Majaliwa Kassim Majaliwa “Ceremonial Prime Minister“? Ofisi yake yazidi kupunguziwa majukumu

Mimi nina machache ya kuchangia kuhusu hili swala, ila nina amini huyu ndio Waziri mkuu akiamua jambo Mkuu kabisa hakwepi na haulizi mradi liwe na faida kwa nchi.

Mimi namiliki viwanda kadhaa ambavyo 2 kati ya hivyo vilihitaji muda kuvi modernise with new technology, japo Waziri mmoja aliondolewa kwa kuto virudisha viwanda serikalini vilivyotaifishwa, nilipo enda kwa PM aliniuliza what is your rehalitation plan/ modernisation implementation plan ? Baada ya kumpatia alinyanyua simu tuu, na nikaendelea kukamilisha shuguli zangu japo nilipewa notice ya muda nisiuvuke.

Ni PM ambaye unazungumza nae kama rafiki, japo heshima lazima. Cheo hakijambadili Kasim Majaliwa ni mkweli na anaaminika.

Kila kibaya kinauzuri wake, Hii ndio serikali ambayo maamuzi yakifikiwa wanatekeleza kama ulivyokubaliana nao.

Kuna mengi tuu ambayo nguvu yake iko wazi na kwa hili wote wenye kuhusiana nae kikazi watathibitisha na ana msaada na kuaminika.

Mimi ni Mtanzania wa kwanza kuuza Nguzo za Umeme Njee ya nchi, na mikaratusi yote Upareni kusini (Same District )na Mwanga District nilivuna mimi kwa ajili ya treated poles za umeme/simu for export to kenya and Lebanon.

Na kwa mwelekeo wangu Ningeletewa taabu sana undeshaji wa viwanda vya kuchemsha nguzo kama vile Mkumbara/Korogwe.

Lakini kodi ya TRA na Maduhuri ya serikali hakikisha unalipa. Ukiwa na risiti uliolipia kodi za serikali mkononi unapokwenda kwao kuomba msaada wanakusaidia bila kigugumizi.

Na mpango wao wa Rural Electrification umekwisha zailisha zaidi ya billionaires 20 hapa Tanzania, kwa nguzo pekee yake.

Na angekuwa na roho mbaya nisingepata indorsement ya kuwa Chairman wa Africa Energy Developement Corporation.

Mengine tunachangia hapa JF kwa hisia na siyo kwa uhalisia. Lakini ndio hivyo mkiwa wengi kwenye jamii watakuwepo watakao toa maoni kwa hisia na wenye ushahidi na uhalisia.

Kukaa kimya tutakuwa tunadhihaki mazuri ambayo tumefaidika nayo na tutapunguza moyo wake wa kufanya mazuri.

mtu kazi yake ni kushinda twitter anakwambia majaliwa hana cheo wala nguvu.

yaani wakati mwingine unakaa unawaza hawa wenzetu wako sawa kweli!!!!
 
Viongozi wengi wanaoteuliwa na meko wanakubali nyadhifa hizo siyo kwa moyo mweupe bali wanakubaki ili kuogopa zengwe na kufanywa mfano.

Wengi wanajua hakuna utendaji ila ni kuchukua nafasi tu wakisubiri kufurushwa hama kutenguliwa, hakuna utendaji wa kazi kutoka kwenye mtima katika kipindi hiki.
 
Back
Top Bottom