Majengo ya ofisi za mizani ya kupimia uzito wa magari(Weigh Bridge), yawe ya rangi moja nchi nzima na ikiwezekana hata ramani ya majengo iwe ni moja

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Kila naposafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine kwa njia ya barabara, huwa nashangazwa kuona majengo ya ofisi katika vituo vya kupimia uzito wa magari (weigh bridge) hapa nchini yakitofautiana kwa rangi na hata style ya ujenzi ingawa yote yako chini ya serikali moja na yanafanya kazi ile ile.

Sidhani kama inapendeza kukuta katika babara(highway) A, ofisi hizi zina rangi kama ya njano na katika barabara B, majengo haya yana rangi tofauti kabisa huku hata ramani za majengo haya nazo zikiwa tofauti tofauti.

Najua kuna watu watasema kufanya kazi moja si sababu ya msingi ya kutaka majengo haya yawe na rangi moja ila binafsi naamini itapendeza zaidi iwapo kutakuwa na uniformity hasa ya rangi au rangi zitazotumika katika kuyapaka rangi majengo haya ila yaweze kutambulika kwa rangi zake mahususi kama ilivyo kwa vituo vya Polisi, majengo ya ofisi za vyama vya siasa ambayo hupakwa rangi za vyama vya siasa, n.k.

Naamini ofisi hizi zikiwa na rangi zake maalumu basi zitapendeza sana na hii imaana zaidi kwani hata wafanyakazi wa mizani hizi wanakuwa na uniform zinazofanana hivyo si vibaya hata rangi za majengo haya nazo zikawa zinafanana nchi nzima.

Swala la kuwa na ramani moja labda hili ndio linaweza kuwa gumu kidogo, ila kama linawezekana, basi itapendeza zaidi.

Ni ushauri tu kwa wenye mamlaka.
 
Back
Top Bottom