mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,767
- 7,115
Katika hali ya taharuki jana majambazi walivamia maduka mawili Bunjua Shule na kupola karibu 6m na simu, katika maduka mawili ya m-pesa , yaliingia na gari dogo corola na kupora baada ya kuwatisha kwa bastora na bunduki kubwa, kabla ya kupora walipiga risasi moja juu, ambayo iliwafanya watu wote wa kwenye mabaa na wapanda pikipiki kukimbia kama swara, wengi wakiwa baa ya Kibira na parking waliingia uvunguni mwa viti na meza. police kama muda wa dakika 5 hivi walifina na kukuta washatokomea. Kibaya zaidi cha kushangaza, police muda wote huwa maeneo hayo kuanzia saa kumi na mbili na nusu pale pembeni mwa baa ya Satori mita kumi kutoka eneo la tukio. nami mara nyingi huwa nawaona na nawafahamu, tunajiuliza walikuwa wapi wakati wa tukio?