Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Ntambaswala

JF-Expert Member
Dec 7, 2008
255
78
Take a break, na tujikumbushe enzi zile za RTD, ambapo kulikuwa hakuna FMs rado kama sasa. Hakika kulikuwa na watangazaji, vipindi bomba na hata nyimbo za kutambulisha vipindi zilikuwa makini sana. Hebu ngoja niwakumbushe baadhi ya watangazaji wa wakati huo.

1. Nassoro Nsekeli- alikuwa na sauti kama ya mafua hivi alikuwa mtaalamu wa kipindi cha Majira- ndiye aliyetangaza kifo cha Nico Zengekala

2. Bujago Izengo wa Kadago- Kibesi chake kilikuwa safi sana

3. David Wakati (DG) - kipindi cha Nipe habari- Kwaherini wote, mungu awalinde na mmbaki salama, mungu akipenda..............

4, Khalid Ponera- Zilipendwa

5. Ahmed Kipozi- taarifa ya habari

6. Hassan Mkumba- matangazo ya vifo

7. Siwatu Luwanda

8. Salama Mfamao
9. Mohamed Amani (Mohamed Dahman)

10. Salim Seif Nkamba

12. CHisunga Steven- kipindi cha Ugua pole duu

13. Bathoromeo KOmbwa (bati Kombwa) - WAkati wa Kazi

14. Ahmed Jongo- Mpira

15. Christina Chokunogela

16. Dominic Chilambo- Mpira

17. Edda Sanga
18. Debora Mwenda- Mama na Mwana
19. Aloycea Maneno- Ombi lako, cheichei Shangazi, mama na mwana

Duu nawamiss sana hawa watu tofauti na watangazaji wa sasa
 
1. Dunstan Tido Mhando.

2. Suleiman Kumchaya.

3. Ben Kiko (Benedict Kikoloma - Homeboy) - Wakati wa vita ya nduli Amin.

4. Leonard Mambombotela???

5. Idd Rashid Mchata - Mchatta (kulikuwa na KM Chadema/Mtangazaji na Refa (nimekumbushwa).

6. (Abdul Masoud)inasemekana aliuawa kwa utapeli 80's. Wamenikumbusha.
7. Mzee Kijaruba Abdallah Mlawa.

8. Mikidadi Mahmoud. (http://www.bongocelebrity.com/2009/03/12/tanzania-rhythm-rtdmikidadi-mahmoud/).

9. Julius Nyaisanga.

10. Sango Kipozi.

11. Charles Hilary.

12. Mshindo Mkeyenge.......
 
Sikonge,
Idd Rashid Mchata alikuwa ndo mtangazaji nafikiri aliwahi kuwa kiongozi wa UVCCM Dar, alikuwa na sauti fulani hivi ya kukwaruza, lakini nzuri sana.

Nadhiri Mayoka

Karim Besta

Salim Mbonde- Tunawaletea Mzungumzo ya Habari.......

Faudhiat Ismail Abood- alikuwa hakosei hata akisoma taarifa ya habari

Leonard Mambo Mbotela alikuw KBC na kipindi cha Je huu ni Ungwana?
 
20. Michael Katembo
21. Abdul Ngalawa
22. Halima Mchuka
23.....................
24......................
25......................
 
Sarah Dumba - RTD (Sasa ni Mkuu wa Wilaya Mpya isiyo na Umeme!)

Athumani Magoma (rip)
Titus Steven (rip) huyu alifariki kwa gari lake kugongwa na treni pindi tu aliporudi kutoka BBC London baada ya Tz kupata uhuru.
Japhet Muura
Godfrey Mngodo
Thecla Gumbo
Abdul Baker (maelezo baada ya habari)
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Take a break, na tujikumbushe enzi zile za RTD, ambapo kulikuwa hakuna FMs rado kama sasa. Hakika kulikuwa na watangazaji, vipindi bomba na hata nyimbo za kutambulisha vipindi zilikuwa makini sana. Hebu ngoja niwakumbushe baadhi ya watangazaji wa wakati huo.

1. Nassoro Nsekeli- alikuwa na sauti kama ya mafua hivi alikuwa mtaalamu wa kipindi cha Majira- ndiye aliyetangaza kifo cha Nico Zengekala

2. Bujago Izengo wa Kadago- Kibesi chake kilikuwa safi sana

3. David Wakati (DG) - kipindi cha Nipe habari- Kwaherini wote, mungu awalinde na mmbaki salama, mungu akipenda..............

4, Khalid Ponera- Zilipendwa

5. Ahmed Kipozi- taarifa ya habari

6. Hassan Mkumba- matangazo ya vifo

Du mwanangu hapa umeniacha hoi, teh teh, yaani huyu mtangazaji ali specialize kwenye matangao ya vifo! mweh!
 
1. Dunstan Tido Mhando.

2. Suleiman Kumchaya.

3. Ben Kiko (Benedict Kikoloma - Homeboy) - Wakati wa vita ya nduli Amin.

4. Leonard Mambombotela???

5. Mchatta (kulikuwa na KM Chadema/Mtangazaji na Refa - Sikumbuki ni yupi).

6. Ni yupi inasemekana aliuawa kwa utapeli miaka ya 80? Jina limenitoka.

7. Mzee Kijaruba Abdallah Mlawa.

8. Mikidadi Mahmoud. (http://www.bongocelebrity.com/2009/03/12/tanzania-rhythm-rtdmikidadi-mahmoud/).

9. Julius Nyaisanga.

10. Sango Kipozi.

11. Charles Hilary.

12. Mshindo Mkeyenge.......

Kama nakumbuka vizuri alikuwa akiitwa Abdul Masoud, alikuwa maarufu katika utangazji wa mpira na kipindi cha michezo.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom