Majambazi yenye silaha za moto yapora Sinza Kumekucha, Kijiweni, White Inn

Mkuu mnamzalilisha mzee Lowasa kwa kutumia picha yake ya akili kuandika mambo yasiyo na akili...kueni basi kidogo.
Ulitaka niandike mambo ya kukufurahisha wewe mkuu mm sio Lumumba buku 3.wameshamaliza kuvamia ma studio wameanza mitaani ni Bashite na vijana wake hao wanaume wa Dar mmepatikana safari hii
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Habari wakuu,

Majambazi yenye silaha za moto na usafiri wa pikipiki usiku huu yametembelea vibanda ya pesa kuk majambazi yakafyatua risasi juu. Nilikuwa nimembeba mwanangu, nilichomoka vibaya sana.

Baada mtu kwa risasi.
Tupo busy kuvamia vituo vya redio, runinga na kugombea front page
 
Police tumewakatisha 'mood'sisi raia, wanakesha kulinda mali zetu na maisha bt from no where police akifa raia tunafurahi unategemea nn hapo! Tufe tu na hata mali zichukuliwe tu na hawa majambazi coz wa tz akili zetu tunazijua wenyewe.

Wafunge basi na hivyo vituo vya polisi na wale wanaovaa nguo nyeupe tusiwaone barabarani, na mwisho kabisa watoe tangazo rasmi kuwa RAIA TUJILINDE WENYEWE..
 
Polisi wanastress ya posho yao ya vinywaji bado hawajapewa!!! Morale imeshake kidogo.....
 
walikuwa wanenda kuteka hao wakamkosa mtekwaji wakaamua kuvamia vibanda
 
majambazi wajanja washajua kuwa polisi skuizi hawana kazi wapo wapo tuuu
 
Pale delux wakati shaba inalia ndio nilikuwa napita, yaani ghafla palikuwa peupe unaona watu wanakimbia tu. Kwa style ile sizani kama majambazi yanaweza kukamatwa coz hakuna raia ata mmoja mwenye ujasiri wa kuwaangalia majambazi wakifanya yao.
 
Police tumewakatisha 'mood'sisi raia, wanakesha kulinda mali zetu na maisha bt from no where police akifa raia tunafurahi unategemea nn hapo! Tufe tu na hata mali zichukuliwe tu na hawa majambazi coz wa tz akili zetu tunazijua wenyewe.
Umesema ukweli mkuuu, lakini sikufichi miongoni mwa watu wapuuzi, washenzi, wanafiki, wakatili, vigeugeu, walinda wezi, wachumia tumbo ni polisi wetu JAPO SI WOTE, kwa miaka mingi sasa polisi wetu hawana maadili yaani inafika hatua nasema bora polisi wasiwepo ili waarifu waneemeke tu, masikini na raia wa kawaida ambao ni wengi na ndo wahitaji misaada kwa polisi hatuna hamu nao, sasa sijui vyuo vya mafunzo suala la kuwafunza maadili na miiko ya kazi zao kama huwa lipo au wanafundishwa tu na kushika mitutu? Polisi ni mojawapo ya sehemu kuu tatu ZILIZO OZA hapa nchini. Heko kwa JWTZ maana wao wanajua wanachokifanya
 
Ukiona mtu amekuja kuiba au kavamia sehemu jua huyo keshaagana na dunia
 
Delux wamechukua ela, na alietoa ela eti kajifanya kuita weziiii.... Akala ya mguu. Wakahamia wait in wamechukua kias chao wakasepa

Ni wamezikusanya kwelikweli
waliamua kukusanya mauzo.. na huku kijichi mida ya sa nane nimesikia mlio sijui ni walifanya tukio huku pia au ni jamaa alimua kutisha wezi
 
Kwa usawa huu wa pombe wakikuchomoa 3m utatamani ufe. Poleni mliokutwa na janga hilo. Polisi fanyeni uchunguzi wa kina kubaini waliofanya uhalifu.
 
Delux wamechukua hela na alietoa hela eti kajifanya kuita weziiii, akapigwa risasi ya mguu. Wakahamia wait in wamechukua kiasi chao wakasepa.

Ni wamezikusanya kwelikweli.
Nilisikia Ambulance ikielekea kijiweni wakati huo nishatoka nduki nipo home. Aisee walisababisha hadi mangi mtaani kafunga duka saa mbili wakati huwa anafunga saa tano usiku
 
Na hapo ndipo utamjua Mtanzania. Akiwa mbele ya keyboard shujaa balaa kumbe hata bastola hajashika mkononi. Hamorapa alitoka mkuu wakati hata risasi haikufyatuliwa. Ingeitika si ajabu angejikojolea. Na angekuwa Hamorapa leo kamalaika hako ka Mungu si ajabu kangetupwa huko halafu akatoka mkuku. Hongera kwa kumlinda mwanao..

Tuna bahati sana Watanzania kwamba mpaka mtu anazeeka na kuaga dunia anakuwa bado hajaisikia risasi ikirindima karibu yake. Kumbe Somalia, Burundi, Libya na kwingineko mpaka walishazoea. Ila tunacheza cheza sana na tusipojiangalia tutafika huko aisee. Mungu na Apishie mbali kikombe hicho...
Asante mkuu, labda nisingekuwa na mtoto ningemng'ang'ania mmoja. Nilicheza kama komando John.
 
Vipi mtoto hakupiga kelele.Mimi ilishatokea majambazi yalivamia sehemu yakapiga risasi kama 10 na kuua mlinzi,nilikua kama mita 20 na mtoto wangu wa miezi 5,alikuwa ni mliaji sana,lakini nilishangaa tokea risasi zimeanza mpaka zimenyamaza hakutoa sauti,
Mtoto alistuka tu wala hakulia.
 
Back
Top Bottom