Uchaguzi 2020 Majaliwa: Mchagueni Dkt. Magufuli kwasababu ana uwezo wa kusimamia kazi ipasavyo, si mlalamishi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa amewaomba Watanzania wote wakiwemo na wakazi wa Kigoma wahakikishe wanamchagua Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ni mgombea urais kwa tiketi ya CCM kwa sababu ni kiongozi shupavu, mpenda maendeleo na si mlalamishi.

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumapili, Oktoba 18, 2020) alipozungumza na wakazi wa Kigoma kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mwanga Centre wakati akimuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Kilumbe Ng’enda na wagombea udiwani wa CCM.

“Tumchague Dkt. Magufuli kwa sababu ni kiongozi tunayemjua na ametumikia katika nafasi ya urais kwa ufanisi mkubwa. Dkt. Magufuli ameweza kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo ya afya, elimu, barabara na maji katika kipindi cha muda mfupi wa miaka mitano, tumpe ridhaa ya kuongoza miaka mitano mingine ili tupate maendeleo zaidi.”

Amesema CCM ndio chama pekee chenye dhamira ya kuwaletea maendeleo na wasifanye makosa kwa kuchagua wagombea wasiokuwa na uwezo wa kuwatumikia na badala yake wachague wagombea kutoka CCM kwani ina ilani ambayo imeorodhesha miradi yote ya maendeleo itakayotekelezwa nchi nzima ikiwemo na Kigoma.

Amesema wananchi wanatakiwa wamchague Dkt. Magufuli kwa sababu ni kiongozi muadilifu, mchapakazi na mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu na upendo kwa watu wa dini zote na anauwezo wa kusimamia kazi ipasavyo na ndio sababu Tanzania sasa inamaendeleo makubwa. “Oktoba 28 mwaka huu nendeni mkamchague Dkt. Magufuli.

Akizungumzia kuhusu miradi ya ujenzi wa barabara iliyotekelezwa Kigoma, Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali imetoa sh. bilioni 63.323 kwa ajili ya ujenzi barabara kutoka Kidahwe hadi Kasulu kwa kiwango cha lami na tayari mradi huo umekamilika na utanufaisha maeneo ya Wilaya za Kasulu na Kigoma.

“Serikali imetoa shilingi bilioni 47.159 kwa ajili ya mradi wa ujenzi barabara kutoka Nyakanazi hadi Kabingo yenye urefu wa kilomita 50 kwa kiwango cha lami, ambapo kwa sasa mradi huo umefikia asilimia 86 na utanufaisha maeneo ya Wilaya ya Kakonko.”

Mheshimiwa Majaliwa amesema miradi mingine ya barabara za mkoa wa Kigoma ambazo zimetengewa fedha katika Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2020/2021 ni pamoja na ujenzi wa barabara kutoka Manyovu – Kasulu – Kabingo, shilingi bilioni 372.109 zitatumika kujenga kilomita 260.6 kwa kiwango cha lami.

Awali, katika kuonyesha kuwa wakazi wa Manispaa ya Kigoma wamechoshwa na upinzani wanachama 200 wa Vyama vya Upinzani wengi wao kutoka ACT Wazalendo wakiongozwa na aliyekuwa meneja wa kampeni wa Zitto Kabwe, Patrick Mzigama wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM baada ya kuridhishwa na kasi kubwa ya maendeleo iliyofanywa na serikali ya CCM katika awamu ya kwanza ya Uongozi wa Rais Dkt. Magufuli.

Mzigama ametumia fursa hiyo kuwaomba radhi wakazi wa Kigoma Mjini kwa sababu yeye ndiye aliyewaongoza katika kuchagua vibaya mwaka 2015, hivyo amewaomba wabadilike na siku ya kupiga kura itakapofika wakawachague wagombea wote wa CCM. “Rais Dkt. Magufuli amejenga miradi mikubwa na maendeleo, amerudisha nidhamu kwa watumishi wa umma na wanafunzi wanasoma bure hivyo hatuna sababu ya kumchagulia mtu ambaye hawataongea lugha moja.”
 
"Nchi hii imeliwa sana" tangu 2015 kauli ni hiyo hiyo au huo siyo ulalamishi?
Unataka tumpe Mbowe na genge lake aimalizie sio?. Wao Sera yao ni kuuza mashirika ya umma yote, pamoja na rasilimali zetu, huku wakiuza kwa kanda nchi hii kwa mabeberu.. Yani Magufuli asimamie kodi zetu vizuri, anunue ninyi muuze aisee. Nendeni mkauze pale Ufipa.
 
1 Mkichagua wapinzani sitoleta maendeleo.

2 Mwanamke mweupe nitampa kipao mbele kuliko mwanamke mweusi.

3 Kwani serikali ndio ilioleta tetemeko? Hela iliochangwa kwa wahanga naijengea airport Chato.

Kiongozi anatakiwa awe mnyenyekevo na hana ubaguzi kwa raia wake Magu hatufai mbaguzi na mlafi wa hela za waathirika.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Jiwe si mlalamishi?

Hahaha huyu mzee amekunywa nini mapema yote hii? naona zimemruka. Jiwe liendelee kupiga magoti tu kura halipati ng'o, tumechoka drama zake
 
Unataka tumpe Mbowe na genge lake aimalizie sio?. Wao Sera yao ni kuuza mashirika ya umma yote, pamoja na rasilimali zetu, huku wakiuza kwa kanda nchi hii kwa mabeberu.. Yani Magufuli asimamie kodi zetu vizuri, anunue ninyi muuze aisee. Nendeni mkauze pale Ufipa.
Ila lumumba kwa kukaririshana maneno mpo vizuri, eti mabeberu.
 
FB_IMG_16031094235415065.jpg
 
beth nini maoni yako kwa wagombea wa CCM waliopita bila kupingwa kuhusiana na suala la kumpigia kampeni mgombea wao wa Uraisi? Kwa maoni yangu, wote waliopita bila kupingwa kwa namna moja au nyingine wanamuhujumu mgombea wao maana wasingepita bila kupingwa wangekuwa uwanjani kumwombea mgombea wao wa Uraisi kura.

Michezo mingine haina tija mfano Mh January alikuwa na tishio gani toka upinzani mpaka apite bila kupingwa? Kuna haja ya kuwachunguza wote waliopita bila kupingwa walichofanya kwenye huu uchaguzi kuchangia ongezeko la kura za CCM
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa amewaomba Watanzania wote wakiwemo na wakazi wa Kigoma wahakikishe wanamchagua Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ni mgombea urais kwa tiketi ya CCM kwa sababu ni kiongozi shupavu, mpenda maendeleo na si mlalamishi.

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumapili, Oktoba 18, 2020) alipozungumza na wakazi wa Kigoma kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mwanga Centre wakati akimuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Kilumbe Ng’enda na wagombea udiwani wa CCM.

“Tumchague Dkt. Magufuli kwa sababu ni kiongozi tunayemjua na ametumikia katika nafasi ya urais kwa ufanisi mkubwa. Dkt. Magufuli ameweza kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo ya afya, elimu, barabara na maji katika kipindi cha muda mfupi wa miaka mitano, tumpe ridhaa ya kuongoza miaka mitano mingine ili tupate maendeleo zaidi.”

Amesema CCM ndio chama pekee chenye dhamira ya kuwaletea maendeleo na wasifanye makosa kwa kuchagua wagombea wasiokuwa na uwezo wa kuwatumikia na badala yake wachague wagombea kutoka CCM kwani ina ilani ambayo imeorodhesha miradi yote ya maendeleo itakayotekelezwa nchi nzima ikiwemo na Kigoma.

Amesema wananchi wanatakiwa wamchague Dkt. Magufuli kwa sababu ni kiongozi muadilifu, mchapakazi na mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu na upendo kwa watu wa dini zote na anauwezo wa kusimamia kazi ipasavyo na ndio sababu Tanzania sasa inamaendeleo makubwa. “Oktoba 28 mwaka huu nendeni mkamchague Dkt. Magufuli.

Akizungumzia kuhusu miradi ya ujenzi wa barabara iliyotekelezwa Kigoma, Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali imetoa sh. bilioni 63.323 kwa ajili ya ujenzi barabara kutoka Kidahwe hadi Kasulu kwa kiwango cha lami na tayari mradi huo umekamilika na utanufaisha maeneo ya Wilaya za Kasulu na Kigoma.

“Serikali imetoa shilingi bilioni 47.159 kwa ajili ya mradi wa ujenzi barabara kutoka Nyakanazi hadi Kabingo yenye urefu wa kilomita 50 kwa kiwango cha lami, ambapo kwa sasa mradi huo umefikia asilimia 86 na utanufaisha maeneo ya Wilaya ya Kakonko.”

Mheshimiwa Majaliwa amesema miradi mingine ya barabara za mkoa wa Kigoma ambazo zimetengewa fedha katika Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2020/2021 ni pamoja na ujenzi wa barabara kutoka Manyovu – Kasulu – Kabingo, shilingi bilioni 372.109 zitatumika kujenga kilomita 260.6 kwa kiwango cha lami.

