Majambazi wakamatwa Kigoma na Mzigo wa risasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majambazi wakamatwa Kigoma na Mzigo wa risasi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Amigo, Sep 28, 2011.

 1. Amigo

  Amigo Senior Member

  #1
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kg.jpg


  Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wamekamatwa na wanashikiliwa na Polisi Mkoani Kigoma wakiwa na risasi 1,200 za silaha za kijeshi aina ya SMG wakizisafirisha kwenda Mpanda mkoani Rukwa.

  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma Mratibu
  Mwandamizi wa Polisi SSP Kihenya Mzulwa Kihenya, amewataja watuhumiwa waliokamatwa wakiwa na risasi hizo kuwa ni Chamtu Tunugu(43) mkazi wa Kibande wilaya ya Kasulu na Ismail Mateo(43) mkazi wa Mlole Kigoma Vijini.

  kamanda Kihenya amesema kuwa watuhumiwa hao┬ů

  Pardon Mbwate, wa Jeshi la Polisi Kigoma

  Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wamekamatwa na wanashikiliwa na Polisi Mkoani Kigoma wakiwa na risasi 1,200 za silaha za kijeshi aina ya SMG wakizisafirisha kwenda Mpanda mkoani Rukwa.

  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma Mratibu
  Mwandamizi wa Polisi SSP Kihenya Mzulwa Kihenya, amewataja watuhumiwa waliokamatwa wakiwa na risasi hizo kuwa ni Chamtu Tunugu(43) mkazi wa Kibande wilaya ya Kasulu na Ismail Mateo(43) mkazi wa Mlole Kigoma Vijini.

  kamanda Kihenya amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa jana majira ya saa 7:00 mchana huko kwenye pori la Uvinza mkoani humo wakielekea katika pori la Mishamo wilayani Mpanda maeneo ambayo yanaishi wakimbizi wa Burundi.

  Amesema kuwa Askari Polisi wakiwa katika Operesheni maalumu ya kupambana na uhalifu ukiwemo wa ujambazi wa kutumia silaha na wahamiaji haramu walipata taarifa za kuwepo kwa watu hao katika pori hilo na hivyo na ndipo walipowaona na kufukuzana nao hadi kuwakamata na kiasi hicho cha risasi.

  Hiyo ni mara ya tatu kwa Polisi mkoani Kigoma kukamata kiasi kikubwa cha risasi za bundiki za kijeshi aina ya SMG ambapo mara ya kwanza zilikamatwa risasi 1,858 na mara ya pili zilikamatwa 2,200 na kufanya risasi ambazo zimekwishakamatwa hadi sasa kufikia 5,258.

  Kamanda huyo amesema bado Polisi wanaendelea na intelijensia kujua zinakotoka risasi hizo na watu wanaoziingiza na kwamba wanatafuta kujua mahala palipo na silaha zinazotumia risasi hizo.

  Katika hatua nyingine, Polisi kikosi cha Usalama barabarani mkoani Kigoma wamekusanya zaidi ya shilingi 810,000 katika kipindi cha siku mbili kati ya Septemba 25 na 26 ikiwa ni makusanyo ya faini za papo kwa papo kwa madereva wasiozingatia taratibu, sheria na kanuni za Usalama barabarani.

  Jeshi la Polisi mkoani humo limeendelea kutoa wito kwa kuendeleza juhudi za kuwafichua wahalifu ili waweze kukamatwa na kukabiliana na mkoano wa sheria.

  Aidha Kamanda Kihenye amewataka Madereva na Wamiliki wa vyombo vya moto yakiwemo Mabasi ya Abiria mkoani humo, kuhakikisha kuwa magari yao yapo katika hali ya usalama na yenye viwango vya ubeba abiria kwa mujibu wa sheria.

  Amewataka wale wote wenye leseni za zamani kuharakisha kuzibadilisha na kupata leseni mpya ili kuepuka usumbufu wa kukamatwa na Polisi kwa kutokuwa na leseni inayokubalika kimataifa
   
Loading...