Majambazi Kuua watu 14 Mwanza;Waziri Masha jiuzuru! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majambazi Kuua watu 14 Mwanza;Waziri Masha jiuzuru!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malafyale, Jan 18, 2010.

 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,210
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Mbiu ya kila siku ya CCM ilikuwa ni kujivunia utulivu na amani miongoni mwa watz,lkn leo hii watz wanauawa kila siku na majambazi bila mikakati yeyote endelevu toka serikalini hasa wizara ya Mambo ya ndani ya nchi kuwalinda watz wasio na hatia!

  Tumevumilia sana,tumevumilia toka mauaji ya kutisha ya albino hadi vifo vya watz maelfu vitokanavyo na madereva wazembe lkn kwa hili la majambazi bila uoga kuua watu 14 huko Sengerema-Mwanza tunasema sasa basi!

  Tuwe na hulka ya kujizuru kama likitokea kosa kubwa kwenye nafasi zetu za kazi,kumbuka uongozi ni dhamana na kuwajibika ni sehemu ya uongozi uliotukuka!

  Masha jiuzuru kwani umeshindwa kazi;serikali isiyoweza kuwalinda watu wake haifai kuwepo madarakani!Kumbuka Rais mstaafu Mwinyi alijizuru nafasi hii kwenye miaka ya 70 kwa sababu tu ya mauaji ya vikongwe huko Shinyanga.
   
 2. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,659
  Likes Received: 21,878
  Trophy Points: 280
  Na serikali hiyo hiyo inafahamu kuwa kuna magenge ya kihalifu katika visiwa vya ziwa Victoria na baadhi ya vikundi hivyo vinafadhiliwa na wafanya biashara maarufu wa Mwanza na Mara ambao ukifika ktk ofisi zao utakuta wametundika picha walizopiga na viongozi wakuu wa Serikali wakiwa katika harambee mbalimbali za kuchangia.
  Habari za vikundi hivyo zimeripotiwa sana siku za nyuma bila hatua zozote kuchukuliwa,ilifikia wakati baadhi ya visiwa vikawa na utawala wao na serikali ikabaki kimya tuu. Haya sasa ni matokeo ya kimya hicho na Waziri muhusika anapeta tuu.
   
 3. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Tungepata mwana JF ambaye kafika kisiwa kile angetuhabarisha, ila nilishawahi kusikia kuhusu kisiwa hiki kwamba ni hatari sana, kuna kila ufilauni kule, ubabe mtupu. hiki ni kisiwa kinachokaliwa na wavuvi katika ziwa victoria.

  Huko hakuna sheria kama zetu, kuna sheria zao wenyewe, nasikia hata ukienda na mkeo jamaa anaweza kumchukua na usifanye chochote. kuna kasino kule za kikwao na sheria zake.

  Mwana JF hasa wa ukelewe au mwanza anaweza kutuhabarisha zaidi kuhusu kisiwa hiki kilichojitangazia Jamhuri yao huru na bendera. Kwa ufupi kule hakuna serikali wala kituo cha police.
   
 4. G

  Godwine JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  jamani lakini mnawaonea majambazi nahisi kwakuwa na wao hawajapata fedha za ufisadi , wanakusanya manoti ya kampeni 2010 kwani madaraka yatauzwa kipindi hicho, kama hatupambani na ufisadi na uongozi mbaya, rushwa na tunaacha viongozi wafanye wanavyotaka basi na majambazi nao tuwaache> kwani madhara ya jambazi ni kuua watu kumi lakini ufisadi unaua mamilioni ya watz so nadhani tumuache masha kidogo kwani inawezekana ndio sera za taifa kwa sasa, ukiambiwa wanataka kupunguza umasikini ni pamoja na kuua masikini au ufahamu masikini wakifa ndio tumepunguza umasikini? ukishindwa kuwapa watu maisha bora wape changamoto kama za ujambazi na ufisadi ili bongo zao zifikiri jibu, unajua watanzania ni wavivu wa kufikiri wanaogopa ujambazi wakati nchi iko kwenye tetemeko na imepoteza uelekeo, majambazi wanawashitua ni jinsi gani jamii imeanza kuchoka, msipulize moshi bali zimeni moto, hivi ni nini kimewashitua ujambazi au kumuacha mzungu achukue madini yetu na kuua watu kwa sumu nyamongo na waziri wa madini anapeta je huu si unnafiki kumfukuza waziri kwa ajiri ya watu kumi na kumwacha aliyesababisha maelfu kufa,
  kijana ila una wazo zuri la uwajibikaji lakini si unafahamu viongozi wamenunua madaraka, je wewe ukitaka kuvunja nyumba yako jirani atakuzuia, ngojeni 2010 ili muwauzie madaraka wengine wenye pesa zaidi ya viongozi wa sasa ili wapate kuvuna kipindi cha miaka 5 mingine kumbuka "Silence is argument carried out by other means"
  nakukumbusha Uwajibikaji au kujiuzuru is not an apple that falls when it is ripe. You have to make it fall. kwa hiyo wananchi wakiwa tayari katika kuwawajibisha viongozi nao viongozi watatambua kama wakifanya kosa watajiwajibisha lakini bila wananchi kutambua si ajabu waziri akatoka hadharani na kuwaita wanaotaka awajibike ni wehu
  chamsingi ni kutumia 2010 vizuri uwezi ukamfukuza kifaranga wa bata kabla ya kumkamata bata mwenyewe.
  kumbuka mahamuzi ya tz yatafanyika kama ifuatavyo
  wanaunga mkono masha aondoke waseme ndioooooooooooooooooooooooo
  wasiounga mkono masha aondoke waseme siooooooooooooooooooooooooo
  waliosema sioooooooooooooooooo wameshinda
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Jan 18, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Ni Sengerema au Ukerewe?
  Hii ni aibu kubwa kwa nchi inayojivunia amani na utulivu, mimi naona ingefaa serikali nzima ijiuzuru kwa kushindwa kulinda amani!
   
 6. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2010
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,747
  Likes Received: 376
  Trophy Points: 180
  nani alisema tanzania kuna kalcha ya kujiuzulu? kama ipo tungeanza na serikali za kijiji, kata, tarafa, wilaya na mkoa ndipo tufike kwa masha kwani kiutawala ni kamti ya ulinzi ndiyo ingewajibika kabla ya waziri... hivi si kuna maafisa usalama kila kona ya tanzania na wanakula pesa yetu???

  maneno haya si ya kumsafisha masha bali ni kuweka mambo sawa tu
   
 7. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Inaelekea wewe unadamu ya kijambazi
   
 8. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,210
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Sahihisho ni Wilaya ya Ukerewe Kwa mama Mongela na nyumbani kwa Makamu Mwenyekiti Taifa wa CCM na Spika aliyepita Pius Msekwa

  Kuna habari toka huko zinasema kuwa Polis wanachojua wao ni kufuatilia tu dili za magendo,na wakiambiwa kuna jahazi zimebeba mali za magendo huwa wanajazana ufukweni kuzisubiri ili "wazishughulikie"lkn kwenye majambazi "labda sio kazi yao"

  Masha unasubiri nini kujiuzuru hadi sasa baada ya watu zaidi ya 16 kufa kwenye shambulio la ujambazi??
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu taratibu usije ukaripotiwa tu!!
   
 10. B

  Bull JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Only Great Thinker Ali Hassan Mwinyi did and can do this
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Masha akijiuzulu mimi narudisha passport yangu uhamiaji na kujiondoa ktk orodha ya watanzania wa asili
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu wako wachache sana... pia kuna mrema, mwandosya (aliacha ile wizara ya JK na kurudi chuo) labda na mimi na wewe tunaweza kuachia hivi vikazi vya majasho... lakini sio viongozi wetu... tena hasa tuliowachagua kwa kura
   
 13. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kujiuzuli piga ua ajiuzulu mtu hiyo ndo tanzania zaidi ya uijuavyo
   
 14. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #14
  Jan 18, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  pole msanii

  nini kurudisha pass ataukitoa uhai wako ajiuzulu mtu mkuu we vumilia tu ipo siku isonajina mungu ata leta neema ya kweli
   
 15. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #15
  Jan 18, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Rafiki yangu, imeshindikana kujiuzulu kutokana na mabomu ya mbagala ambayo ni uzembe wa wazi halafu atajiuzulu mtu kwa ajili ya hili? Siyo rahisi. Kwanza Masha mwenyewe alishakufa siku nyingi. tunasubiri mazishi tu. Yeye huwa anasikika kwenye vitambulisho vya taifa tu kwa kuwa huko kuna 10% haya mengine yeye hayamhusu.
   
 16. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #16
  Jan 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,659
  Likes Received: 21,878
  Trophy Points: 280
  Utaisubiri siku hiyo hadi uhai utakutoka bila kuiona. Neema na mabadiliko ya nchi hii yataletwa na sisi wenyewe (Raia) tukiamua kufanya hivyo. Mwenyezi Mungu alishajitoa kwenye hilo baada ya kupata haki yetu ya kikatiba kuweka madarakani uongozi kwa kura. TUAMUE SASA
   
 17. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #17
  Jan 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ajiuzulu KWA HILI TU?......kwanza halina COST IMPLICATION!

  AMESEVU LA VITAMBULISHO ajiuzulu kwa hili?

  NAH!...
   
 18. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2010
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hakika tunahitaji mwanzo mpya; na huu utaletwa na watanzania wenyewe - kwa ujumla wao. Pindi kila mtu atakapofahamu haki yake, na ni kwa nini yupo; hakika mambo yatabadilika. Kwa hali ilivyo hivi sasa ya nchi kuendeswa na viongozi kana kwamba wanawafanyia hisani wananchi; mambo hayawezi kwenda.
   
 19. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #19
  Jan 18, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,750
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  my sincere condolences!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 20. G

  Godwine JF-Expert Member

  #20
  Jan 19, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kimbweka naona unawaogopa majambazi zaidi. tanzania tunaitajika kujenga misingi uhuru wa kutoa mawazo , je unafahamu ya kuwa watu wanaojihusisha na ujambazi ni watumishi wakubwa wa jeshi la polisi? na je unafahamu ya kuwa tanzania ni nchi ya 86 kwa ujambazi duniani? lakini je umejaribu kufanya tafiti madhara ya ujambazi? ukosefu wa dawa mahospitalini? wizi kwenye sekta ya umma?: na upotevu wa fedha katika mikataba ya madini ? kwa mfano alex stewart pekee analipwa shs bilioni 11 kwa mwaka wakati gharama zake za uendeshaji ni shs bil 5, je uoni ujambazi anaoufanya ni mkubwa zaidi lakini je waziri wa madini anafanya nini? watanzania wamezoea wameshindakushambulia matokeo na si kutafuta chanzo. kwa hiyo lazima tuanze kupambana na vitu vyenye hatari zaidi na kuvifanya ni vipao mbele , kwa mfano tukiweza kuleta malezi bora kwa watu wetu tutapunguza ujambazi. na tukiongeza ajira za watu wetu pia tutapunguza ujambazi kwa hiyo rais na waziri wa ajira wao ndio wangekua wa kwanza katika kujiuzuru na si kushambulia matokeo,.......................................
  naweza kuwauliza watz je
  wanaunga mkono masha aondoke waseme ndioooooooooooooooooooooooo
  wasiounga mkono masha aondoke waseme siooooooooooooooooooooooooo
  waliosema sioooooooooooooooooo wamewazidi wa ndio.
  lakini cha msingi ni misingi ya utawala bora na utendaji na si mtu binafsi
   
Loading...