MAJAMBAZI wamemchinja mlinzi wa duka la dhahabu katika Mtaa wa Misheni, Kata ya Kalan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAJAMBAZI wamemchinja mlinzi wa duka la dhahabu katika Mtaa wa Misheni, Kata ya Kalan

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 11, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MAJAMBAZI wamemchinja mlinzi wa duka la dhahabu katika Mtaa wa Misheni, Kata ya Kalangalala, wilayani Geita, na kupora masalia ya mchanga wa madini hayo.Mlinzi huyo, Bw. Fikiri Bundala (27) mkazi wa Kijiji cha Kamena
  aliuawa katika tukio hilo lililotokea jana usiku katika duka hilo linalomilikiwa na Bw. Martine Mwanageni.

  Hadi sasa hakuna taarifa zilizopatikana kutoka polisi, lakini Mganga wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Geita, Dkt. Patrick Bulugu, aliyeufanyia uchunguzi mwili wa mlinzi huyo, alisema kuwa alikufa kutokana na jereha kubwa la kuchinjwa shingoni na kitu chenye makali kama panga na kupoteza damu nyingi.

  Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kalangalala, Bw. Hamadi Hussein, alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo alilosema kuwa ni la kusikitisha.Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi habari, Wakurugenzi wa duka hilo, Bw. Martine Mwanageni na Bw. Kilabasa Muhinda walisema kuwa kuuawa kwa mlinzi huyo kumegundulika baada ya kufika dukani hapo.

  "Tumebaini kuuawa kwa mlinzi wa duka letu mara tulipofika hapo asubuhi, na hapo huwa tunapatumia kuchambulia na kuchomea dhahabu kabla ya kuingizwa katika mfumo wa duka la Sonara tunalolimiliki sisi wenyewe," Alisikika akisema mmoja wa wamiliki hao.
   
Loading...