Majambazi yenye sare za Jeshi la Rwanda yauawa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
49,264
19,595
Majambazi yenye sare za Jeshi la Rwanda yauawa


*Yakutwa na silaha nzito yakiwemo mabomu

Na Esther Macha, Mbeya

MAJAMBAZI watatu yakiwa na sare za Jeshi la Rwanda yameuawa na wananchi wenye hasira wakati yakijiandaa kufanya uhalifu mkubwa, sambamba na kulipua kijiji kwa kutumia bomu la mkono eneo la Kasumulu, Kyela mpakani mwa Tanzania na Malawi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Bw. Zelothe Stephen, alisema watuhumiwa hao wanaosadikiwa kuwa raia wa Rwanda, waliuawa juzi asubuhi walipojaribu kuwapora wafanyabishara wa fedha.

Akielezea tukio hilo, Kamanda Stephen, alisema majambazi hayo yaliwasili stendi mpya ya mabasi mjini Kyela Agosti, 24 saa 2 asubuhi na kukutana na kijana mmoja (jina limehifadhiwa) na kumtaka ayasaidie kubeba mizigo na kuyaelekeza ulipo msikiti ambapo yalikwenda kusali na baadaye kufikia katika nyumba ya kulala wageni ya Kimako.

Alisema siku ya pili yake, yaani Agosti, 25 asubuhi watu hao walielekea mpakani Kasumulu wakiwa na wenyeji wao wawili na kufikia nyumba ya kulala wageni White Stone ambako baadaye walimwagiza mtu aliyetajwa kwa jina la Ras, awatafutie wafanyabiashara wa kubadilisha fedha.

Baada ya Ras kurejea na mtu huyo wakiwa fedha za Malawi, Kwacha 438,050 na kuziweka mezani mmoja wa majambazi hayo alivuta sanduku jekundu na ghafla alifungua na kutoa bunduki aina ya SMG na kuanza kufyatua risasi ovyo kwa lengo la kupora fedha hizo.

Hali hiyo ilizua mtafaruku na kuwafanya Polisi wa kituo kidogo cha Kasumulu kukimbilia eneo hilo kutoa msaada na kufanikiwa kuyazingira na kuyauwa wakati yakijaribu kukimbilia mto Kiwira na Songwe kwenda Malawi.

Alibainisha kuwa majambazi hayo baada ya kuuawa, yalikutwa na sare za Jeshi la Rwanda, ikiwemo mikanda na buti na hati za kusafiria, bomu moja la kutupa kwa mkono na bunduki moja aina ya SMG yenye namba A.362745, magazini moja na risasi 12 za SMG.

Vitu vingine walivyokutwa navyo ni pamoja na bastola moja yenye namba FN-T.348244 Brownings 9MM na magazini yake ikiwa na risasi mbili, simu tatu za kiganjani na laini tatu za mtandao wa simu wa kampuni ya MTN pamoja na tiketi sita za kusafiria kati ya Agosti 20 na 23 mwaka huu.

Kamanda Stephen alisema majambazi hayo yalikutwa na hati mbili za dharura za kusafiria zikiwa na viza ya kutoka Kasumulu, Kyela kuingia Malawi Agosti,25 zikiwa na majina ya Amin Mohamed Sadiki wa sanduku la barua Bukoba, Mkulima, yenye namba AB. 056494 iliyotolewa na Idara ya Uhamiaji ya Isaka Dry Port Agosti 21 mwaka huu.

Hati nyingine ilitolewa kwa mtu aliyetajwa kwa jina la Yalid Harid Suedi wa sanduku la barua Bukoba, Mkulima yenye namba AB. 0596496 iliyotolewa tarehe hiyo hiyo.

Alisema majambazi hayo pia yalikutwa na hati mbili za kusafiria za Rwanda namba RSM 23/9/08 C iliyotolewa kwa jina la Ndagatimana Ferdinand na nyingine namba RSM 1860/07C iliyotolewa kwa jina la Nenziyimana Said.
 
mambo hayo!yale yale ya Arusha ya majambazi kuwa na mabomu sasa ukiambiwa kuna mtu jeshini anawalinda ama ndiye sponsor usibishe!ndiyo haya ya kina Mahita na Mohammed Chiko ambao leo hii wanaponda raha tuu bila hatia zozote zile!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom