugombea urais azisahau tu, vinginevyo utokee muujiza.

Kwa hizi kauli za viongozi, bora abaki huko huko.
Nna uhakika ktk kipindi Lissu ataishi kwa amani ni kipindi akirudi Bongo na ulinzi watamuwekea bila kupenda,hata akiumwa malaria tu watapata tabu sana.

Maana akifanyiwa figisu yoyote kwa jinsi alivyokichafua huko duniani ndipo patashika nguo kuchanika.

Bob wine alivopewa kichapo Uganda akaenda huko Marekani kutibiwa akakutana na wanasiasa huko states,medias etc baada ya kurudi Uganda Mseveni amemfanya nini?
 
Mkuu uhai hauna hauwekwi rehani. Kauli za hawa jamaa kuanzia juu hadi chini haziashirii nia njema kwa TL. Unamkumbuka Hanga wa Unguja na kilichomtokea?
 
Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,303
2,000
Nimemsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola akifafanua baadhi ya mambo yanayohusu kesi ya Tundu Lissu. Pamoja na mambo mengine, amemuomba Lissu aje ayaeleze hayo mambo mengi waliyonayo kuhusu kesi yake. Ninachokiona ni umuhimu wa maelezo ya mlalamikaji katika hatua za awali za upelekaji wa kesi za jinai mahakamani.

Nelson,
Dodoma
Kwani mpaka aje. Haweawezi wasiliana naye kwa Skype?
Au ndyo wanataka aje wammalize. Na haji ngo!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfiaukweli

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
5,603

Hiyo kesi mshtaki ni serikali (haina mlalamikaji). Lissu atakuwa shahidi upande wa serikali (mwendesha mshtaka akipenda). Kila mkijaribu kutafuta upenyo wa kujinasua mnakutana na dead-end. Ukweli haushindwi na uongo siku zote.
 
mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
26,506
2,000
Mkuu uhai hauna hauwekwi rehani. Kauli za hawa jamaa kuanzia juu hadi chini haziashirii nia njema kwa TL. Unamkumbuka Hanga wa Unguja na kilichomtokea?
Let's wait&see mkuu,though siasa zimebadilika sana sasa hivi mkuu.

Siku hizi ukicheza vibaya tu utasikia USA&EU wanamtambua mpinzani wako kama rais wa nchi(Mfano Venenzuela),hahah.
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
1,884
2,000
TL akirudi atakua na wakati mgumu sana. Ikumbukwe kufikia maamuzi ya kumshambulia, ilitokana na ukweli kwamba kisheria ilikua ngumu sana kumshinda, ikapelekea hayo yaliyotokea yamkute. Bahati akapina.

Akirudi ataundiwa zengwe la kesi za uhaini au kushambuliwa kikamilifu warekebishe kosa walilofanya awali. Ndito za kugombea urais azisahau tu, vinginevyo utokee muujiza.

Kwa hizi kauli za viongozi, bora abaki huko huko.
Woga umetutawala sisi watanzania,tumekuwa mpaka tunaogopa vivuli vyetu,elewa yanayotokea Kenya now kuna damu imemwagika pale ili waoga kama mimi na wewe tuwe huru,pale SA damu ilimwagika ili wengine wawe huru,Venezuela damu inamwagika ili waoga kama wewe na mimi(tulio hodari kuandamana kwenye key boards) tuwe huru,Mh.Lisu damu yake itamwagika na kuteswa(elewa watoto wake wanakuwa bila baba)ili waoga mimi na wewe tupumue hewa ya uhuru.usitishe watu wewe na uoga wako tulia.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
24,840
2,000
Kama nyumba tu ya mkuu wa wilaya/mkoa inalindwa na police unadhani sehemu yenye nyumba za Mawaziri/naibu spika etc itakua haina police wa kulinda?

Kweli nimeamini common sense isn't so common.
Mkuu wa mkoa ni mkuu wa majeshi yaliyoko mkoani kwake na mkuu wa wilaya ni mkuu wa majeshi yaliyomo wilayani mwake ulinzi wake sio sawa na wa mbunge au Waziri .Ni mkubwa zaidi.Sababu wao ni viongozi wa jeshi wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya.
 
The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
15,034
2,000
Let's wait&see mkuu,though siasa zimebadilika sana sasa hivi mkuu.

Siku hizi ukicheza vibaya tu utasikia USA&EU wanamtambua mpinzani wako kama rais wa nchi(Mfano Venenzuela),hahah.
Inategemea wanamaslahi mapana kiasi gani kwenye hiyo nchi.

Wenzetu wapo makini sana na utaifa na maslahi ya nchi.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
24,840
2,000
Kwani mpaka aje. Haweawezi wasiliana naye kwa Skype?
Au ndyo wanataka aje wammalize. Na haji ngo!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sheria hazitambui Skype zinatambua mahojiano ya ana kwa ana.Peleka mswada wa marekebisho bungeni utakaotambua Skype kuwa njia mojawapo inayokubalika kisheria za Tanzania kwa mahojiano.Sheria zilitungwa kabla ya Skype kuwepo na hazijabadilishwa.Tundu Lisu na dereva wafike tu Tanzania wahojiwe
 
The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
15,034
2,000
Woga umetutawala sisi watanzania,tumekuwa mpaka tunaogopa vivuli vyetu,elewa yanayotokea Kenya now kuna damu imemwagika pale ili waoga kama mimi na wewe tuwe huru,pale SA damu ilimwagika ili wengine wawe huru,Venezuela damu inamwagika ili waoga kama wewe na mimi(tulio hodari kuandamana kwenye key boards) tuwe huru,Mh.Lisu damu yake itamwagika na kuteswa(elewa watoto wake wanakuwa bila baba)ili waoga mimi na wewe tupumue hewa ya uhuru.usitishe watu wewe na uoga wako tulia.
Mie sijatisha mtu mkuu. Nimetahadharisha. Najua iko siku ntakufa kama ilivyo kwa wengi wetu lakini sio kufa kizembe.

Baba wa taifa alikufa? Mandela alikufa? Sio kila mabadiliko yanahitaji damu kumwagika.

Akirudi wakamuua na ukombozi usipatikane itakufaidia kitu gani?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom