Majeneza ya kukodi na makaburi ya kupanga

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
182,874
2,000
Mi nikajua 'idea' umeitoa kwenye link flani niliiona google, ipo kama ulivyoelezea.

Nilishuhudia jinsi hayo makaburi ya kupangisha yalivyo, ni vyumba vidogo vidogo mfumo wa drawers vinavyoweza kuhifadhi ukubwa wa jeneza moja kila kimoja, zilizojengwa kwenye ukuta mmoja.

Jeneza ama mkebe wa majivu ukishahifadhiwa humo, mlango hufungwa kwa slab ya zege na kuwekwa jina ama namba ya utambulishi.

Namna ndugu wanavyokuja kuondoa mabaki ya mpendwa wao, kuyahamisha ama hela ya pango kuisha, slab iliyofungia huvunjwa na kuchomoa jeneza.

Hayo mabaki yakishatolewa, chumba hubakia wazi kungojea mpangaji mwingine!
Nimeipata

A Cemetery Where You Pay Rent To Keep The Dead!
By Syeda Farah Noor
Updated: July 12, 2017

Letting the dead part away is quite painful and if it is something that you need to pay an amount for, it's the worst thing!

We live in a world where everything is pricey and when it comes to paying for the dead, it would surely break your heart.

A cemetery in Guatemala is one such place where the dead bodies are removed if the family members do not pay the price for their graves!

Check out this more bizarre story of not letting the dead be at peace for the cost of money!

It Is A Daily Task Here…
Death is painful and when it is your loved one, it would surely be devastating. What's worse is knowing that the men who work in this graveyard remove the corpses. People whose families can no longer afford the luxury of a private crypt are removed when the lease on a grave expires. Removing the deadbodies from their coffins is a daily task here.

The Rental Agreement…
It's all in the rental agreement. Families of the deceased must pay a "rent" to ensure their loved ones remain undisturbed within their vertical tombs. According to the agreement, the first six years of burial are free, but after that, they are charged $24 for every successive four years. This is a lot of money for most of the folks burying their loved ones in these crypts
10-1499662588-2.jpg
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
182,874
2,000
Eneo la Kinondoni makaburini pamejaa mno na makaburi yamepandiana.. Ni vigumu kulikuta salama kaburi la mpendwa wako ukikaa muda mrefu bila kulitembelea..
Kwa hili wazo langu kaburi litakuwa salama hata usipolitembelea kwa muda mrefu.. Ila uwe tu na hakika ya ku clear bill utakapokuja!
 
Mar 13, 2019
17
45
Naweza kuonekana mwendawazimu kwa hii mada lakini wenye kuona mbali wataona mantiki yake!
Ni hili la majeneza ya kukodi na makaburi ya kupanga..Maisha yanaenda kasi sana na mabadiliko mengi yasiyotarajiwa yanatokea kwa kasi kubwa...
Miaka 30 nyuma ilikuwa ni ajabu kukuta jeneza likiwa limeshatengenezwa tayari likisubiri maiti.. Iliitwa uchuro... Jeneza lilitengenezwa baada ya mtu kufa.. Na haikuwa bidhaa ya kujiingizia kipato..

Miaka 30 nyuma sehemu za kuzikia zilitolewa bure na kwa wale ambao hawakuwa na ndugu ama walikufa na hawakujulikana asili yao wala ndugu zao walizikwa na manispaa kwenye makaburi ya serikali... Siku hizi hao ndugu ni dili.. Kuna watu wananunua misiba!

Nje ya hayo ya marehemu vitu kama harusi na sherehe mbalimbali havikuwa na michango ya lazima kama ilivyo leo hii.. Sehemu za wazi ndio zilitumika na kama kuna kumbi basi zilitolewa bure au kwa malipo kidogo
Hakukuwa na caterers
Hakukuwa na ma mc wa kukodi
Hakukuwa na wapambaji wa kukodi nk
Nguo za harusi pia zilikuwa rasmi kabisa za wahusika ..hazikikodishwa kama ilivyo leo hii.. Na hizo nguo za harusi zilitunzwa mpaka kifo cha mhusika.. Na ndio nguo atakazovishwa siku yake ya mwisho duniani

Sasa kwa dunia ya wenzetu tayari wako hatua tano mbele wao hawaziki tena.. Wanachoma moto na kukodi sehemu ya kuhifadhi majivu yaliyoko kwenye jeneza dogo la mkebe.. Mkataba ukiisha wanaweza ku renew ama kuhamisha...!
Sisi huku bado hatujafikia hatua hiyo na hata hivyo sio mila na tamaduni zetu kuchoma wapendwa wetu
Kwa tunakoelekea na kwa hizi gharama kubwa za mazishi kwasasa ni lazima sasa tuanze kuangalia option ya kuwa na majeneza ya kukodi na makaburi ya kupanga

Maisha yetu yamegawanyika katika sherehe kuu tatu 1. Kuzaliwa 2. Harusi 3. Kifo.. Kila mojawapo ya hizo ndugu jamaa na marafiki hujitahidi kulifanya tukio kubwa na la kukumbukwa kwa muda mrefu..
Sasa basi kwenye hili la kifo tuanze kujiandaa kuwa na majeneza ya kukodi na makaburi ya kupanga

Kila mtu anapenda kitu kizuri hivyo basi kuwepo na majeneza mazuri ya kukodi.. Haya mwisho wake ni pale makaburini ambapo wakati wa kuzika ..mwili utabadilishwa na kuwekwa kwenye jeneza la kawaida tuu..kuliko kutumia gharama kubwa kununua jeneza la gharama ambalo linaenda kuharibika ardhini...!

Kuhusu makaburi ya kupanga iko hivi... Unapata msiba wa ndugu yako, mwanao mke,mume nknk.. Lakini kipindi hicho mambo yako bado hayako kivile na huna kwako mwenyewe unaishi sehemu ya kupanga ...Kwenye situation kama hii ukipata msiba unaweza kwenda kuhifadhi mwili kwenye makaburi ya kupanga mpaka utakapopata sehemu yako mwenyewe...

Nitandelea
Kaka mshana samahani naomba unisaidie namba zako za cm nina shida very urgent
 
SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,612

Yap, hii ya majeneza ya kukodi haipo mbali sana. Kwa mfano, unaweza kuwa na jeneza zuri sana (material inayodumu (metal?), nyepesi, etc) kubwa kidogo hili ndio linakodishwa. Hilo linatengenezwa kuweza Ku accommodate jeneza dogo ndani na kulifanya liweze kufunguka kwa urahisi wakati wa kulitoa hilo jeneza dogo......hili jeneza dogo linakuwa la kawaida tu.... la mbao laini na lisilo na marembo kabisa....hili ndio linabakia kaburini.

Kwa upande wa makaburi ninaloona ni kuwa watu wanaweza kuanza kuchimba na kutengeza (kujenga) makaburi kadhaa katika eneo fulani....katika mpangilio mazuri wa kuvutia na unaotumia vizuri ardhi.....kwa hiyo ukitaka kuzika mpendwa wako, "unanunua" kaburi (shimo?) ambalo lipo tayari kila kitu, tena mpaka ule mfuniko (wa zege) unakuwa umetengenezwa tayari,....ni kuuinua na kufunika kaburi tu.
 
Ni wazo zuri pia lakini hapo kumbuka kuna ya kukodi na kuna ya kununua moja kwa moja
 
  • Thanks
Reactions: SMU

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom