Majambazi watatu wameuawa jijini Dar es Salaam

Hivi risasi 300 ni nyingi au Mimi ndio sielewi?
Aina ya silaha ni SMG... Magazini yake moja full loaded yaani ikiwekwa risasi full inakuwa na risasi 30!!

Apo taarifa ya polisi inasema waliwakuta na magazini kumi (10) ina maana 10 x 30 = 300 risasi

Japo ni jambo la kutisha sana yaani mtu ambaye sio askari anamiliki magazini kumi za SMG!! Inabidi hao jamaa wachunguzwe vizuri..
 
Screen-Shot-2016-08-22-at-3.28.16-PM.png

Majambazi watatu wameuwawa jijini Dsm huku mmoja wao katika eneo la mabibo na kukutwa na Magazini kumi zenye risasi mia 300 za Bunduki aina ya SMG pamoja na bomu huku majambazi wengine wanne wakitoroka baada ya kurusha bomu la mkono.

Kamishna wa Polisi kanda Maalum dsm CP Simon siro amesema tukio hilo limetokea alfajiri ya kuamkia leo ambapo vijana wapatao hamsini waliwaitilia mashaka watu watano waliokuwa wamebeba mabegi ambayo ndani yake kulikuwa na silaha.

Jeshi hilo limeanzisha msako mkali dhidi ya majambazi wengine wanne wanaosadikiwa kuwa na bunduki za SMG na kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa ili kufanikishwa kutiwa mbaroni kwa majambazi hao.

Katika tukio lingine kinara wa wizi wa vifaa vya magari Salum Issa Hassan mfabiashara eneo la kariakoo anashikiliwa na jeshi hilo baada ya kukutwa na vifaa vya wizi vilivyoibwa katika magari zaidi ya 300 zikiwemo,sight Milla,taa.Vioo pamoja na Vitasa vya magari.

Katika kukabiliana na tishio la Operesheni Ukuta jeshi hilo limefanikiwa kumkamata mfanyabiashara Yoram Sethy Mbyela akiwa na fulana zaidi ya 200 zenye maneno ya Uchochezi kuhamasisha maandamano ya Ukuta na Hapa anatoa onyo.
Huyu jamaa ni mfanyabiashara wa Tunduma, yeye ndio msambazaji mkuu wa bidhaa za Chadema hapa Tunduma.

Pole yake.!
 
Daaah!!Hatimaye Salumu Mpemba muuza vifaa vya wizi kakamatwa?Lakini atatolewa kesho tu huyo!!Anajuwa sana kula na Polisi

Hugo mtu apelekwe management na afungwe miaka minhi sana. Ameharibu sana ustaaranu we DSM
 
Mungu anisamehe tu, lakini kuelekea Sept mosi, siwezi kushangaa ikiwa hizi taarifa ni mojawapo ya sarakasi......sijui ni kwa nini nazitilia mashaka sana!
 
Mi naomba kuuliza jambazi ni mtu gani? Je ni raiya wa kawaida anaeweza kutumia SMG au mafunzo ya matumizi ya kutumia hiyo yanatokea wapi tofauti na jeshini au mafunzo ya uaskari.. Na yale makampuni ya ulinzi je ?

Hata mafunzo vijana wanayopata JKT nayo yanachangia kujua jinsi ya kutumia silaha.
 
Ifike wakati polisi itumie hawa watu kujua mianya ya uingizaji holela wa silaha nchini, tofauti na hapo tutakwisha.
 
Screen-Shot-2016-08-22-at-3.28.16-PM.png

Majambazi watatu wameuwawa jijini Dsm huku mmoja wao katika eneo la mabibo na kukutwa na Magazini kumi zenye risasi mia 300 za Bunduki aina ya SMG pamoja na bomu huku majambazi wengine wanne wakitoroka baada ya kurusha bomu la mkono.

Kamishna wa Polisi kanda Maalum dsm CP Simon siro amesema tukio hilo limetokea alfajiri ya kuamkia leo ambapo vijana wapatao hamsini waliwaitilia mashaka watu watano waliokuwa wamebeba mabegi ambayo ndani yake kulikuwa na silaha.

Jeshi hilo limeanzisha msako mkali dhidi ya majambazi wengine wanne wanaosadikiwa kuwa na bunduki za SMG na kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa ili kufanikishwa kutiwa mbaroni kwa majambazi hao.

Katika tukio lingine kinara wa wizi wa vifaa vya magari Salum Issa Hassan mfabiashara eneo la kariakoo anashikiliwa na jeshi hilo baada ya kukutwa na vifaa vya wizi vilivyoibwa katika magari zaidi ya 300 zikiwemo,sight Milla,taa.Vioo pamoja na Vitasa vya magari.

Katika kukabiliana na tishio la Operesheni Ukuta jeshi hilo limefanikiwa kumkamata mfanyabiashara Yoram Sethy Mbyela akiwa na fulana zaidi ya 200 zenye maneno ya Uchochezi kuhamasisha maandamano ya Ukuta na Hapa anatoa onyo.
Chini ya utawala wa Dr Magufuli tutalala milango wazi....
 
Kodi juu>kazi zinapungua>vijana wanapunguzwa kazi>vijana wanazagaa mtaani> matukio ya UKABAJI NA UPORAJI yanaongezeka ktk kila pembe yanchi.
 
aiseee hongereni sana jeshi la polisi, nyie ni makamanda, hao waliobaki wasakeni mpaka wapoteane.
 
Hii habari ya hili tukio,itakua polisi wameamua kutengeneza tu ili kutisha watu kisiasa... haiingii akilini majambazi wenye SMG risasi 300 na mabomu ya kutupa, eti wakathibitiwe kwenye mapambano na raia walio mikono mitupu...

Halafu eti kabla ya kurusha bomu alikuwa akipiga Takbiiiiir
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom