Mr.Professional
JF-Expert Member
- Oct 4, 2010
- 1,582
- 258
Tukio la hivi punde la jamaa yangu wa karibu kuvamiwa na majambazi na mkewe kubakwa limezua majonzi makubwa ndani ya familia hiyo. Mwezi kama mmoja uliopita rafiki yangu alivamiwa na majambazi ambao walichukua mali nyingi lakini hawakuishia hapo kwani walimbaka mkewe pia!
Baada ya kukaa kwa wiki tatu jamaa na mkewe wakiwa na machungu makubwa wanapata machungu mengine pale wanapoenda kupima na kuambiwa mke ameambukizwa virusi vya ukimwi.
Jamaa huwa tunashauriana mambo mengi hivyo akanitonya juu ya majibu kutokana na maswahiba yaliyowakuta na anakaniomba ushauri "Je aendelee na mahusiano na mke wake wakati mke tayari ni muathirika na yeye ni mzima?" Ila anachosema anampenda mke wake kupika maelezo.
Wanajamvi hebu nisaidieni mawazo hawa ndugu wafanye nini ili kusiwe na mfarakano na familia isitengane kwani wanapendana hata mie ni shahidi.