Majambazi wawashangaa Police kwa kuwaacha wakiendelee kutesa tu

BabaH

JF-Expert Member
Jan 25, 2008
704
225
Jeshi la Police linabidi lipitie ushahidi uliotolewa na mashahidi waliokuwa wakitoa ushahidi wao kuhusu kesi ya Zombe
Ebu wanaJF angalie ni kwa jinsi gani police wa tanzania walivyokuwa na mambo yao ya ajabu

Hii inatoka kule majira ndugu zangu


SHAHIDI wa 25 katika kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa Ofisa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Bw. Abdallah Zombe na wenzake; Bw. Shabaan Manyanya amedai kuwa wafanyabiashara wa Mahenge hawakustahili kuuawa bali yeye na wenzake ndio waliostahili kifo hicho.

Alidai mahakamani jana kuwa yeye na wenzake walistahili kuuawa kutokana na kushiriki tukio la uporaji fedha katika gari la kampuni ya Bidco katika barabara ya Sam Nujoma, Dar es Salaam.

Bw. Manyanya alidai hivyo katika Mahakama Kuu ya Tanzania mbele ya Jaji Kiongozi Salum Masati, wakati akitoa ushahidi katika kesi hiyo yenye washitakiwa 13.

Shahidi huyo aliongozwa na wakili wa Serikali Bw. Alexander Mzikila kama ifuatavyo:

Swali: unaishi wapi?
Jibu: Kwa sasa naishi Songea, lakini kipindi cha nyuma nilikuwa naishi Mwananyamala, Dar es Salaam.

Swali: Mwanzoni mwa Januari 2006 kilitokea nini?
Jibu: Nakumbuka kipindi hicho nilifuatwa na rafiki yangu Bw. Grayson na kuniambia kuwa ana biashara fulani ambayo tungeifanya na rafiki yake, Bw. Ally.

Swali: Ulimjibuje?
Jibu: Nilimwambia amlete huyo Ally nijue hiyo biashara na alifanikiwa kumleta na kuzungumza naye, lakini tena niligundua kuwa mhusika mkuu ni dereva wa Bidco anayeitwa Mashaka.

Swali: Nini kiliendelea?
Jibu: Niliongea na Mashaka moja kwa moja na kunieleza kuwa gari lao hufanya biashara ya mafuta na sabuni, ambazo huzisambaza sehemu mbalimbali na jioni hupitia makusanyo ya fedha hivyo alitaka tuibe fedha hizo.

Swali: Mlikubaliana nini?
Jibu: Mimi nilimwambia kuwa huwa situmii silaha ya aina yoyote bali mdomo tu ndiyo silaha yangu, hivyo tulikubaliana tukutane kesho yake ili niwatafute watendaji wangu watakaofanikisha kazi hiyo.

Swali: Uliwapata hao watendaji?
Jibu: Ndiyo niliwapata, akina Kiwalaka, Ramadhan na Mawenga na tulimwita dereva wa gari hilo, ili atoe maelezo ya mwisho na eneo zuri la kufanyia kazi hiyo ambayo alituambia kuwa ni barabara ya Sam Nujoma.

Swali: Mlifanya kazi hiyo?
Jibu: Kazi hiyo ilikwama kama siku mbili mfululuzo, kwani siku ya kwanza dereva alitufahamisha kuwa mzigo wote wamekopesha na siku ya pili mzigo ulipelekwa Zanzibar nako ulikuwa mkopo vilevile.

Swali: Je, Januari 14, 2006 nini kilifanyika?
Jibu: Siku hiyo pia nilijipanga na watu wangu na Mashaka alipiga simu na kutujulisha kuwa mzigo wa siku hiyo ulikuwa wa cash (taslimu) hivyo tujipange kukamilisha kazi hiyo.

Swali: Je mlifanya?
Jibu: Niliwapanga vijana wangu na aliongezeka kibarua mmoja wa Bidco ambaye alikuwa kwa ajili ya kulinda maslahi ya dereva wake, lakini mimi na Bw. Grayson hatukwenda eneo la tukio.

Swali: Nini kiliendelea?
Jibu: Ilipofika jioni nilisikia mlango unagongwa na nilipofungua, niliwakuta wenzangu waliokuwa eneo la tukio na kusema wamemaliza biashara, lakini imekuwa ndivyo sivyo, kwani zilipatikana sh. milioni sita badala ya sh. milioni 36 ambazo waliahidiwa.

Swali: Mlifanya nini?
Jibu: Hapo tulianza 'karata' (kugawana fedha) na tuligawana kulingana na ugumu wa kazi, hivyo mimi nilipata sh. 400,000 tu.

Swali: Nini kiliendelea tena?
Jibu: Kwa upande wangu ilipofika saa mbili tu nilikwenda zangu baa kujipongeza na nikiwa hapo baa alikuja askari Polisi wa Oysterbay kwa jina anaitwa Kulwa Wafoo ambaye aliniuliza kama nimeiba na nilimjibu, ndiyo.

Baada ya hapo nilirudi zangu kulala, lakini alfajiri yake nilisikia mlango ukigongwa, na mke wangu alitoka na kukuta askari ambao walimwambia wananihitaji mimi.

"Niliamka na kuwakuta askari wa Oysterbay ambao ni Henjewele, Gallus, Kulwa na mwingine simjui kwa jina na muda huo walikuwa na Grayson na Mawenga na kunitaka nitoe zile fedha, kwani ametumwa na bosi wao anaitwa Madaraka," alidai.

Swali: Uliwapa hizo fedha?
Jibu: Niliwapa sh. 350,000 na wenzangu walinijulisha kuwa tayari wameshawapatia fedha hizo, hivyo Henjewele alinitaka kuondoka Dar es Salaam mara moja na kwenda mkoani mpaka tukio hilo litakapopoa.

Swali: Uliondoka?
Jibu: Ndiyo nilikwenda zangu Zanzibar na kukaa huko, lakini baada kama ya siku nne hivi, nilimwona afande Zombe akitangaza kuua majambazi waliopora Bidco, tukio ambalo lilinishangaza sana, lakini nilinyamaza tu kwani nilishangaa kwa nini askari hao hao wameua na hao hao wamechukua fedha zetu!

Swali: Ulifanya nini?
Jibu: Nilirudi Dar es Salaam na Rais alipounda Tume ya Mauaji hayo nilikwenda na kutoa maelezo kama haya.

"Nilikwenda kutoa maelezo Tume kutokana na uchungu wa kuuawa watu ambao hawakustahili, kwani tuliotakiwa kuuawa ni mimi na wenzangu tuliochukua fedha hizo," alidai.

Akihojiwa na mawakili wa utetezi ilikuwa kama hivi:

Maira: Kwa nini uko hapa badala ya kuwa gerezani?
Jibu: Waulize polisi kwa nini siko gerezani.

Magafu: Huogopi kukamatwa kwa sasa?
Jibu: Siogopi kwani nilishakamatwa na kunyang'anywa fedha zangu na mimi ni mwizi kama miaka 10 iliyopita na sitaacha mpaka kufa.

Magafu: Ulishawahi kukamatwa?
Jibu: Huwa nakamatwa, lakini namalizana na askari lakini kuhusiana na tukio la Bidco, askari wa Oysterbay walikuwa wanalifahamu.

Shahidi wa 26 Bw. Ramadhan Said (32) aliongozwa na wakili wa Serikali Bw. Angaza Mwipopo na ilikuwa ifuatavyo:

Swali: Unaishi wapi?
Jibu: Mwananyamala Kisiwani.

Swali: Januari 14, 2006 ulikuwa wapi?
Jibu: Nilikuwa nyumbani kwangu na ilipofika saa tano nilifuatwa na Bw. Manyanya na kuniambia ule mpango tayari umekamilik, hivyo tuliondoka hadi Mwenge kituo cha daladala, tukisubiri maelekezo kutoka kwa watu walioko ndani ya gari.

Swali: Nini kiliendelea?
Jibu: Tulipata taarifa kuwa gari hilo linakwenda kushusha mzigo Mabibo hivyo sisi tulipanda teksi na kufuatilia gari hilo mpaka liliposhusha mzigo, baada ya hapo tulielekezwa kulifuata gari hilo mpaka Ubungo, ambako nako lilishusha mzigo.

Swali: Nini kiliendelea?
Jibu: Mmoja wetu aliwasiliana na Mashaka ambaye alisema anaelekea kiwandani na fedha iliyoko ndani ya gari ni sh. milioni sita tu.

"Gari hilo liliondoka na kupitia barabara ya Sam Nujoma ambapo sisi tulifuata na kumpigia honi akasimamisha gari ghafla na sisi tukashuka na kugawanyika, mimi nikiwa kwa 'cashier'ambaye nilimwambia atupe chetu, kutokana na uoga wao walitupa mfuko tukaondoka zetu," alidai.

Swali: Mlielekea wapi?
Jibu: Tulielekea Mwananyamala, tukakutana na wenzetu tukagawana hizo fedha na mimi nilichukua sh. 1,070,000 nikaachana na wenzangu,

Swali: Nini tena kiliendelea?
Jibu: Nilikuja kukamatwa na askari wa Oysterbay ambao ni Madilu na Abeya, ambao mwisho wao walitaka niwape sh. 200,000 lakini sikuwapa, kwani tayari Henjewele alishachukua sh. 400,000 hivyo niliwabembeleza mpaka sh. 40,000.

Shahidi wa 26 Mrakibu Mwandamizi Masinde Sebastian (54) ambaye alikuwa Mkuu wa Kituo cha Chuo Kikuu aliongozwa na Mugaya Mutaki na ilikuwa ifuatavyo:

Swali: Januari 14, 2006 ulikuwa wapi?
Jibu: Nilikuwa Chuo cha Diplomasia na nilirudi saa mbili usiku.

Swali: Ulipata taarifa gani?
Jibu: Nilipewa taarifa na Koplo Omary kuwa kuna majambazi wamekamatwa wakiwa na bastola na sh. milioni tano.

Swali: Januari 15, 2006 ulikuwa wapi?
Jibu: Nikiwa kazini kwangu nilipata taarifa kutoka kwa Afande Zombe kupitia 'radio call' ambayo ilinitaka kwenda na vijana wangu.

Swali: Je, ulikwenda nao?
Jibu: Ndiyo nilikwenda nao na tulipofika tulimkuta Zombe katika ofisi ya Tibaigana (Alfred) na wakuu wa vituo wote walikuwapo.

Swali: Nini kiliendelea?
Jibu: Alitueleza kuwa vijana wamepambana na majambazi na kuwakamata wakiwa na bastola na sh. milioni tano, hivyo akatutaka kuandika mapendekezo ya kupandishwa vyeo vijana hao.

Swali: Je mlifanya hivyo?
Jibu: Tuliweka kama rekodi tu ili siku kikitokea kitu cha namna hiyo, tuangalie ni kijana gani anatakiwa kupanda cheo kutokana na alichokifanya.

Swali: Nani mwingine alikuwa na vijana wake?
Jibu: Christopher Bageni wa Oysterbay alikuwa na vijana wake na Ahmed Makele naye alikuwa nao na mimi.

Washitakiwa katika kesi hiyo wanadaiwa kuwa Januari 14, mwaka juzi wakiwa katika msitu wa Pande Luisi ulioko Mbezi, Dar es Salaam, walimuua kwa makusudi Bw. Ephraim Chigumbi, Bw. Sabinus Chigumbi, Bw. Juma Ndugu na Bw. Mathias Lukombe.

Washitakiwa hao ni Bw. Zombe, Bw. Bageni, Bw. Makele, F5912 Noel Leonard, WP4513 Jane Andrew, D6440 Nyangerella Moris, D1406 Mabula, E6712 Felix, D8289 Michael, D2300 Abeneth, B1321 Rashid Lema, D4656 Rajab Bakari na D1367 Festus Gwabisabi.
 

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,951
2,000
Kwa hali hii ya rushwa, kazi ipo. Polisi anapomfuata jambazi kwenda gawana ngawira na vilevile kumshauri apotee hadi hali itakapotulia, tumekwisha!!!! Waziri Masha upo!!!!???
 

Nemesis

JF-Expert Member
Feb 13, 2008
4,732
2,000
mambo haya nimekuwa nikiona maigizo ya akina ze comedy, Onyango, vituko mahakamani, Ice Cube nk. kumbe huwa vinatokea mahakamani ki kweli kweli loh! mi ningekuwepo hapo mahakamani ingenilazimu kuondoka ili nisiwekwe ndani kwasababu ya kucheka kwa nguvu.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,961
2,000
Huyo shahidi wa 25 mimi ningempa hata Uwaziri!! Kwa sababu ni mtu pekee aliyekubali kusema "mimi ni mwizi na nimekuwa nikiiba kwa miaka 10 na sitaacha daima"...
 

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,327
2,000
hii spirit isipite bila kupongezwa....! ushauri wangu ni kuwa na wengine ambao wametenda maovu (EPA,KIWIRA,RICHMOND,etc) waige mfano wa hawa nasi tuwapongeze na tusiwalaumu........!
"....... ITAFUTENI KWELI.....NAYO KWELI ......ITAWAWEKA HURU....."
ILA WASAIDIWE KUFUTA KAULI YAO KUWA HAWATAACHA WIZI......!
 

Zion Train

JF-Expert Member
Jun 5, 2008
503
195
baadhi ya hao mashahidi wamenena, kwamba wamejisikia uchungu sana baada ya kuona wao ndiyo walioiba, lakini wameuliwa wengine, kwangu mimi ni kitendo cha kishujaa sana.hivi ni viongozi wangapi ambao wanaiba mapesa ya wananchi na wanauzulia katika misiba ya hao wananchi waliowibia pesa zao ambao wamekufa kwa kukosa ka panadol tu na hata aibu hawaoni?
 

P. Mwainunu

New Member
May 22, 2008
3
0
Tanzania haina utawala wa sheria, inaumiza na ni mbaya lakini tulipofikishwa Watanzania bora na hili Jeshi la mafisadi nalo lingejaribu kuchukua nchi sote tukacharazwa viboko, wakianzwa watawala au viongozi wa mafisadi hata kwa miaka mitano tu ndio tutashika adabu nchi hii. Inauma lakini ni heri kuliko ilivyo
 

Ibambasi

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
8,361
2,000
Huyo Mwizi/Shahidi naamini kama angekuwapo enzi za Yesu nadhani ni sawa na yule Mama Mgoni aliyekamatwa na kuletwa kwa Yesu au pia yule Mfarisayo aliyesimama nyuma kabisa ya sinagogi na kusema "mimi mdambi nihurumie".

Bottomline ni kuwa huyu bwana hajawa mnafiki.
 

Masaki

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,464
1,250
Huyo shahidi kaamua kufa na Zombe maana lazima Zombe aliwanyanyasa sana kipindi akiwa madarakani. Yaani mnaiba, halafu polisi wanakuja mpaka nyumbani kisha mnagawana pesa, au wanachukua zote!!! Inatisha sana!! Halafu negotiations zilikuwa zinaruhusiwa, yaani kutoka shs. 350,000 mpaka shs. 40,000 kweli jeshi letu la polisi linatia kinyaaa!!!!
 

Zanaki

JF-Expert Member
Sep 1, 2006
545
195
Hii story nimesoma nimecheka ile mbaya...haswa pale alipomfukuza yule polisi kwenye bar.Nakumbuka kuna wakati nilikuwa naongea na rafiki yangu mmoja polisi na akawa anasema kila akisikia kwenye radio call jambazi au majambazi wameuawa na polisi,wakifika kwenye tukio wanakuta wale majambazi mifuko yao iko inside out,yaani wamepekuliwa na polisi! Sasa hivi ndio naanza kujiuliza hivi wangapi kati ya hao walikuwa ni raia wema tu.
Lakini lazima tujiulize what the hell is going on! Mwizi anasema yeye ni mwizi na ataendelea kuwa mwizi...na huyu mizi polisi wanamjua na walimfuata na akawafukuza.Raia wema wameuawa kikatili na watu waliokula kiapo kuhahakisha usalama wao na mali zao!
 

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,958
2,000
Kwa hali hii ya rushwa, kazi ipo. Polisi anapomfuata jambazi kwenda gawana ngawira na vilevile kumshauri apotee hadi hali itakapotulia, tumekwisha!!!! Waziri Masha upo!!!!???
tatizo hapo mama mdogo ni mshahara mdogo wanao lipwa pamoja na nyumba chakavu wanazo ishi askari wetu.Hata ukiwa wewe huwezi kukataa fweza za ubwete 400000 wkt mshahara wako 90,000/= kwa mwezi na unafamilia ndani unasomesha ndugu kijijini wanakuangalia wewe hujavaa n.k lazima utapokea tu na kula deal la nguvu.
 

