Majanga matano makuu yanayoangusha tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majanga matano makuu yanayoangusha tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by emmanuel1976, Jul 12, 2011.

 1. emmanuel1976

  emmanuel1976 JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukiiangalia kwa makini nchi yetu sasa inakabiliwa na majanga makuu yasiyokuwa na idadi. Mie nitaje matano tu.

  Janga la kwana; suala la udini ambalo limeruhusiwa rasmi katika taifa hili lililojulikana mwanzo kuwa ni taifa lisilo na dini, hata dini zenyewe kwa zenyewe sasa zinakashfiana hadharani huku dola haina majibu.

  Janga la pili ni mtikisiko ama mgawanyiko wa chama tawala ambacho ndicho kinachobeba dhamana ya kuliongoza taifa hili, chama hiki kina mpasuko mkuu sana unaokifanya kishindwe kuendesha ama kusimamia dola, viongozi wake wamebaki kuvutana wao kwa wao.

  Janga la tatu, ni la ufisadi usiotamkika ndani ya vyombo vya dola, rushwa iliyokithili, pamoja na kutowajibika ipasavyo kwa watumishi wa umma.

  Janga la nne ni umaskini unaoongezeka kila kukicha na tofauti kubwa kati ya walionacho na wasiokuwa nacho, na mwisho jnga la tano ni mpasuko ambao unaitwa ufa wa muungano wetu baina ya Tanganyika na Zanzibar... wazanzibar wanataka nchi yao na watanganyika nao wamechoka na malalamika hayo nao sasa wanasema ondokeni.

  Swali langu ni hili, pamoja na mambo mengine je wahusika wanatambua kuwa haya mambo yanatateketeza taifa letu?
   
Loading...