Majembe kuhakiki kumbi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,073
1,250
KAMPUNI ya Majembe Auction Mart imepewa jukumu la kusimamia kuhakiki kumbi zilizopo jijini Dar es Salaam, ambazo hazijasajiliwa zitafungiwa.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lilitoa tamko hilo kupitia Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Bw. Ghonche Materego jijijini Dar es Salaam.

Materego alisema kuwa, imeipa mamlaka Kampuni ya Majembe kuhakiki zoezi zima la kuhakiki kumbi za strehe ambazo hazijasajiliwa na ambazo hazipo katika viwango stahili .

Alisema kuwa tayari wameshaingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni hiyo na itaanza kazi rasmi ili wapatiwe ripoti kwa kuwa zoezi hilo lilikuwa liko jikoni kwa muda mrefu.

Alisema kampuni hiyo ina uzoefu mkubwa na itbaini wale wote wenye kumbi za burudani ambao wanaendesha shughuli hizo kiujanja ujanja bila kusajiliwa na kubaini kumbi ambazo viwango stahili
 

tanga kwetu

JF-Expert Member
May 12, 2010
2,195
2,000
.....huyu mnyalu Mwamoto anatisha kwa netwoking! baada ya daladala sasa yupo kwenye kumbi za 'starehe'? dar kuna kumbi za burudani? watu wanapoza machungu ya maisha na wamiliki wanaganga njaa mbona mnataka kuwasumbua wabongo wenzenu? kama mkitaka kumbi za starehe zote jijini dar zisajiliwe hakya'mungu zitabaki nusu tu ya sasa! hivi hawa BASATA si pia wanahusika kiasi kikubwa na hakimiliki ya wasanii? kule wameishia wapi? si watumie nguvu ku-promote ngoma za asili kuliko kuhangaika na huu ulaji wa Majembe? Tanzania bana!
 

mpenda pombe

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
1,312
2,000
Hapa swala la msingi la BASATA ni kuwasaidia Wasanii na Hakimiliki.. Haya mengine hayana tija..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom