Majambazi yatikisa Kijiji cha Bunju, ni mita 100 kutoka Kituo cha police Bunju Usalama

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Katika hali ya taharuki jana majambazi walivamia maduka mawili Bunjua Shule na kupola karibu 6m na simu, katika maduka mawili ya m-pesa , yaliingia na gari dogo corola na kupora baada ya kuwatisha kwa bastora na bunduki kubwa, kabla ya kupora walipiga risasi moja juu, ambayo iliwafanya watu wote wa kwenye mabaa na wapanda pikipiki kukimbia kama swara, wengi wakiwa baa ya Kibira na parking waliingia uvunguni mwa viti na meza. police kama muda wa dakika 5 hivi walifina na kukuta washatokomea. Kibaya zaidi cha kushangaza, police muda wote huwa maeneo hayo kuanzia saa kumi na mbili na nusu pale pembeni mwa baa ya Satori mita kumi kutoka eneo la tukio. nami mara nyingi huwa nawaona na nawafahamu, tunajiuliza walikuwa wapi wakati wa tukio?
 
Hoja yako ni Polisi kutokuwa maeneo hayo au majambazi kuibiwa watu? Acha chuki binafsi na Jeshi letu....

Hoja ni kuripoti, la police kuchelewa katika tukio na kutokuwepo kwa masaa fulani huwa ni kawaida yao , kama wewe ni polisi basi tufafanulie kwa nini mnachelewa sehemu za lindo?
 
Hii ndio Tanzania, watu wanachukua chao mapema.

Watatufanya tuogope kunywa bia usiku kwa mtindo huu

Poleni sana mliofikwa na janga hilo.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Katika hali ya taharuki jana majambazi walivamia maduka mawili Bunjua Shule na kupola karibu 6m na simu, katika maduka mawili ya m-pesa , yaliingia na gari dogo corola na kupora baada ya kuwatisha kwa bastora na bunduki kubwa, kabla ya kupora walipiga risasi moja juu, ambayo iliwafanya watu wote wa kwenye mabaa na wapanda pikipiki kukimbia kama swara, wengi wakiwa baa ya Kibira na parking waliingia uvunguni mwa viti na meza. police kama muda wa dakika 5 hivi walifina na kukuta washatokomea. Kibaya zaidi cha kushangaza, police muda wote huwa maeneo hayo kuanzia saa kumi na mbili na nusu pale pembeni mwa baa ya Satori mita kumi kutoka eneo la tukio. nami mara nyingi huwa nawaona na nawafahamu, tunajiuliza walikuwa wapi wakati wa tukio?
Wengine walikuwa wamejificha mvunguni mwa counter, wengine nao walikimbia kama swala.
Kumbuka nao ni binadamu kama raia, tofauti ni uhuru wa kupiga na kuua raia wema na kupora mali zao ndio tofauti iliyopo kati ya policcm na wadanganyika
 
Ilikuwa saa ngpi?

mnamo saa mbili na nusu, inawezekana ikawa saa tatu maana baada ya milio ya bunduki hakuna wa kukumbuka saa. jamaa aliyeng'ang'ania pesa aliumizwa kweli kweli. We jamaa anayetetea police fuatilia pale Bunju A shule saa 12.30 utakuta askari wa doria , sasa muda huo walikuwa wapi, na police mmoja alisikia mlio mkubwa akaogopa kufika kwani inasemekana alishindwa kujua mlio ni wa bunduki ya aina gani. Kama waendesha boda boda wanavyosema na walioshuudia tukio.
 
Hilo eneo kuna lindo maalum au kunakuwaga na doria za hapa na pale tu?
 
Hii ndio Tanzania, watu wanachukua chao mapema.

Watatufanya tuogope kunywa bia usiku kwa mtindo huu

Poleni sana mliofikwa na janga hilo.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Kweli inasikitisha..Purukushani lote hilo na marisasi kwa tshs milioni sita tu??wanataka kutoa roho za watu??
 
Hilo eneo kuna lindo maalum au kunakuwaga na doria za hapa na pale tu?

Yale maeneo ya bar huwa kuna Difender la Polisi mida ya usiku, na pia zile bar wateja wakubwa ni mapolisi.

Bunju kuna askari Jeshi wastaafu wengi sana, usikute nao walilala chini ya meza na viti badala ya kutumia uzoefu wao wa kijeshi.

Kumbe Wajeshi wetu fujo zao ni kwa raia wasio na slaha, na wakikutana na wanaume wengine wajanja wanalala chini ya meza na viti.

MIZAMBWA
INANIUMA SNA!!!
 
Polen!! Nunueni mishale na nyinyi!
 
Polisi kanda ya kinondoni wanatakiwa waongezewe nguvu ya idadi ya askali na zana,hii ni kuanzia sasa kielekea mwishoni mwa mwaka. Wananchi tutoe ushirikiano kwa jeshi kwa kuwareport haraka watu tunaohisi si wakawaida mitaani mwetu na kwenye sehemu za starehe. Pamoja tunaweza!
 
Back
Top Bottom