Brigedia Chan-ocha
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 1,353
- 2,842
Jenerali MUSA SAVAGE na Jenerali Badjie wamemgomea Rais wa Gambia Bwana Yahya Jammeh, wakisema tarahe 19 January 2017 wataanza kumtii Rais mteule ADAMA Barrow, linataarifu Gazeti la FREEDOM la Nchini humo.
Taarifa zinasema, Jana Alhamis Ikulu ya Gambia kulikuwa na Kikao cha " SECURITY BRIEFING" ambapo Rais Yahya Jammeh ametaarifiwa kuwa wakuu wa Battalions zote wamekubaliana kutoruhusu Jeshi kupigana ikiwa itatokea uvamizi wa Nchi za ECOWAS ili kumuondoa madarakani.
Jenerali MUSA SAVAGE tayari amewaarifu wenzake kuwa hataruhusu Battalion yake ipigane na kwamba ni lazima maamuzi ya wananchi wa GAMBIA yaheshimiwe.
Hali ilibadilika jana ndani ya ikulu punde baada ya Yahya Jammeh kuarifiwa hivyo ambapo alibadilika na kuondoka ndani ya kikao asiamini kile alichoelezwa na mtu wake wa karibu Jenerali Badjie.
Taarifa mpya zinasema, Tayari mazungumzo yameanza ili Rais Yahya Jammeh aende uhamishoni katika moja ya nchi za AMERICA KUSINI ambapo nchi hizo hazina utaratibu wa kutekeleza amri za ICC za kumsalimisha mtu kwenye mahakama hiyo.