Awali, katika kuonyesha kuwa wakazi wa Manispaa ya Kigoma wamechoshwa na upinzani wanachama 200 wa Vyama vya Upinzani wengi wao kutoka ACT Wazalendo wakiongozwa na aliyekuwa meneja wa kampeni wa Zitto Kabwe, Patrick Mzigama wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM baada ya kuridhishwa na kasi kubwa ya maendeleo iliyofanywa na serikali ya CCM katika awamu ya kwanza ya Uongozi wa Rais Dkt. Magufuli.

Mzigama ametumia fursa hiyo kuwaomba radhi wakazi wa Kigoma Mjini kwa sababu yeye ndiye aliyewaongoza katika kuchagua vibaya mwaka 2015, hivyo amewaomba wabadilike na siku ya kupiga kura itakapofika wakawachague wagombea wote wa CCM. “Rais Dkt. Magufuli amejenga miradi mikubwa na maendeleo, amerudisha nidhamu kwa watumishi wa umma na wanafunzi wanasoma bure hivyo hatuna sababu ya kumchagulia mtu ambaye hawataongea lugha moja.”
Mtu unaposema kiongozi ni mcha Mungu halafu kiongozi huyo huyo chini ya utawala wake, wanaomkosoa wanauawa, wanatekwa, wanashambuliwa, wanapotezwa, wanabambikiziwa kesi za uhujumu uchumi; kiongozi huyo huyo anawabagua watu kwa itikadi zao, haheshimu haki za watu za kuchagua viongozi wanaowataka, anatunga sheria za kuwagandamiza watu na kufuta uhuru wao - kiongozi wa namna hiyo ni mcha Mungu au mcha miungu? Maana kuna miungu ambayo hutaka sadaka za damu, labda kama ni anamaanisha miungu ya namna hiyo LAKINI haiwezekani awe ni Mungu yule wa Ibrahim, wa Isaka na Yakobo, yaani yule anayeabudiwa katika KWELI NA ROHO WA MUNGU.

Kila alitumiaye jina la Mungu kuwahadaa watu, ataionja ghadhabu ya Mungu. Mungu hajaribiwi wala kudhihakiwa.

Majaliwa awadanganye watu kwa lugha na maneno yote anayoweza kuyatengeneza lakini asimhusishe Mungu na udhalimu. Uuaji, utekaji, upotezaji watu - siyo miongoni kwa matendo ya wacha Mungu wa kweli.

Kiongozi anaweza kufanya makosa yote, na akasamehewa LAKINI muuaji hastahili msamaha wa aina yoyote. Ukimpa kura muuaji maana yake unashiriki uuaji na utajibu mbele za Mungu.

Ni aheri umpe kura yako hata Rungwe kuliko kumpa mgombea ambaye una uhakika kabisa ameua, ametesa ameonea. Ukimpa kura yako mgombea wa namna hiyo maana yake unataka watu waendelee kuawa, kushambuliwa, kuonewa au kupotezwa. Je, unajua safari hii atakayeuawa au kupotezwa au kuonewa siyo wewe, siyo kaka yako, baba yako, mjomba wako, rafiki yako, mwanajumuia mwenzako, classmate wako au jirani yako?

Zuia mauaji, mateso, utekaji, uonevu na ubaguzi kwa kujitenga kabisa na wagombea wanaoyapalilia hayo. Chagua viongozi wanaopigania haki ya kila mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Mkichagua wapinzani sitoleta maendeleo.

2 Mwanamke mweupe nitampa kipao mbele kuliko mwanamke mweusi.

3 Kwani serikali ndio ilioleta tetemeko? Hela iliochangwa kwa wahanga naijengea airport Chato.

Kiongozi anatakiwa awe mnyenyekevo na hana ubaguzi kwa raia wake Magu hatufai mbaguzi na mlafi wa hela za waathirika.

Ndukiiiii
We ulitaka asemaje ??
Acha uzuzu mjomba.
Kwanza baada ya kusema hayo umepungukiwa nini hahahah acha uchawi wewe bwana.
 
Majaliwa tuna imani na Lissu, alianza kuwatetea wachimbaji wadogo wa dhahabu Nyamongo na aliwatoa magereni walikowekwa na serikali ya CCM.
Mjomba kwanza magerezani unapelekwa na serikali ya Ccm au na polisi kwa makosa yako mwenyewe acha uzuz mjomba wewe.
 
Mkuu umesoma habari vizuri, eti saiv sio waziri mkuu tena ni mjumbe! Ccmna serikali yake maigizo mtaacha lini?
Ulitaka tumuite jina lako au laaah maana chama chenu hakina mbele wala nyuma hata mfumo wa uongozi haupo vyema kwahiyo unashangaa kusikia mjumbe kamati kuu inawezekana hata huelewi maana yake.
Baki na chama chako tuachie chama chetu mjomba
 
Back
Top Bottom