Tuandamane

JF-Expert Member
Feb 2, 2008
1,221
1,195
Kwa hali hii ya rushwa, kazi ipo. Polisi anapomfuata jambazi kwenda gawana ngawira na vilevile kumshauri apotee hadi hali itakapotulia, tumekwisha!!!! Waziri Masha upo!!!!???
Mama MDogo,

Na wezi wa EPA ndivo hivohivo waliambiwa
 

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,603
2,000
Nimeamini hakuna jiwe litakalo achwa bila kugeuzwa.Tukitaka kuiponya nchi yetu basi tuwe wakweli kama hawa jamaa,kwa ukweli huu nchi za wenzetu zingewapa ushauri maalumu ili waishi maisha safi.
Mimi nauliza swali,hawa polisi wa Kituo cha O`bay wanaposoma uoza huu bado wanaendelea kuvaa sare na kwenda kazini?
 

Tuandamane

JF-Expert Member
Feb 2, 2008
1,221
1,195
tatizo hapo mama mdogo ni mshahara mdogo wanao lipwa pamoja na nyumba chakavu wanazo ishi askari wetu.Hata ukiwa wewe huwezi kukataa fweza za ubwete 400000 wkt mshahara wako 90,000/= kwa mwezi na unafamilia ndani unasomesha ndugu kijijini wanakuangalia wewe hujavaa n.k lazima utapokea tu na kula deal la nguvu.

wanaipenda hiyo hali bwana, kama wangekuwa hawaipendi wasingekuwa wanawalinda hao viongozi wezi wao kazi yao kulala mika chini chini tuu... they should do something ili viongozi wajue wanachokitaka... we fikiria walipoifungua JF na walivosingizia kuwa ni magaidi... hapo utasema hawaipendi hali yao ya uchumi kweli
 

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,958
2,000
wanaipenda hiyo hali bwana, kama wangekuwa hawaipendi wasingekuwa wanawalinda hao viongozi wezi wao kazi yao kulala mika chini chini tuu... they should do something ili viongozi wajue wanachokitaka... we fikiria walipoifungua JF na walivosingizia kuwa ni magaidi... hapo utasema hawaipendi hali yao ya uchumi kweli
ndo hapo ninapo choka kwa hiyo wameridhika.Lakini wanapata fidia kwa kuwatorosha watuhumiwa namna hii kesho wewe au mm tukiibiwa sijui itakuwaje bila kukata cha mtu mtuhumiwa utamwona anadunda uswazi kama kawa.
 

Tuandamane

JF-Expert Member
Feb 2, 2008
1,221
1,195
ndo hapo ninapo choka kwa hiyo wameridhika.Lakini wanapata fidia kwa kuwatorosha watuhumiwa namna hii kesho wewe au mm tukiibiwa sijui itakuwaje bila kukata cha mtu mtuhumiwa utamwona anadunda uswazi kama kawa.
Hapo wanashangaa nini wananchi wanapochukua sheria mikononi
 

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,693
1,250
mh hapa huyu mwizi anatoa siri kwa sababu aliporwa pia na waporaji wa raia wa nchi hii.
Kinacho nishangaza ni usemi bila kificho kuwa amekuwa anaiba kwa miaka 10 na hataacha maisha yake yote???????!!!!!!! na hapa tumsaidie vipi? maana is a next victim wa kifo asipoacha wizi.
 

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,156
2,000
mwizi.jpg

Mmoja wa mashahidi katika kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abdallah Zombe na wenzake, Bw. Shaban Manyanya, akiwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam, baada ya kutoa ushahidi wake jana. (Picha na Peter Twite).

View attachment 1673
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,862
1,250
Kwa hali hii ya rushwa, kazi ipo. Polisi anapomfuata jambazi kwenda gawana ngawira na vilevile kumshauri apotee hadi hali itakapotulia, tumekwisha!!!! Waziri Masha upo!!!!???
Unamuuliza Masha juu ya hili wakati na yeye ana yake ? Ama umesahau kuna mjadala hapa ? Tofauti ni kwamba wale wanatumia silaha na hata kuua Masha anaua pole pole huku kavaa suti .Nina maana ya yeye na Kampuni kuwa katika ufisadi .By the way Masha kesha fungua ile kesi iliyo vuma hapa siku za nyuma kwamba anaenda kufungua ?
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
100,404
2,000
Kwa hali hii ya rushwa, kazi ipo. Polisi anapomfuata jambazi kwenda gawana ngawira na vilevile kumshauri apotee hadi hali itakapotulia, tumekwisha!!!! Waziri Masha upo!!!!???
waziri Masha atakuwepo naye yumo ndani ya chama cha mafisadi? Nchi haina mwenyewe!!! Inasikitisha sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom