Kalamu ya Mwananchi
Senior Member
- Oct 27, 2020
- 100
- 550
Yaani hawa viongozi wanataka kufanya uhuru wa kujieleza kuwa ni dhambi. Kana kwamba wao wenyewe tu ndo wenye haki ya kusema kuhusu mambo yanayoendelea nchini. Wakae wakitambua kuwa kwasasa teknolojia haiepukiki, wamepambana nayo ilikuzuia watu wasijieleze ila mpaka sasa bila bila. Waelekeze nguvu zao kwenye kutumikia wananchi na kutatua shida zao, wala hawatasikia 'wakisemwa vibaya'.
Teknolojia imeleta usawa na kumruhusu mwananchi wakawaida kutoa maoni kuhusu mambo yanayoendelea nchini, na akasikia, kwahiyo teknolojia inabidi ilindwe na sio kuanza kupambana nayo. Kweli Tanzania kuna ombwe la uongozi. Tuna safari ndefu sana.