Majambazi sita yauawa Biharamulo

Gwataimbwa

JF-Expert Member
Sep 15, 2014
342
123
Inasemekana majambazi sugu sita yauawa biharamulo mjini mwenye taarifa atujuze.
======================
Jeshi la Polisi mkoani Kagera limewauwa majambazi sita waliokuwa wanapanga kuteka mabasi.
10433843_654342624676715_4806544554963766339_n.png

Jeshi la Polisi mkoani Kagera limefanikiwa kuwauwa majambazi sita waliokuwa wanapanga kuteka mabasi katika eneo la ngazi saba wilayani Biharamulo.

Akizungumza mkoani Kagera kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Henri Mwaibambe amesema jeshi la Polisi lilipata taarifa ya kwamba kunakundi la majambazi linafanya mpango wa kuteka magari na kufanya uporaji katika eneo la ngazi saba wilayani Biharamulo ambapo jeshi hilo lilifanya doria na kufanikiwa kuwauwa majambaizi sita.

Kamanda Mwaibambe ameongeza kuwa kati ya majambazi hao sita ni mmoja tu aliyetambulika kwa jina Gahungu Gerad raia wa Burundi na wengine watano bado hawajafahamika.

Hata hivyo kamanda Mwaibambe ametoa onyo kwa wahalifu mbalimbali kwa kuwataka waache kabisa kufanya vitendo vya uhalifu kwani serikali inamkono mrefu wakiutawala na kwamba jeshi la Polisi sasa limeimarisha ulinzi katika mapori ya Kasindaga na Biharamulo kwa lengo la kudhibiti majambazi wanao ingia kutoka nchi jirani za Rwanda, Burundi na Uganda.

Chanzo:ITV
 
Halafu hawana hatia innocent! je wezi waliokwapua bil mia tatu za escro maiti zao zitatambulia muhimbili lini nasi tukaangalie kama kutakuwa na ndugu zetu!
 
Matukio ya ujambazi nchini yamezidi kushika kasi, lakini sita kati ya watu wanaojihusisha na matukio hayo wamejikuta wakikatishwa maisha baada ya kuchakazwa kwa risasi hadi kufa wakati wa mapambano na askari wa jeshi la polisi huko Biharamulo mkoani Kagera.

Hayo yamethibitishwa na Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso aliyesema kwamba, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi, majira ya saa saba.

Alisema, siku ya tukio wananchi wema walitoa taarifa polisi kuwa, kuna majambazi 6 walikuwa wamesuka mpango wa kufanya utekaji wa magari ya abiria na yale ya mizigo yanayopita katika eneo la pori la Bwanga.

Kutokana na taarifa hizo, askari walivamia pori hilo na kujikuta wakipambana kwa kurushiana risasi na majambazi hao ambao wote walifia katika eneo la mapambano.

Polisi walifanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na risasi 180 zilizokuwa zinamilikiwa na majambazi hao ambao hata hivyo hawajaweza kufahamika mara moja.

Tukio hilo lilitokea siku moja baada ya mtu anayesadikiwa kuwa ni jambazi, Bhoke Mohere kumpiga risasi na kumuua askari Polisi mwenye namba F. 4268, D/C Pendo aliyekuwa katika utekelezaji wa majukumu ya kikazi kwenye kijiji cha Genkuru wilayani Tarime.

Askari huyo alikwenda kumkamata Mohere nyumbani kwake kwa kosa la unyanganyi wa kutumia silaha na kumiliki silaha isivyo halali. Baada ya mauaji hayo, muuaji huyo alifanikiwa kutoroka.

"Hali hii inaonesha ni jinsi gani askari polisi wanafanya kazi katika mazingira hatarishi, pamoja na kwamba wanakuwa wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata matakwa ya sheria, lakini kuna mahali wanakutana na mazingira ya watu wabaya wanaokaidi kutii sheria, hali inayowalazimu polisi nao kutumia nguvu kumdhibiti mhalifu," amesema Senso.

Kutokana na matukio hayo, ameiomba jamii kuongeza ushirikiano katika kutokomeza vitendo vya uhalifu nchini.

Aidha, amewataka wananchi wanaomiliki silaha bila ya kibali kuendelea kuitikio wito wa kuzisalimisha kwa hiyari, kabla ya kuanza kwa operesheni maalumu baada ya Oktoba 31 mwaka huu.

Chanzo: Magangaone
 
Halafu hawana hatia innocent! je wezi waliokwapua bil mia tatu za escro maiti zao zitatambulia muhimbili lini nasi tukaangalie kama kutakuwa na ndugu zetu!

...nanyi nendeni mkaibe hile mitambo iliyowekezwa pale IPTL! kuliko kuwatesa raia wema, ambao ni walala hoi..

"ASANTE SANA WOTE MLIOSAIDIA KUANGAMIZA HAO MAJAMBAZI"

"nawapongeza kwa kazi mzuri ya ulinzi shirikishi"
 
Matukio ya ujambazi nchini yamezidi kushika kasi, lakini sita kati ya watu wanaojihusisha na matukio hayo wamejikuta wakikatishwa maisha baada ya kuchakazwa kwa risasi hadi kufa wakati wa mapambano na askari wa jeshi la polisi huko Biharamulo mkoani Kagera.

Hayo yamethibitishwa na Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso aliyesema kwamba, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi, majira ya saa saba.

Alisema, siku ya tukio wananchi wema walitoa taarifa polisi kuwa, kuna majambazi 6 walikuwa wamesuka mpango wa kufanya utekaji wa magari ya abiria na yale ya mizigo yanayopita katika eneo la pori la Bwanga.

Kutokana na taarifa hizo, askari walivamia pori hilo na kujikuta wakipambana kwa kurushiana risasi na majambazi hao ambao wote walifia katika eneo la mapambano.

Polisi walifanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na risasi 180 zilizokuwa zinamilikiwa na majambazi hao ambao hata hivyo hawajaweza kufahamika mara moja.

Tukio hilo lilitokea siku moja baada ya mtu anayesadikiwa kuwa ni jambazi, Bhoke Mohere kumpiga risasi na kumuua askari Polisi mwenye namba F. 4268, D/C Pendo aliyekuwa katika utekelezaji wa majukumu ya kikazi kwenye kijiji cha Genkuru wilayani Tarime.

Askari huyo alikwenda kumkamata Mohere nyumbani kwake kwa kosa la unyanganyi wa kutumia silaha na kumiliki silaha isivyo halali. Baada ya mauaji hayo, muuaji huyo alifanikiwa kutoroka.

“Hali hii inaonesha ni jinsi gani askari polisi wanafanya kazi katika mazingira hatarishi, pamoja na kwamba wanakuwa wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata matakwa ya sheria, lakini kuna mahali wanakutana na mazingira ya watu wabaya wanaokaidi kutii sheria, hali inayowalazimu polisi nao kutumia nguvu kumdhibiti mhalifu,” amesema Senso.

Kutokana na matukio hayo, ameiomba jamii kuongeza ushirikiano katika kutokomeza vitendo vya uhalifu nchini.

Aidha, amewataka wananchi wanaomiliki silaha bila ya kibali kuendelea kuitikio wito wa kuzisalimisha kwa hiyari, kabla ya kuanza kwa operesheni maalumu baada ya Oktoba 31 mwaka huu.

Chanzo: Magangaone

...thx!
na mkoani hapa Arusha POLISI IMEFANIKIWA kumuua kinara namba mbili wa ujambazi wa kuua na kupora wanawake, Wecensilaus Matei(32), maarufu Mandela, Jacob au Star.
 
Back
Top Bottom