Majaliwa: Kumejitokeza tabia ya Watu kutumia vibaya Uhuru wa kutoa Mawazo kwenye Mitandao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Akiahirisha Shughuli za Bunge, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza Waziri wa Katiba, Waziri wa Mambo ya Ndani, Nje, Waziri wa Utumishi, Waziri wa Mawasiliano kutumia Sheria, kanuni na taratibu kuhakikisha vitendo vya matumizi mabaya ya mitandao vinadhibitiwa

Majaliwa amesema "Hivi karibuni kumejitokeza tabia ya baadhi ya watu kutumia vibaya haki ya uhuru wa mawazo. Matumizi mabaya ya mitandao yamesababisha kusambazwa kwa taarifa za upotoshaji na wakati mwingine kudhalilisha Watu, vikundi ama Viongozi"
 
Kama kulikuwa na neno kuwa rais Samiah anashauriwa vibaya basi huyu jamaa ni mmojawapo pamoja na Mwigulu Nchemba,Job Lusinde,Job Ndugai hawa ndiyo wanaomharibia huyu mama ili 2025 wamwondoe kirahisi.
 
Kikwete "dhaifu"? Au Kikwete yupi?
Kati ya jamii zinazoweza kustahimili ukosoaji ni pamoja na jamii ya mwambao wa pwani, rafiki zangu wazaramo na jamii zinazoshabihiana nazo ndio maana Mkwere aliishi na kuheshimiana na wakosoaji wake. Na akapata kuheshimika na kuwa na amani na furaha popote aendapo duniani.Kwa kawaida palipo na ukosoaji mwingi maana yake yapo mambo mengi yasiyokubalika na jamii inayokosoa, lengo likiwa ni kutarajia mabadiliko katika yale yanayo lalamikiwa. Iwapo anayelalamikiwa hana utayari wa kutafuta suluhu ya yale yanayolalamikiwa matokeo yake atajenga chuki na mlalamikaji. Kiasi hata ya kumwona ni adui. Nakawaida adui hawezi pata haki zake au kuwa salama mbele ya anaemlalamikiwa kwa maana yakuitaka haki yake.
 
Kuna uongo gani? Kwani Chief HANGAYA akupigwa picha ambazo kiuhalisia zina uliza maswali mengi? Moja ya picha imemuonesha Chief Hangaya akiwa mkubwa kumzidi tembo.

Halafu huyu waziri mkuu, kaanza chokochoko mapema asitegemee kwa kuongea huko atachukua madaraka 2025.
 
Kati ya jamii zinazoweza kustahimili ukosoaji ni pamoja na jamii ya mwambao wa pwani, rafiki zangu wazaramo na jamii zinazoshabihiana nazo ndio maana mkwere aliishi na kuheshimiana na wakosoaji wake. Na akapata kuheshimika na kuwa na amani na furaha popote aendapo duniani.Kwa kawaida palipo na ukosoaji mwingi maana yake yapo mambo mengi yasiyokubalika na jamii inayokosoa, lengo likiwa no kutarajia mabadiliko katika yale yanayo lalamikiwa. Iwapo anayelalamikiwa hana utayari wa kutafuta suluhu ya yale yanayolalamikiwa matokeo take atajenga chiki na mlalamikaji. Kiasi hata ya kumwona ni adui. Nakawauda adui hawezi pata haki zake au kuwa salama mbele ya anaemlalamikia kwa maana yakuitaka haki yake.
Mbona sasa hamtaki Mkiti wetu wa kudumu akosolewe kama mnajua hilo? Maana akiguswa huyo lazima mporomoshe matusi ya nguoni
 
Back
Top Bottom