Majangili wapora Ng'ombe kupeleka Kenya wilayani Handeni

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,556
21,482
1.jpg
Wakati serikali ya awamu ya tano ikiagiza kufanywa haraka kwa zoezi la upigaji chapa ng'ombe wa hapa nchini,kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majangili waliokua na silaha za moto limevamia ranchi za wafugaji wilayani handeni kisha kupora ng'ombe 155 kwa ajili ya kusafirisha katika minada ya mifugo iliyopo mombasa nchi jirani ya kenya.

Katika tukio hilo lililotokea katika eneo la kabuku lililopo wilayani handeni majangili hao walipora ng'ombe hao kisha kuzisafirisha kwa kutumia magari ya mizigo aina ya fusso lakini baadhi ya wachungaji waliokuwa na ng'ombe hao ambao baadhi yao wamejeruhiwa waliwahi kutoa taarifa polisi baada ya kamba walizokuwa wamefungwa za mikononi na miguuni katika pori kuzifungua ndipo operesheni ilipoanza.

Akielezea jitihada walizozifanya ili kuokoa mifugo hiyo kamanda wa polisi mkoani tanga benedict wakulyamba amesema mara baada ya kubaini kua mifugo hiyo inasafirishwa kenya waliweka mitego na kufanikiwa kuwwakamata wasafirishaji wa ng'ombe waliokuwa wakielezea nchini kenya huku wakiwa na mifugo yao ndani ya gari aina ya fusso.

Kufuatia hatua hiyo naibu waziri wa mifugo na uvuvi mheshimiwa abdalla ulega akiwa mkoani tanga mwishoni mwa wiki kisha kuzungumza na afugaji aliopo mpakani mwa kenya na tanzania amewaagiza viongozi wa serikali ngazi za vijiji hadi kata kuhakikisha anasimamia vyema zoezi la upigaji chapa mifugo ili kuzuia uvushaji wa ng'ombe kutoka nchi moja kwenda nyingine sanjari na serikali iweze kupata takwimu halisi za mifugo iliyopo nchini.


ITV
 
Back
Top Bottom