Uchaguzi 2020 Majaliwa: Nafasi ya Urais inagusa maisha yako, sio jambo la mchezo

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,278
2,000
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Masasi watambue kwamba nafasi ya urais inagusa maisha yao na wala si jambo la mchezo.

“Wazee wangu, mama zangu na vijana wenzangu, urais siyo jambo la mchezo, urais ni maisha yako wewe. Urais wa Tanzania unataka mtu mwenye uwezo wa kuongoza watu zaidi ya milioni 60 wenye dini, vyama, makabila, na uwezo tofauti,” amesema.

Ametoa wito huo leo (Jumatano, Oktoba 21, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa mji wa Masasi katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba kata ya Mkuti, wilayani Masasi, mkoani Mtwara.

“Leo usije ukachagua mtu anayeendekeza mambo ya udini, utakuwa umefanya kosa kubwa sana. Nchi hii imejengwa kwa misingi na uadilifu, hatuangalii kabila au dini ya mtu, kipato cha mtu au rangi ya mtu,” amesisitiza.

Mheshimiwa Majaliwa ambaye yuko mkoani Mtwara kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Masasi, Bw. Godfrey Mwambe; mgombea ubunge wa jimbo la Ndanda, Bw. Cecil Mwambe; mgombea ubunge wa jimbo la Lulindi, Bw. Issa Ally Mchungaela na wagombea udiwani wa CCM.

Tunataka kiongozi atakayehubiri amani, tunataka kiongozi ambaye tuna historia naye, tuache kufanya uchaguzi kwa kufuata upepo. Tunataka kiongozi ambaye ataleta maendeleo. Tumchague Rais, narudia tumchague Rais, tusichague mtu wa kwenda kukaa Ikulu,” amesisitiza.

Mapema, akiwa njiani kuelekea Masasi, Mheshimiwa Majaliwa alisimamishwa na wakazi wa vijiji vya Chienjele, Namakuku na Mibura katika kata ya Chienjele, wilayani Ruangwa ambako aliwaomba wakazi hao ifikapo Jumatano ijayo, (Oktoba 28) wampigie kura za ndiyo mgombea urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli.

Mbunge wa jimbo la Ruangwa, Kassim M. Majaliwa na diwani wa kata hiyo, Bw. Rashid Nnunduma, wote wamepita bila kupingwa.

Aliwaeleza wakazi hao kwamba kiasi cha sh. bilioni 58 kimeshatolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Nanganga-Ruangwa kwa kiwango cha lami. “Fedha imeshatolewa, mkandarasi wa Kichina ameshaanza kazi kutoka Namahema kwenda Nanganga na naamini watakamilisha kazi yao ifikapo Agosti, 2021 kama walivyoahidi,” amesema.

Alisema barabara ya kutoka Namahema na Nandangala kuelekea Makutano – Nachingwea nayo pia itajengwa kwa kiwango cha lami. Alisema miradi ya maji inaendelea kujengwa ili kuwaondolea adha wakazi hao na akawaomba wamchague Rais Magufuli ili akamilishe kazi aliyoianza.
 

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
1,352
2,000
Hata mkoloni tuna historia nae lakini ameondoka. Wawe wanaeleza maisha ya watu namna yalivyoboreshwa wala sio kusema kuna mambo akayamalizie. Mambo hayo ni yapi? Nchi sio banda au shimo kwamba ukishamaliza ujenzi unapumzika.

Nchi inajengwa kilasiku na wakiendelea na tabia ya kusema kuna mambo ameyaanza hajayamaliza hata baada yamiaka mitano watasema katiba ibadilishwe ili apate muda wa kumaliza mambo aliyoyaanzisha.

Mheshimiwa Majaliwa kua mwepesi kukiri mapungufu kama mzunguko wa hela kua mgumu,maslahi ya wafanyakazi,matatizo ya time ya uchaguzi kama vile wewe kupita bila kupingwa.
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
10,934
2,000
“Wazee wangu, mama zangu na vijana wenzangu, urais siyo jambo la mchezo, urais ni maisha yako wewe. Urais wa Tanzania unataka mtu mwenye uwezo wa kuongoza watu zaidi ya milioni 60 wenye dini, vyama, makabila, na uwezo tofauti,” amesema.
That's why I love politics and hate football!!

Mrisho Halfan Ngassa, aliyezaliwa 1989 eti anaitwa mzee, huku Kassim Majaliwa aliyezaliwa December 1960 anajiita kijana!!

Hata JPM aliyezaliwa October 1959 huwa anamwita JK mzee kwa sababu na yeye anajiona kijana!!!

Kwa maana nyingine, Mgombea wa wapenda mabadiliko, Mheshimiwa Tundu Lissu aliyezaliwa January 1968, yeye ni kavulana fulani hivi!!

Hakika haya yasingetokea kama tusingekuwa na watu aina ya Juma Kapuya, Stephen Wassira, na wengine wengi kama wao!!!

Sasa mimi si nitakuwa katoto fulani hivi!!!

Na katoto mimi itabidi nikapigie kura kavulana manake tutakuwa tunaendana endana kwa sababu hata ile michezo michezo ya vitoto kama kombolela itakuwa hakajasahau!!
 

kurlzawa

JF-Expert Member
Jan 23, 2018
12,317
2,000
Ndio maana tumemkataa msaliti wa Nchi Lissu
Umevishwa minyororo ya dhahabu hauna tofauti na chief mareare hapo tu baba ako sio majaliwa na sio JPM je ungekuwa mtoto wa hao si ungetolea watu risasi.
 

Kilimbatz

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
303
250
Kwani uraisi unasomewa?

Hauoni hata aibu waziri mkuu mzima kuwa mbunge wa viti maalum
 

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,539
2,000
Ndio maana tunataka tupige kura kwa Lisu na chadema.

CCM mmekuwa miungu watu, mnatunyanyasa raia kwenye nchi yetu.
 

IDEGENDA

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
2,482
2,000
Huyu awadanganye watu wa kusini kama yeye sisi siyo wajinga kama watu wa kusini
Nyie ni watu wa wapi? Ambako hamuihitaji kura za wajinga wa kusini?

Basi usijali hao wajinga wa kusini watamchagua Magufuli.

Ninyi werevu mtamchagua Amsterdam.
 

HRT

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
437
500
Ni kweli nafasi ya Rais inagusa maisha yetu. Hivyo hatuwezi kuchagua mtu mbaguzi na anayeona ni halali kuua wenzake kisa madaraka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom