barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,863
Maafisa wa usalama wa Kenya na Tanzania wameanzisha operesheni ya pamoja ya kuwasaka wawindaji haramu wanaoshukiwa kumwuua kifaru mmoja mweusi katika mbuga ya wanyamapori ya Maasai Mara.
Msemaji wa shirika la wanyamapori nchini Kenya (KWS), Paul Udoto, alisema kuwa operesheni hii ilianzishwa baada ya kupata mzoga wa kifaru huyo bila pembe zake karibu na mto wa Sand, mita 300 kutoka kwa mpaka wa Kenya na Tanzania.
"Kutokana na hali ya mzoga, kuna uwezekano kuwa kifaru huyo mwenye umri kati ya 15-20 aliuliwa siku ya Ijumaa, alipokuwa anavuka mpaka wa Kenya na Tanzania kutoka kwa mbuga ya Serengeti ," Uduto alisema katika taarifa yake, mjini Nairobi
Chanzo: China Xinhua News