Majambazi yakamatwa na kumtaja raia mmoja wa Kenya kama bosi wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majambazi yakamatwa na kumtaja raia mmoja wa Kenya kama bosi wao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Feb 13, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Lile wimbi la ujambazi jijini dare s salaam liliendelea jana baada ya majambazi 2 kukamatwa eneo la rombo ( ubungo ) wakijaribu kutorosha gari walilipora maeneo ya mbagara baada ya kumtishia dereva wa gari hilo na silaha
  Walioshuhudia tukio hilo wanasema kwamba baada ya majambazi hayo kufanikiwa kupora gari hilo walianza kuendesha kwa mwendo wa kasi kupita barabara ya morogoro road huku dereva aliyeporwa nae akiwafuata kwa nyuma na gari lingine
  Baada ya kufika karibu na kona ndipo walipoparamia tuta ndipo gari hiyo iliyoibiwa ikagonga gari ya abiria iliyokuwa imepaki katika kituo cha rombo , mmoja wa majambazo hayo anayetambulika kwa jina la juma alifanikiwa kukimbia akiwa na bastola
  Majambazi wengine 2 ndio walifanikiwa kudhibitiwa na wananchi wenye hasira , wananchi hao waliwapiga na kisha kuwapeleka kituo cha karibu cha polisi cha rombo .
  Baada ya kufanyika mahojiano na polisi kituoni hapo mmoja wa majambazi hao alijitambulisha kama seif mkazi wa mbagala alikuwa anafanyakazi katika baa moja aneo hilo mwingine anaitwa kr nae mwenyeji wa huko huko mbagara , wote wana umri wa miaka 19
  Taarifa zilizotufikia baadaye zinasema kwamba watu hao walikiri kutumwa na mkenya mmoja kuiba gari hilo , kituo chao cha kwanza kilikuwa morogoro kisha walipeleke Kenya kupitia Dodoma na Arusha .
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Tunalalamikia miundo mbinu mibovu ya Dar, lakini wakati mwingine ina advantage, kwa mfano kwenye tukio hili lingetokea like Moro...sijui kama wangewakamata hao jamaa. Jambazi akipora gari ktkt ya Dar akitaka kutoka nje ya Dar, lazima apite Ubungo (asilimia kubwa)....so becomes easy to trace them!
   
Loading...