singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi, wakiwa na bunduki aina ya AK 47 na milipuko, wameuawa na polisi eneo la Engosheraton-Sinoni, huku mwanamke akishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alimtaja mmoja wa watu waliouawa ni Athumani Ramadhani (26) au kwa jina lingine Kassimu na mkewe, Nasri ndiye anashikiliwa.
Alisema wengine hawajafahamika na miili yao iko chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mount Meru ya Mkoa wa Arusha kwa ajili ya uchunguzi na kutoa nafasi kwa wananchi kuwatambua.
Kamanda Sabas alisema Jumamosi iliyopita, asubuhi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kwamba huko Engosheraton–Sinoni, kuna kijana mmoja wanayemtilia shaka kuwa anajihusisha na matukio ya uhalifu.
Alisema waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata Athumani na baada ya kumpekua, alikutwa na milipuko aina ya Explogil TMV6 water explosive 17 na Giogel Kubela 10. Vitu vingine walivyomkuta navyo ni makoti makubwa mawili na kofia moja ya kuficha uso.
Alisema baada ya mahojiano naye, aliwaeleza kuwapo wenzake wawili anaoshirikiana nao katika matukio ya uhalifu.
“Tuliandaa mtego na majira ya saa 5 usiku, polisi wakiongozana na mhusika walienda eneo la Fire kwenye nyumba iliyodaiwa wenzake wapo. Polisi waligonga na wakati mlango ukifunguliwa, Athumani alipiga kelele ‘takbir’, na baada ya kelele hizo, polisi walianza kurushiwa risasi kutoka kwa watuhumiwa walioenda kuwakamata,” alisema.
Alisema kwa kutumia mbinu za kivita, polisi walifanikiwa kuzima mashambulizi hayo na kuingia chumbani, walikokuta vijana wawili waliokuwa wamejeruhiwa kwa risasi.
Alisema wakati wa majibizano ya risasi kati yao, wahalifu hao walimpiga risasi mwenzao Athumani na wote watatu walifariki wakati wakipelekwa hospitali.
Alisema upekuzi ulipofanyika katika chumba cha watu hao, walikuta sare tano za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kofia tano za kuficha nyuso, vazi moja la karate na pikipiki moja iliyobomolewa yenye namba bandia MC 983 BMK.
Aliitaja vitu vingine walivyokutwa navyo ni bendera mbili nyeusi zenye maandishi ya lugha ya Kiarabu, kisanduku cha chuma, hati ya kusafiria ya Abrahaman Athuman Kangaa iliyotolewa Aprili 2, 2013.
Vingine ni simu tano za mkononi, ambapo kati ya hizo moja baadaye ilitambuliwa kuwa ni ya Mary Joseph, aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Februari 20, mwaka huu huko Engosheratoni-Sinoni.
Pia alisema walikuta kifurushi cha unga wa baruti, kisu kimoja kikubwa, karatasi zenye ujumbe wa vitisho unaosema, ‘Nasaha kwa Kova, mzee andaa kamati ya mazishi ya vipolisi vyako, tukimaliza tutakufikia wewe.”
Alisema walikuta mafuta ya kusafishia bunduki na bunduki aina ya AK 47, iliyotumika kuwashambulia askari polisi yenye namba 1998-AFV0822 ikiwa na magazini yake na risasi 18.