Majambazi Yapanga Mawe Na Kupora Manyoni.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majambazi Yapanga Mawe Na Kupora Manyoni..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, Jan 27, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Niliondoka Singida Mjini saa kumi na moja alfajiri kuelekea Dodoma. Kilomita 40 kutoka Manyoni nilikutana na hali hiyo pichani kunako saa kumi na mbili na nusu. Eneo la tukio niliwakuta askari watano wamevalia kiraia wakiwa na silaha za moto. Wameniambia tukio limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya kuanzia saa sita usiku na linawahusisha maja majambazi wasiopungua wanane.

  Kuna walioporwa fedha, simu na mali zao . Mahali hapa kuna pori kubwa upande wa kushoto. Inaaminika majambazi hayo yenye silaha yangali yamejiicha porini.
  Hakuna aliyekamatwa. Nilishuhudia polisi hao wakifuatilia nyayo huku wakinionyesha mahali majambazi hayo yalilala chini kujificha wakisubiri giza na kuanza kupanga mawe yao. Kwa kusoma mazingira ya eneo kwangu mimi napata tafsiri kuwa majambazi hayo yalifanya maandzi ya mpango wao kwa siku kadhaa.

  Maana, mawe hayo mazito yanaonekana kuwa yalikuwa yakisogezwa usiku karibu na tukio na kufikia idadi waliyohitaji. Intelijensia ya kipolisi ingefanya kazi yake sawa sawa na kwa kushirikiana na wenyeji ingewezeza kubaini mapema movement ya mawe yale. Na katika dunia ya sasa , mbwa wa polisi waliopewa mafunzo wangefanya kwa haraka na kwa ufanisi zoezi la kufuatilia majambazi porini badala ya polisi kufuatilia nyayo kwa macho. Angalia picha zaidi; Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  sasa hawa polisi waliambiwa kuwa majambazi wanarudi hapo?intelejensia nyingine ukiziamini zinaweza kukuambia wewe ni wa kike.
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,521
  Likes Received: 5,666
  Trophy Points: 280
  Hahahahaha!
   
 4. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kama sikosei mahali hapo panaitwa Mbwasa. Ni eneo la mlima Nunge, mtindo huo upo sana sehemu hiyo. Majambazi hao wanatoka maeneo ya mbali na hapo.
   
Loading...