Majambazi yakamatwa ndani ya treni yakiwa na silaha za kivita!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majambazi yakamatwa ndani ya treni yakiwa na silaha za kivita!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gudboy, May 6, 2010.

 1. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

  Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu wanne kwa tuhuma ya kupatikana na silaha za mbili za kijeshi aina ya SMG zikiwa na risasi 492 kwenye treni ya abiria iliyokuwa ikitokea Mpanda mkoani Rukwa kuelekea Tabora.

  Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Kamishna Msaidizi Lebelatus Barrow amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Ibrahimu Joseph Mnange maarufu kama Ibra(36), mkazi wa Nyakato mkoani Mwanza na mwanamke pekee Hadija Ibrahim Mtenyi maarufu kwa jina la Bugusi(20) Mkazi wa Nyamongo mkoani Mara.

  Kamanda Barrow, amewataja watuhumiwa wengine kuwa ni Nassoro Said Mohamed maafufu kwa jina la Kalega(31) mkazi wa Kijiji cha Kangeme kilichop katika wilaya ya Urambo mkoani Tabora na Jafari Juma Mohamed maarufu kama Malega(50) Mkaziwa Kijiji cha Lingula Tarafa ya Kaliua pia wilayani Urambo mkoani Tabora.

  Kamanda huyo amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa juzi majira ya saa 5.00 asubuhi na askari waliokuwa wakisindikiza treni hiyo baada ya kuishitukia mizigo waliyoibeba wakati wa safari yao ambapo baada ya kupekuliwa mizigo yao walikuwa wakiwa na silaha hizo moja ikiwa na namba 1966-AFU -3404 na nyingine ikiwa na namba2571 pamoja na Magazine tatu ambapo mbili kati ya kizo kila moja ikiwa imesheheni risasi 30 kila Moja.

  Amesema kua Risasi nyingine zilifungwe wenye mfuko wa Rambo ambapo amesema kuwa watuhumiwa wote wane walikuwa ni Abiria kwenye Behewa NambaTCB 3643 na walipandika katika Stesheni ya Kangeme kwenda Tabora Mjini na walikamatwa baada ya Askari kuwatilia mashaka pamoja na mizigo waliokuwanayo.

  Katika hatua nyingine, Kamanda Barrow amesema Polisi mkoani humo wanamshikilia mkazi mmoja wa kijiji cha Ufuruma wilayani Uyui Omary Musa maarufu kwa jina la Buchonzo( 27), mkazi wa kijiji hicho kwa tuhuma za kupatikana na silaha moja aina ya bastola ikiwa na risasi tano.

  Amesema mtuhumiwa alikamatwa na wananchi wa kijiji cha Ufuruma baada ya kumtishia kumuua mwanakiji mwenzake aitwaye Majaliwa Jumanne(22) Ambaye ni mfanyabiashara akiwa njiani akitokea katika kijiji kingine cha Ugowela kwa Shughuli za kibiashara.
  Kamanda Barrow amewapongeza wananchi wanaoendelea kutoa taarifa kwa Polisi kuelezea juu ya matishio ya kihalifu na kwamba amewataka kuendelea na utaratibu huo na kuwahakikishia kuwa siri zao zitatunzwa kwa usalama wa maisha yao.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,436
  Likes Received: 22,349
  Trophy Points: 280
  Hii ni hatari.
  Hivi kweli tuko salama kiasi gani tunapotumia vyombo vya usafiri.
  Hawa jamaa walikuwa na uwezo wa kuteka behewa zima, na kupora, ikiwezekana kumwaga damu kabisa.
  Kuna haja ukaguzi na upekuzi wa kina ufanyike kwa kila abiria kabla ya safari.
   
 3. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Asikari wetu wamekaa kiuchaguzi zaidi
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Nakumbuka nilipokuwa mdogo tulivokuwa tunasafiria TAZARA askari walikuwa wanakagua mizigo, na wanapekua kila kitu. Sina hakika kama wanaendelea na utaratibu huo. Ila kwa upande wa TRL nadhani hiyo ni ndoto maana abiria ni wengi kaa kwenye daladala na utaratibu mzima ni hobelahobela.
   
Loading...