Majambazi ya DRC yaua askari wa Tanzania ziwa Tanganyika, OC-CID apigwa risasi kifuani

Wasije wakawa ni wale askari wanaomtii Brg. Gen. Mozes Ntaganda ambaye anatafutwa na Ocampo.
 
M/Mungu wabariki mashujaa wetu wapone haraka ila nashauri wanajeshi wetu waimarihe ulinzi mipakani
 
Pole kwa makamanda wetu.tunalo la kujifunza hapa.mapigano haya tumetumia askari wetu tunaowaamini yaani Police Force na JWTZ na hawa ndio wataalamu kabisa wa mapigano ya silaha na tunaowategemea tukivamiwa.majeshi yetu hayaandaliwi vizuri na ni aibu kwa kundi kubwa la askari kujeruhiwa namna hii.upo umuhimu wa kuwaandaa askari wetu kulingana na ulimwengu wa sasa.Tunahitaji askari wanaoweza kufikiri vizuri kwenye mazingira ya hatari na ya ghafla na si pupa.Pole kwa wafiwa huyo askari amekufa akimpigania raia aliyeapa kumlinda hata kwa damu yake.
 
utaona macho yatakavyo watoka kisa askali kauwawa lakini huku uraiani watu wanachinjwa kama kuku..

Wewe nawe si Mtanzania nini? hata lugha yako ya Taifa inakushinda kuandika vizuri, ni "askari" sio "askali".
 
Wote wanaendelea vizuri. Wanategemea kusafirishwa kwenda muhimbili leo hii. Wanasubiri ndege ya jeshi. Nimeongea nao wote. Askari wetu mmoja tu ndo aliuawa baada ya kupigwa risasi ya shingo.
 
Wata ripoti wakishasoma humu na wataiita breaking news! hakuna atakaeitaja JF kama source
 
Nimeshasema sana humu, sisi hatuna jeshi, jeshi letu has been corrupted. Ma-askali wetu wanachojua ni kuiba tu kama kina Lt. Gen. Shimbo, lakini kwenyd battle field hakuna kitu, sasa wacha wafundishwe adabu hawa jeshi-ccm...


You are NOT thinking straight! Au hujaielewa taarifa. Level ya utayari kwa vita ilikuwa juu sana pale mpakani, na hii ndiyo maana wote JW na polisi walijua kuna Mtanzania katekwa--ingawa tunahitaji kujua ni mtanzania wa aina gani huyu alikuwa katekwa: je alikuwa askari? je alikuwa raia mvuvi? alikuwa mvusha magendo? alikuwa Mtanzania wa aina gani. Ishu ya utayari imekaa vizuri sana. Naomba usileta kuidhalilisha nchi yetu pasipo sababu ya msingi.
 
Ni imani yangu toka moyoni kuwa jamaa hawa ( askari) wanahusika kwenye mauaji yasiyofuata sheria mara kwa mara hasa pale wanapoua na kutangaza 'majambazi 5 wauawa.....'

Pia hapa utasikia uchunguzi unafanywa haraka sana wkt huko Arumeru wako kimya. Sina imani na askari wetu.:closed_2:
 
Back
Top Bottom