Majasusi vinara walio itikisa Dunia, na hatma zao

Nimejifunza kitu kikubwa sana hapa. Kwamba kuna majasusi ambao walifuata utashi wao katika kitumiza wajibu kwa jamii badala ya kutumikia nchi ama serikali zao katika mambo ya dhuluma. Wengine kwa ku-behave hivi wamesaidia sana dunia ibaki kuwa eneo salama kwa kuishi.
 
RICHARD SORGE

Jasusi huyu anahesabika kama jasusi mwerevu kuliko wote katika karne ya 20. Jasusi huyo Mrusi na mwalimu wa hujuma alifanya kazi dunia nzima kabla na wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Katika shuguli zote alijifanya mwandishi wa habari za kimataifa, alitembelea sehemu mbalimbali za Ulaya kuangalia uwezekano wa wakomunisti kuleta vurugu.
Wakati Vita ya Pili ya Dunia inaanza alienda nchini Japani akijifanya mwandishi wa habari kutoka Ujerumani ndipo akaanza kupeleka Urusi habari kuhusu silaha na wanajeshi wa Ujerumani na Japani.
Pia, akaonya kuhusu shambulio la Japani katika bandari ya Pearl ( Marekani ), mipango ya Ujerumani kuvamia Urusi, na mengine mengi lakini yote ilikataliwa na Stalin ambaye alikua kiongozi wa Urusi enzi hizo.
Sorge alikamatwa na Wajapani mwaka 1944, ingawa hakuwahi kukiri kama alikua jasusi wa Urusi, alinyongwa muda mfupi baadaye. Warusi hawakuwahi kumpa heshima yake mpaka mwaka 1964, ndipo alipotangazwa kama shujaa.

MATA HARI

Huyu alikua mcheza dansi na muuza mwili wa bei kubwa jijini Paris, Ufaransa ambaye pia alikua jasusi wa Ujerumani wakati wa vita ya kwanza ya dunia.
Jina lake halisi ni Margaretha Geertruida Zelle alizaliwa Uholanzi na alianza kazi za ujasusi baada ya kuwa mfanyakazi wa mahakama akiwakilisha wanasiasa maarufu na wanajeshi wenye vyeo vikubwa .
Kazi zake za kimahakama na uraia wake wa Uholanzi ( kipindi hicho Uholanzi haikua na upande wakati wa vita ), ulimfanya kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuwa jasusi na alipata fursa ya kulala na wanajeshi pamoja na wanasiasa maarufu wa Ufaransa ili kupata siri za kupeleka Ujerumani .
Shuguli za Mata Hari zilifika kikomo Januari 1917, wakati wanausalama wa Ufaransa waliponasa mawasiliano kati ya maofisa wa Ujerumani jijini Paris na Berlin wakikiri kupata taarifa nyingi za kijasusi toka kwa mtu anayeitwa H-21. Mata Hari alitambulika na akakamatwa katika moja ya hoteli jijini Paris Februari 1917. aliuwawa Septemba 1917 kwa kupigwa risasi kwa kosa la ujasusi na hujuma.

JULIUS na ETHEL ROSENBERG

Hawa walikua wanandoa wa Kimarekani waliokua wanafuata siasa za kikomunisti waliouawa mwaka 1953 kwa kosa la kutoa siri kuhusu silaha za nyuklia kwa Urusi kipindi hicho USSR . Ujasusi waliuanza mwaka 1942, wakati Julius alipopewa kazi hiyo na KGB. Alitakiwa kutoa taarifa zote zinazohusu nyuklia kuanzia ramani za mitambo, mabomu, sehemu zilipo wataalamu na nyingine nyingi . taarifa hizo zilisaidia jeshi la Urusi kutungua ndege ya kipepelezi ya Marekani aina ya U-2 mwaka 1960. Alikua anasaidiwa na shemeji yake Sajenti David Greenglass, aliyesaidia kuandika.
Kesi yao ilianza mwaka 1951 na wote wakakutwa na makosa ya kufanya ujasusi na hujuma na waliuawa kwa kupigwa shoti ya umeme katika gereza la Sing Sing. hawa walikua ni Wamarekani pekee kuuawa kwa ujasusi wakati wa vita baridi.

ALDRICH AMES

Jasusi huyu alipewa mafunzo na Shirika la Ujasusi la Marekani CIA kisha kupelekwa Uturuki kuanza kazi mwaka 1985. Alipokua Uturuki alitakiwa ajipendekeze kwa KGB wa Urusi ili wamchukue kisha aanze kutoa siri kwa Wamarekani lakini haikuwa hivyo, alikua na shida ya fedha na maisha ya juu ndipo Warusi walipompatia kwa hiyo akawa upande wa Urusi .
Aldrich Ames aliweza kupata taarifa za majasusi wa Marekani waliokuwepo KGB na katika Jeshi la Urusi kisha kuzipeleka kwa KGB .
Suala hilo lilifanya majasusi 100 wa Marekani kujulikana na wengine 10 kunyongwa. Ames aliweza kukwepa mara 2 kunaswa na CIA lakini tatizo lilikua ni maisha yake ya kifahari na jumba la kifahari alilonunua kwao Marekani na bili kubwa za maongezi ya simu zilizotakiwa kulipiwa na CIA. FBI walimkamata mwaka 1994 na kuhukumiwa kifungo cha maisha.

