Majambazi waiba nembo ya Taifa la Tanzania! Masaaa "72" yatumika kuwasaka! Inasidikiwa viongozi wa wazito wahusika kupanga njama!

winnerian

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
335
530
1107541

Kutokana na mwenendo wa siasa za Tanzania katika nembo yetu Taifa letu la Tanzania ni dhahiri kabisa vyama vyetu vya siasa husasani vile vikongwe vimeanza kuiba nembo yetu ya Taifa

1. Uhuru - uhuru wetu upo mashakani kutokana na kile kinachoendelea sasa. Sheria mbovu zinatungwa, watu wanawekwa vizuizini kwa kutoa mawazo yao, mikataba inaingiwa na wachache bila kushirikisha wengi, wachache wanazidi kuneemeka kanakwamba tunatumia mfumo wa kifalme. Nisikuchoshe nafahamu unajua hali ya Taifa lako.

2. Umoja - Siasa zimeacha mwelekeo wa kuliunganisha Taifa liwe moja, kama Baba wa Taifa Mwl. Nyerere alivyolitengeneza yeye; zimelenga zaidi ukanda na uitikadi. Kama wewe sio wa chama kile au hiki basi unaonekana adui, unoanekana mwizi jambazi, unaonekana mkaskazini au mkusini au mkanda wa ziwa. Ukivaa nguo ya rangi fulani unaonekana sio Mtanzania mwema, unaonekana mtu wa fujo, unaonekana fisadi mkubwa na mwizi wa kutupwa. Kama wewe ni mfanyabiashara na unamapenzi ya chama fulani basi lazima matatizo yakukumbe na makubwa zaidi hata kufungwa kifungo kirefu.

#KUNA KILA DALILI YA NEMBO YA TAIFA KUIBIWA NA KUPELEKWA KUSIKOJULIKANA
#UHURU NA UMOJ

Uzalendo wa kweli hauna chama,
Uzalendo wa kweli hauna dini
Uzalendo wa kweli hauna kanda
Uzalendo wa kweli hauna rangi
Uzalendo wa kweli hauna lugha

Kemea wizi huu ewe Mtanzania.
 
Back
Top Bottom