Majambazi Kuua watu 14 Mwanza; Waziri Masha jiuzuru!

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,813
11,123
Mbiu ya kila siku ya CCM ilikuwa ni kujivunia utulivu na amani miongoni mwa watz,lkn leo hii watz wanauawa kila siku na majambazi bila mikakati yeyote endelevu toka serikalini hasa wizara ya Mambo ya ndani ya nchi kuwalinda watz wasio na hatia!

Tumevumilia sana,tumevumilia toka mauaji ya kutisha ya albino hadi vifo vya watz maelfu vitokanavyo na madereva wazembe lkn kwa hili la majambazi bila uoga kuua watu 14 huko Sengerema-Mwanza tunasema sasa basi!

Tuwe na hulka ya kujizuru kama likitokea kosa kubwa kwenye nafasi zetu za kazi,kumbuka uongozi ni dhamana na kuwajibika ni sehemu ya uongozi uliotukuka!

Masha jiuzuru kwani umeshindwa kazi; serikali isiyoweza kuwalinda watu wake haifai kuwepo madarakani! Kumbuka Rais mstaafu Mwinyi alijizuru nafasi hii kwenye miaka ya 70 kwa sababu tu ya mauaji ya vikongwe huko Shinyanga.
 
Na serikali hiyo hiyo inafahamu kuwa kuna magenge ya kihalifu katika visiwa vya ziwa Victoria na baadhi ya vikundi hivyo vinafadhiliwa na wafanya biashara maarufu wa Mwanza na Mara ambao ukifika ktk ofisi zao utakuta wametundika picha walizopiga na viongozi wakuu wa Serikali wakiwa katika harambee mbalimbali za kuchangia.

Habari za vikundi hivyo zimeripotiwa sana siku za nyuma bila hatua zozote kuchukuliwa, ilifikia wakati baadhi ya visiwa vikawa na utawala wao na serikali ikabaki kimya tuu. Haya sasa ni matokeo ya kimya hicho na Waziri muhusika anapeta tuu.
 
Mbiu ya kila siku ya CCM ilikuwa ni kujivunia utulivu na amani miongoni mwa watz,lkn leo hii watz wanauawa kila siku na majambazi bila mikakati yeyote endelevu toka serikalini hasa wizara ya Mambo ya ndani ya nchi kuwalinda watz wasio na hatia!

Tumevumilia sana,tumevumilia toka mauaji ya kutisha ya albino hadi vifo vya watz maelfu vitokanavyo na madereva wazembe lkn kwa hili la majambazi bila uoga kuua watu 14 huko Sengerema-Mwanza tunasema sasa basi!

Tuwe na hulka ya kujizuru kama likitokea kosa kubwa kwenye nafasi zetu za kazi,kumbuka uongozi ni dhamana na kuwajibika ni sehemu ya uongozi uliotukuka!

Masha jiuzuru kwani umeshindwa kazi;serikali isiyoweza kuwalinda watu wake haifai kuwepo madarakani!Kumbuka Rais mstaafu Mwinyi alijizuru nafasi hii kwenye miaka ya 70 kwa sababu tu ya mauaji ya vikongwe huko Shinyanga.

Tungepata mwana JF ambaye kafika kisiwa kile angetuhabarisha, ila nilishawahi kusikia kuhusu kisiwa hiki kwamba ni hatari sana, kuna kila ufilauni kule, ubabe mtupu. hiki ni kisiwa kinachokaliwa na wavuvi katika ziwa victoria.

Huko hakuna sheria kama zetu, kuna sheria zao wenyewe, nasikia hata ukienda na mkeo jamaa anaweza kumchukua na usifanye chochote. kuna kasino kule za kikwao na sheria zake.

Mwana JF hasa wa ukelewe au mwanza anaweza kutuhabarisha zaidi kuhusu kisiwa hiki kilichojitangazia Jamhuri yao huru na bendera. Kwa ufupi kule hakuna serikali wala kituo cha police.
 
Jamani, lakini mnawaonea majambazi, nahisi kwakuwa na wao hawajapata fedha za ufisadi, wanakusanya manoti ya kampeni 2010 kwani madaraka yatauzwa kipindi hicho. Kama hatupambani na ufisadi na uongozi mbaya, rushwa, na tunaacha viongozi wafanye wanavyotaka, basi na majambazi nao tuwaache. Kwani madhara ya jambazi ni kuua watu kumi, lakini ufisadi unaua mamilioni ya watu, hivyo nadhani tumuache Masha kidogo, kwani inawezekana ndio sera za taifa kwa sasa. Ukiambiwa wanataka kupunguza umasikini ni pamoja na kuua masikini, au ufahamu masikini wakifa ndio tumepunguza umasikini? Ukishindwa kuwapa watu maisha bora, wape changamoto kama za ujambazi na ufisadi ili bongo zao zifikiri jibu.

Unajua Watanzania ni wavivu wa kufikiri, wanaogopa ujambazi wakati nchi iko kwenye tetemeko na imepoteza uelekeo. Majambazi wanawashitua ni jinsi gani jamii imeanza kuchoka. Msipulize moshi bali zimeni moto. Hivi ni nini kimewashitua, ujambazi au kumuacha Mzungu achukue madini yetu na kuua watu kwa sumu Nyamongo na Waziri wa Madini anapeta? Je, huu si unafiki kumfukuza Waziri kwa ajiri ya watu kumi na kumwacha aliyesababisha maelfu kufa?

Kijana, ila una wazo zuri la uwajibikaji, lakini si unafahamu viongozi wamenunua madaraka. Je, wewe ukitaka kuvunja nyumba yako, jirani atakuzuia? Ngojeni 2010 ili muwauzie madaraka wengine wenye pesa zaidi ya viongozi wa sasa, ili wapate kuvuna kipindi cha miaka mingine 5. Kumbuka "Silence is argument carried out by other means."

Nakukumbusha, uwajibikaji au kujiuzuru si kitu kinachotokea kama tunda linaloanguka likiwa bado mbichi. Lazima ulivune. Kwa hiyo, wananchi wakiwa tayari katika kuwawajibisha viongozi, nao viongozi watatambua kama wakifanya kosa watatakiwa kujitajirisha wenyewe. Lakini bila wananchi kutambua, si ajabu Waziri akatoka hadharani na kuwaita wanaotaka awajibike ni wehu.

Changamoto ni kutumia 2010 vizuri. Huwezi kumfukuza kifaranga wa bata kabla ya kumkamata bata mwenyewe. Kumbuka, maamuzi ya Tanzania yatafanyika kama ifuatavyo:

Wanaunga mkono Masha aondoke waseme ndiooooo

Wasiounga mkono Masha aondoke waseme sioooo

Waliosema sioooooooo wameshinda.
 
Mbiu ya kila siku ya CCM ilikuwa ni kujivunia utulivu na amani miongoni mwa watz,lkn leo hii watz wanauawa kila siku na majambazi bila mikakati yeyote endelevu toka serikalini hasa wizara ya Mambo ya ndani ya nchi kuwalinda watz wasio na hatia!

Tumevumilia sana,tumevumilia toka mauaji ya kutisha ya albino hadi vifo vya watz maelfu vitokanavyo na madereva wazembe lkn kwa hili la majambazi bila uoga kuua watu 14 huko Sengerema-Mwanza tunasema sasa basi!

Tuwe na hulka ya kujizuru kama likitokea kosa kubwa kwenye nafasi zetu za kazi,kumbuka uongozi ni dhamana na kuwajibika ni sehemu ya uongozi uliotukuka!

Masha jiuzuru kwani umeshindwa kazi;serikali isiyoweza kuwalinda watu wake haifai kuwepo madarakani!Kumbuka Rais mstaafu Mwinyi alijizuru nafasi hii kwenye miaka ya 70 kwa sababu tu ya mauaji ya vikongwe huko Shinyanga.
Ni Sengerema au Ukerewe?
Hii ni aibu kubwa kwa nchi inayojivunia amani na utulivu, mimi naona ingefaa serikali nzima ijiuzuru kwa kushindwa kulinda amani!
 
Nani alisema Tanzania kuna kalcha ya kujiuzulu? Kama ipo, tungeanza na serikali za kijiji, kata, tarafa, wilaya, na mkoa, ndipo tufike kwa Masha, kwani kiutawala ni kamati ya ulinzi ndiyo ingewajibika kabla ya Waziri.

Hivi si kuna maafisa usalama kila kona ya Tanzania na wanakula pesa yetu? Maneno haya si ya kumsafisha Masha bali ni kuweka mambo sawa tu.
 
jamani lakini mnawaonea majambazi nahisi kwakuwa na wao hawajapata fedha za ufisadi , wanakusanya manoti ya kampeni 2010 kwani madaraka yatauzwa kipindi hicho, kama hatupambani na ufisadi na uongozi mbaya, rushwa na tunaacha viongozi wafanye wanavyotaka basi na majambazi nao tuwaache> kwani madhara ya jambazi ni kuua watu kumi lakini ufisadi unaua mamilioni ya watz so nadhani tumuache masha kidogo kwani inawezekana ndio sera za taifa kwa sasa, ukiambiwa wanataka kupunguza umasikini ni pamoja na kuua masikini au ufahamu masikini wakifa ndio tumepunguza umasikini? ukishindwa kuwapa watu maisha bora wape changamoto kama za ujambazi na ufisadi ili bongo zao zifikiri jibu, unajua watanzania ni wavivu wa kufikiri wanaogopa ujambazi wakati nchi iko kwenye tetemeko na imepoteza uelekeo, majambazi wanawashitua ni jinsi gani jamii imeanza kuchoka, msipulize moshi bali zimeni moto, hivi ni nini kimewashitua ujambazi au kumuacha mzungu achukue madini yetu na kuua watu kwa sumu nyamongo na waziri wa madini anapeta je huu si unnafiki kumfukuza waziri kwa ajiri ya watu kumi na kumwacha aliyesababisha maelfu kufa,
kijana ila una wazo zuri la uwajibikaji lakini si unafahamu viongozi wamenunua madaraka, je wewe ukitaka kuvunja nyumba yako jirani atakuzuia, ngojeni 2010 ili muwauzie madaraka wengine wenye pesa zaidi ya viongozi wa sasa ili wapate kuvuna kipindi cha miaka 5 mingine kumbuka "Silence is argument carried out by other means"
nakukumbusha Uwajibikaji au kujiuzulu is not an apple that falls when it is ripe. You have to make it fall. kwa hiyo wananchi wakiwa tayari katika kuwawajibisha viongozi nao viongozi watatambua kama wakifanya kosa watajiwajibisha lakini bila wananchi kutambua si ajabu waziri akatoka hadharani na kuwaita wanaotaka awajibike ni wehu
chamsingi ni kutumia 2010 vizuri uwezi ukamfukuza kifaranga wa bata kabla ya kumkamata bata mwenyewe.
kumbuka mahamuzi ya tz yatafanyika kama ifuatavyo
wanaunga mkono masha aondoke waseme ndioooooooooooooooooooooooo
wasiounga mkono masha aondoke waseme siooooooooooooooooooooooooo
waliosema sioooooooooooooooooo wameshinda

Inaelekea wewe unadamu ya kijambazi
 
Ni Sengerema au Ukerewe?
Hii ni aibu kubwa kwa nchi inayojivunia amani na utulivu, mimi naona ingefaa serikali nzima ijiuzuru kwa kushindwa kulinda amani!

Sahihisho ni Wilaya ya Ukerewe Kwa mama Mongela na nyumbani kwa Makamu Mwenyekiti Taifa wa CCM na Spika aliyepita Pius Msekwa

Kuna habari toka huko zinasema kuwa Polis wanachojua wao ni kufuatilia tu dili za magendo,na wakiambiwa kuna jahazi zimebeba mali za magendo huwa wanajazana ufukweni kuzisubiri ili "wazishughulikie"lkn kwenye majambazi "labda sio kazi yao"

Masha unasubiri nini kujiuzuru hadi sasa baada ya watu zaidi ya 16 kufa kwenye shambulio la ujambazi??
 
nani alisema tanzania kuna kalcha ya kujiuzulu? kama ipo tungeanza na serikali za kijiji, kata, tarafa, wilaya na mkoa ndipo tufike kwa masha kwani kiutawala ni kamti ya ulinzi ndiyo ingewajibika kabla ya waziri... hivi si kuna maafisa usalama kila kona ya tanzania na wanakula pesa yetu???

maneno haya si ya kumsafisha masha bali ni kuweka mambo sawa tu
Only Great Thinker Ali Hassan Mwinyi did and can do this
 
Masha akijiuzulu mimi narudisha passport yangu uhamiaji na kujiondoa ktk orodha ya watanzania wa asili
 
Only Great Thinker Ali Hassan Mwinyi did and can do this
Mkuu wako wachache sana... pia kuna mrema, mwandosya (aliacha ile wizara ya JK na kurudi chuo) labda na mimi na wewe tunaweza kuachia hivi vikazi vya majasho... lakini sio viongozi wetu... tena hasa tuliowachagua kwa kura
 
nani alisema tanzania kuna kalcha ya kujiuzulu? kama ipo tungeanza na serikali za kijiji, kata, tarafa, wilaya na mkoa ndipo tufike kwa masha kwani kiutawala ni kamti ya ulinzi ndiyo ingewajibika kabla ya waziri... hivi si kuna maafisa usalama kila kona ya tanzania na wanakula pesa yetu???