GUACOMO CASANOVA

Huyu alikuwa jasusi wa Venetia aliyeandika kitabu kinachoitwa; Hadithi ya maisha yangu . Kitabu hicho kinaelezea jinsi alivyofanya kazi zake na mahusiano yake ya kimapenzi na wanawake wengi waliokua matajiri na wenye ushawishi enzi zake. Kinachojulikana ni kwamba alifanya kazi kama mwanasheria, na kuanzia mwaka 1774 – 1782 alifanya ujasusi kwa ajili ya Venetia . shuguli zake zilikua nzuri ila alitimuliwa mwaka 1782 kwa kuunga mkono maasi dhidi ya kiongozi mmoja wa jiji hilo.

KLAUS FLUCHS

Huyu alikuwa ni mwanafizikia mzaliwa wa Ujerumani ni kati ya watu wa kwanza kubuni silaha za kisasa na kuanzisha mradi wa kutengeneza bomu la haidrojeni. Baada ya kutoka ujerumani wakati wa utawala wa NAZI, alianza kufanya PHD yake nchini Uingereza ambapo alianzisha mradi wa kwanza wa bomu la atomiki. Mwaka 1943, alienda Los Alamos, ambapo alikua mshiriki wa mradi wa Manhattan.
Wakati anaishi Uingereza ndipo Warusi walipomshawishi awe mtoa taarifa wao naye alikubali, ndio maana Warusi walijua mpango wa mabomu wa Uingereza na Marekani mapema zaidi. Mtindo wake wa kutoa taarifa kwa Urusi ilichukua miaka 2, walijua kuhusu bomu la Hydrojeni, na kujua Wamarekani wanamabomu mangapi. Alikamatwa na maofisa wa Uingereza mwaka 1946 na kuhukumiwa miaka 14 jela hata hivyo alitumikia miaka 2 tu.

JAMES ARMISTEAD LAFAYETTE

Hapo mwanzo, jasusi huyu alikua mtumwa chini ya William Armistead wa Virginia, alipewa ruhusa ya kujitolea jeshini mwaka 1781. kazi yake ilikua kumpeleleza Brigedia Jenerali Benedict Arnold, na taarifa zake zilikua muhimu sana zilizosaidia kuyashinda majeshi ya Uingereza katika vita ya Yorktown.
Pia, ni jasusi wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika. hakuna mtu wa jamii hiyo aliyewahi kufanya shuguli ya ujasusi kumshinda Lafayette mpaka leo.
Jina la kazi aliitwa Black Panther, jina halisi aliitwa Frederick Joubert Duquesne, alikua jasusi wa Ujerumani katika vita zote mbili za dunia. alichukia kitendo cha majeshi ya Uingereza kutesa watoto na kina mama wa kiBoer, ndipo alipogeukia kwenye hujuma na ujasusi, zaidi alikua anatoa taarifa za silaha na mienendo ya majeshi ya ushirika kwa ujerumani. Kazi yake maarufu zaidi ni ya kulipua na kuzamisha meli inayoitwa HMS Hampshire mwaka 1916 iliyokua inampeleka Kitchener Urusi. Duquesne pia alitengeneza kundi la majasusi 33 ambao walihukumiwa miaka 300 jela.
Wajerumani walimpachika jina la Artemis, lakini jina lake halisi ni Virginia Hall yeye alikua jasusi wa Marekani aliyefanya kazi maalumu miaka ya 1940, kisha akaenda CIA. Kazi zake zinahusisha kusaidia wanaharakati wa ufaransa huko Vichy akiwa kama mwandishi wa habari.
Jasusi huyu alikua na mguu mmoja tu, mguu mwingine ulikatwa kutokana na maradhi ya goti.

SHI PEI PU

Jasusi huyu alikua mcheza dansi na muuzaji wa mwili. alikutana na mfaransa Bernard Boursicot mwaka 1964. Kipindi hicho Boursicot alikua mfanyakazi wa Ubalozi wa Ufaransa nchini China huku akifundisha Kiingereza. Walianza uhusiano uliodumu kwa miaka 20 na hata kujifanya ana ujauzito lakini kumbe alimnunua mtoto katika hospitali moja.
Uhusiano huo ulisababisha Bernard Boursicot kutoa nyaraka 150 za siri kwa usalama wa taifa wa China kabla ya kurudi Ufaransa miaka ya 1980. Shi Pei Pu na mtoto wake walikamatwa na kuhukumiwa miaka 6 jela. waliachiwa huru baada ya miezi 11.

