Uchaguzi 2020 Majaliwa: Uongozi wa nchi hauendi kwa upepo na ushabiki

Mocumentary

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
768
1,959
Mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa ya Chama cha mapinduzi (CCM), na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Singida kutafakari aina ya kiongozi wanayemtaka aiongoze Tanzania.

Waziri mkuu ametoa wito huo leo Septemba 15, 2020 wakati akizungumza na wananchi waliohuhudhuria mkutano wa kuwanadi wagombea wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya CCM kata ya Ilongero wilayani Singida.

“Uongozi wa nchi siyo jambo la mchezo, siyo jambo la kujaribiwa, wala haliendi kwa upepo na ushabiki. Ni lazima mkae na kutafakari ni nani anafaa kuongoza nchi hii,” amesema Majaliwa.

Wakati huohuo, Waziri mkuu amempokea aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Singida, Frank Petro Akunay ambaye ameamua kuhamia CCM.

Akunay amehamia CCM akiambatana na mkewe Betina Petro pamoja na mdogo wake Daniel petro akisema kuwa amerejea nyumbani kwani alikuwa CCM kabla ya kujiunga CHADEMA ambako ametoka sasa.

Chanzo: Dar Mpya
 
Mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa ya Chama cha mapinduzi (CCM), na waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Singida kutafakari aina ya kiongozi wanayemtaka aiongoze Tanzania...

Aliyeko kwenye uongozi sasa hivi alikuwa ni mtu sahihi kutoa mawazo kama haya kweli?

Ni kukosa busara tu kunakoweza kumpelekea mtu kujifagilia kitoto toto namna hii.

Kama mnakubalika mizengwe yote ya kuwaengua washindani wenu ya nini mumiani nyie?

#2020 tunakwenda na Lissu. Habari ndiyo hiyo.
 
Mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa ya Chama cha mapinduzi (CCM), na waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Singida kutafakari aina ya kiongozi wanayemtaka aiongoze Tanzania...
Wataongea utopolo wote mwaka huu!!
 
Kwaza yeye yemwenyewe alikuwa wakawaida wakati lisu anapambana na akina mkapa wakati huo yeye sijui alikuwa wapi.
Hivi kweli usaili ungeitishwa kwa kuzingatia wasifu wa mtu, hivi kweli PM angaliweza kuaminika na kupewa nafasi hiyo! Uongozi hujaribiwa ili kuvumbua vipaji vipya, na hii ndiyo maana kubwa ya ubunifu.
 
Mtanzania yoyote mwenye akili timamu anaweza kuwa rais wa nchi hii. Kama JK na Magufuli wameweza kuwa marais, nani atashindwa kazi hiyo?

Hata siku moja. Umaskini ni shida sana. Unaweza kuona mtu anavaa suti, viingereza vingi, kumbe shida yake nafasi ya kupata ubwabwa na kutupelekea bahari Dodoma
 
Back
Top Bottom