maneno haya si ya kumsafisha masha bali ni kuweka mambo sawa tu

kujiuzuli piga ua ajiuzulu mtu hiyo ndo tanzania zaidi ya uijuavyo
 
Masha akijiuzulu mimi narudisha passport yangu uhamiaji na kujiondoa ktk orodha ya watanzania wa asili

pole msanii

nini kurudisha pass ataukitoa uhai wako ajiuzulu mtu mkuu we vumilia tu ipo siku isonajina mungu ata leta neema ya kweli
 
Rafiki yangu, imeshindikana kujiuzulu kutokana na mabomu ya mbagala ambayo ni uzembe wa wazi halafu atajiuzulu mtu kwa ajili ya hili? Siyo rahisi. Kwanza Masha mwenyewe alishakufa siku nyingi. tunasubiri mazishi tu. Yeye huwa anasikika kwenye vitambulisho vya taifa tu kwa kuwa huko kuna 10% haya mengine yeye hayamhusu.
 
pole msanii

nini kurudisha pass ataukitoa uhai wako ajiuzulu mtu mkuu we vumilia tu ipo siku isonajina mungu ata leta neema ya kweli
Utaisubiri siku hiyo hadi uhai utakutoka bila kuiona. Neema na mabadiliko ya nchi hii yataletwa na sisi wenyewe (Raia) tukiamua kufanya hivyo. Mwenyezi Mungu alishajitoa kwenye hilo baada ya kupata haki yetu ya kikatiba kuweka madarakani uongozi kwa kura. TUAMUE SASA
 
ajiuzulu KWA HILI TU?......kwanza halina COST IMPLICATION!

AMESEVU LA VITAMBULISHO ajiuzulu kwa hili?

NAH!...
 
nani alisema tanzania kuna kalcha ya kujiuzulu? kama ipo tungeanza na serikali za kijiji, kata, tarafa, wilaya na mkoa ndipo tufike kwa masha kwani kiutawala ni kamti ya ulinzi ndiyo ingewajibika kabla ya waziri... hivi si kuna maafisa usalama kila kona ya tanzania na wanakula pesa yetu???

maneno haya si ya kumsafisha masha bali ni kuweka mambo sawa tu

Hakika tunahitaji mwanzo mpya; na huu utaletwa na watanzania wenyewe - kwa ujumla wao. Pindi kila mtu atakapofahamu haki yake, na ni kwa nini yupo; hakika mambo yatabadilika. Kwa hali ilivyo hivi sasa ya nchi kuendeswa na viongozi kana kwamba wanawafanyia hisani wananchi; mambo hayawezi kwenda.
 
Kimbweka, naona unawaogopa majambazi zaidi. Tanzania tunaitajika kujenga misingi uhuru wa kutoa mawazo. Je, unafahamu ya kuwa watu wanaojihusisha na ujambazi ni watumishi wakubwa wa jeshi la polisi? Na je, unafahamu ya kuwa Tanzania ni nchi ya 86 kwa ujambazi duniani? Lakini je, umejaribu kufanya tafiti madhara ya ujambazi, ukosefu wa dawa mahospitalini, wizi kwenye sekta ya umma, na upotevu wa fedha katika mikataba ya madini?

Kwa mfano, Alex Stewart pekee analipwa shs bilioni 11 kwa mwaka, wakati gharama zake za uendeshaji ni shs bilioni 5. Je, uoni ujambazi anaoufanya ni mkubwa zaidi? Lakini je, Waziri wa Madini anafanya nini? Watanzania wamezoea wameshindakushambulia matokeo na si kutafuta chanzo. Kwa hiyo, lazima tuanze kupambana na vitu vyenye hatari zaidi na kuvifanya ni vipao mbele.

Kwa mfano, tukiweza kuleta malezi bora kwa watu wetu, tutapunguza ujambazi. Na tukiongeza ajira za watu wetu pia tutapunguza ujambazi. Kwa hiyo, Rais na Waziri wa Ajira wao ndio wangekua wa kwanza katika kujiuzuru na si kushambulia matokeo.

Naweza kuwauliza Watanzania: Wanaunga mkono Masha aondoke waseme "ndio." Wasiounga mkono Masha aondoke waseme "sio." Waliosema "sio" wamewazidi wa "ndio." Lakini cha msingi ni misingi ya utawala bora na utendaji, na si mtu binafsi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom