Majembe Action Mart kuvunja sheria za kudai madeni pasipokuwa na order ya mahakama

queen of the jungle

JF-Expert Member
Mar 17, 2017
228
429
Siku hizi kumekuwa na wimbi la notice la kudai deni kutoka Majembe Action kwa niaba ya kampuni fulani na kutoa taarifa za siku kumi na nne ya kuja kukamata mali za mtu pasipokuwa na kibali cha mahakama, yaani kampuni kama linadai kampuni lingine pasipo kupelekana mahakamani basi huwatumia Majembe Action kukudhalilisha kwa kukutolea vitu nje pasipo kuangalia sheria za mikataba na makubaliano ya pande husika.

Mbali na hivyo wamekuwa wakiongeza deni kwa kukutaka kuwalipa wewe mdaiwa wakati sio wewe ulie watuma wala kuzungumza nao muda mwingine inafika mpaka milioni kumi kufuatana na ukubwa wa deni, yaani unadaiwa na mdeni then anakuongezea gharama zingine za kuwalipa majembe pasipo kuwa na makubaliano hayo.

Sasa je nini maana ya sheria za mikataba na uwepo wa mahakama mpaka kuwatuma hawa watu kuja kudhalilisha watu ambao mliingia mkataba kwa kuheshimiana na mwisho wa siku vitu au ofisi hupigwa mnada pasipokuwa na mazungumzo ya wahusika mamlaka husika iko wapi juu ya uvunjifu huu wa haki za binadamu kwa kuwanyimwa haki ya kusikilizwa.

N.B; Naombeni maoni yenu juu ya hii sheria ya kukamata mali za mtu
 
Ka
siku hizi kumekuwa na wimbi la Notice la kudai deni kutoka majembe kwa niaba ya kampuni fulani na kutoa taarifa za siku kumi na nne ya kuja kukamata mali za mtu pasipokuwa na kibali cha mahakama, yaani kampuni kama linadai kampuni lingine pasipo kupelekana mahakamani basi huwatumia majembe kukudhalilisha kwa kukutolea vitu nje pasipo kuangalia sheria za mikataba na makubaliano ya pande husika.

Mbali na hivyo wamekuwa wakiongeza deni kwa kukutaka kuwalipa wewe mdaiwa wakati sio wewe ulie watuma wala kuzungumza nao muda mwingine inafika mpaka milioni kumi kufuatana na ukubwa wa deni, yaani unadaiwa na mdeni then anakuongezea gharama zingine za kuwalipa majembe pasipo kuwa na ,makubaliano hayo

sasa je nini maana ya sheria za mikataba na uwepo wa mahakama mpaka kuwatuma hawa watu kuja kudhalilisha watu ambao mliingia mkataba kwa kuheshimiana na mwisho wa siku vitu au ofisi hupigwa mnada pasipokuwa na mazungumzo ya wahusika
mamlaka husika iko wapi juu ya uvunjifu huu wa haki za binadamu kwa kuwanyimwa haki ya kusikilizwa.

N.B; Naombeni maoni yenu juu ya hii sheria ya kukamata mali za mtu
Kama unadaiwa dawa ni kulipa tu. Unataka Mwenge mahakamani ili ufanye figisu figisu usimlipe mdai wako. Acha hizo bwana.
 
Back
Top Bottom