SIDNEY REILLY

Huyu jasusi ndie mtu aliyesababisha kutungwa vitabu na filamu za James Bond, huyu ni jasusi ambaye aliwahi kuishi kipindi fulani katika karne ya 20 huku akifanya kazi katika serikali nyingi. Alijulikana kama “Ace of Spies,” alikua hodari kwa uwongo, Ulaghai, kujipaisha na kujipachika vyeo, kwahiyo taarifa nyingi kuhusu yeye hazieleweki sana.
Lakini inajulikana kwamba aliweza kuvuka mipaka ya nchi nyingi kutumia majina ya watu wengine na kufanikiwa kuiba siri nyingi za jeshi, majengo na ramani za ndege. Pia alikua mtongozaji maarufu maana aliweza kupata wake wengi wa maofisa wa jeshi, wanasiasa na wengine maarufu kulala nao kisha kuchukua siri alizokua anataka.
Kazi yake kubwa aliifanya mwaka 1917 ambapo aliteuliwa na serikali ya Uingereza aende Urusi kuangusha serikali ya Bolshevik lakini ilishindikana , kisha akafanya jaribio la kumuua Vladimir Lenin, lakini kundi lake lilijulikana lakini alifanikiwa kutorokea Finland baada ya kutumia jina la Mjerumani mmoja. Alihukumiwa kifo wakati akiwa mafichoni . mwaka 1925 akadanganywa na dada mmoja kurudi tena Urusi ndipo alipokamatwa . Ingawa hakuwahi kukiri kuwa yeye ni jasusi lakini aliuawa kwa kupigwa risasi.

NATHAN HALE

Huyu anahesabika kama jasusi wa kwanza wa kimarekani , Nathan Hale, alikua mwanajeshi ambaye mwaka 1776 alijitolea kwenda kutafuta habari kuhusu maadui. Wakati huo akiwa na miaka 21 alienda mpaka jijini New York, Marekani ili kupata habari na majeshi ya Uingereza. baada ya jiji hilo kutekwa na waingereza, Hale alikamatwa. kipindi hicho shuguli za kijasusi hazikua rasmi kwahiyo akashtakiwa kwa kufanya shuguli za kijeshi kupitia njia ambazo sio rasmi.
Baada ya siku kadhaa akahukumiwa kunyonywa kabla ya kunyongwa alitamka maneno maarufu ya kukumbukwa ambayo ni ” NINA SIKITIKA KWAMBA NINA MAISHA YA KUIPA NCHI YANGU ” Maneno hayo na shuguli zake zimemfanya kuwa shujaa wa Marekani mpaka leo .
Mpaka leo ukienda Makao Makuu ya Shirika la Ujasusi la Marekani ( CIA ) Utakuta sanamu yake kabla ya kuingia ndani.

KIM PHILBY

Kim Philby alikua jasusi wa Uingereza anayeheshimika sana, alitumwa kwenda Afrika, Hispania, Marekani , Urusi, Uturuki na maeneo mengine ya siri. Lakini wakati wote huo alikua pia anafanya kazi ya kupeleka taarifa za kijasusi kwa KGB walioweka kambi yao katika ubalozi wa Urusi nchini Ufaransa.
Ilipofika mwaka 1950 alitumwa na serikali ya Uingereza kwenda Washington DC Marekani kufanya kazi, kipindi hicho aliiba siri nyingi za silaha, michoro na kuzituma Urusi, kitu ambacho kilichangia vita ya Korea ambayo mwisho wake kukawa na Korea Kaskazini na Kusini.
Uingereza ilishamhisi kama anatumiwa na Urusi haikuweza kuthibitisha hilo, kwahiyo aliendelea kuwa jasusi wa Uingereza mpaka alipokimbilia Urusi mwaka 1963. Aliendelea kufanya shuguli za kijasusi mpaka alipokufa mwaka 1988, ambapo alipewa medali na nishani nyingi na serikali ya Urusi .
Mbona "Dr. Shika" hayupo kwenye list? Au mpaka afe ndio atatambulika?
 
Umemsahau Jasusi mmoja Bora zaidi kuwahi kutoka ktk historia ya ujasusi.si mwingine Ni Eli Cohen Jasusi wa Mossad. Msomeni historia ktk kazi alizofanya halafu linginisha na half wengine mtapata majibu Nani zaidi.
 
Umemsahau Jasusi mmoja Bora zaidi kuwahi kutoka ktk historia ya ujasusi.si mwingine Ni Eli Cohen Jasusi wa Mossad. Msomeni historia ktk kazi alizofanya halafu linginisha na half wengine mtapata majibu Nani zaidi.
Mkuu, aijaweka hiatoria kwaajili ya kufanya uahindani.
Ebu tuwekee hiyo hiatoria ili nasi tujifunze kutoka kwako tafadhali...
 
Jasusi nchi za wenzetu wanapewa heshima lakini hapo bongo utaambulia kusutwa na kuitwa mmbeya mara mnafiki.
Baba Morgan pole, ombea nchi yetu iwe na sheria ya ukomo wa SIRI kuendelea kuwa SIRI, siku moja tutazijua kazi zako
 
Back
Top Bottom