Majambazi yaliyoua polisi yakamatwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majambazi yaliyoua polisi yakamatwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Venant Ben, Mar 18, 2011.

 1. Venant Ben

  Venant Ben Senior Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 155
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JESHI la Polisi mkoni Shinyanga likishirikiana na wananchi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wa ujambazi kati ya 10 huku wengine watatu wakiuawa na wananchi wenye hasira, baada ya kuhusishwa na tukio la kuwaua askari wawili katika kituo kidogo cha Kagongwa, wilayani Kahama.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Diwani Athuman, aliyasema hayo jana wakati akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa jeshi lake la kuwatafuta watuhumiwa hao 10 waliotoroka na silaha baada ya kufanya mauaji katika kituo hicho.
  Akizungumza katika kituo kidogo cha Kagongwa wilayani hapa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga alisema kuwa mpaka hivi sasa jeshi lake linawatafuta majambazi wanne waliobaki ikiwemo silaha iliyotoweka.
  Aliwataja wanaotafutwa kuwa ni Kwizela Lionel (26) Mrundi mfanyabiashara mkazi wa Bujumbura nchini Burundi, Ilokoze Willy au maarufu kwa jina la Karumanzira (39) Mrundi dereva Makazi wa Bujumbura Burundi, Simon Mathias au Fred Setty (27) dereva pikipiki mkazi Isamilo Mwanza au Mwenge Dar es Salaam au Moshi mkoani Kilimanjaro na Paulo John Gilioma au Babu (40) mkazi wa Nyasubi Kahama.
  Kamanda huyo wa polisi mkoa wa Shinyanga aliendelea kusema kuwa katika msako ulifanyika katika vijiji vya Iponya, Kishima, Igusule, Motange na Mwalugulu majira ya saa tatu usiku wananchi walitoa taarifa polisi kuwa kuna watu watatu waliokuwa wamejificha katika msitu wa Igusule; huko alikuwa amejificha mtuhumiwa Seleman Mposi huku wengine Kennedy William, Gooluck Leonard au Papaa wakiwa wamejificha katika sehemu nyingine ya msitu huo.
  Aidha, kamanda huyo alisema baada ya wananchi kuwaona walitoa taarifa polisi ndipo walipofika katika sehemu hiyo na kumkamata Seleman Mposi ambaye alianza jitihada za kukimbia hivyo kufanya kulazimika kumfyatulia risasi katika sehemu ya mguuni.
  Pia Emanuel Jackson naye alikamatwa katika maeneo hayo hayo ya msitu huo huku jitihada za wananchi za kusaidiana polisi zikielekea kuzaa matunda baada ya kumkurupusha mtuhumiwa huyo katika msitu huo na kukamatwa tena na polisi.
  Kamanda Athuman alisema mpaka kufikia hivi sasa Emanuel Jackson na John Peter Ngosha wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi huku wakiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama.


  source Tanzania daima+
  Majambazi yaliyoua polisi yakamatwa
  [​IMG]
   
 2. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo huyo paul gilioma nimemfahamu.baba yake alikuwa karani wa mahakama ya mwanzo kahama hivi sasa ni marehemu.
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wameua polisi!watakamatwa woote....
  Na hata kama ikibidi kuwafuata Burundi watafuatwa
   
 4. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Tatizo hapa kwetu tunapenda sana kujisifu na kusolve crisis. Kwa nini hatua hazikuchukuliwa mapema hawa jamaa wasipoteze muda na rasilimali kuwatafuta tena? Ilikuwa rahisi sana au kuimarisha ulinzi kituoni au kuwahamisha kabisa. Inatia simanzi sana kuona kila siku uhalifu wa kutisha unakuwa na mkono wa raia wa kigeni.
  Tumewakamata, sawa, na uhai wa polisi wetu waliokufa? Nani atahesabia? Vipi silaha iliyoporwa? Polisi wetu badilikeni, msipende kutokea daima baada ya maovu kutokea, taarifa za ki-itelijensia hata huku zinatakiwa siyo kwenye maandamano tu!
   
 5. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  .

  Bado sijaona tofauti ya kesi hii na ile ya zombe, naomba munishawishi.
   
 6. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  .

  If you dont mind put in some non spuriousness, tujue chanzo, ni kweli walikamatwa wwakiwa kwenye ujambazi. we may not need to take things so simple.
   
Loading...