Majambazi wavamia nyumba,waambulia elfu 3

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
48,770
102,123
Habari zilizonifikia hivi sasa ni kwamba huko katika kijiji cha Nsimbo Kaliua majambazi watatu wenye silaha za moto wamevamia nyumba ya kadhaa na kupora mali na fedha

Katika nyumba moja majambazi hayo yamefanikiwa kuambulia pesa taslim Shilingi elfu tu. Muadhirika ameeleza chanzo changu kwamba majambazi yalimlazimisha kwa kumuwekea bunduki kichwani awapatie pesa zote alizonazo. " Niliwaeleza wazi kuwa sasa hivi hali ni ngumu,biashara hazitoki,ninayo elfu 3 tu"

Majambazi hayo yenye silaha yalichukua fedha hizo na kuvamia nyumba zingine
 
Ha ha ha hii kweli walivamia mtaani kwetu walianzia madukani wakachukua hela, wakahamia kwenye migahawa alie na maandazi...mikate walibeba...wengine maandazi walikua wanayala hapo hapo nilicheka sanaaa nikasema kweli vyuma vimebana!!
ahaaaa wapi huko tena jamani?
 
yaani unaibiwa ila wakiondoka unacheka tu buku 3 mtu anasepa nayo tena bila wasiwasi kama umeficha nyingine maana anajua huna
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom