Majaliwa Kassim Majaliwa “Ceremonial Prime Minister“? Ofisi yake yazidi kupunguziwa majukumu

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,531
8,615
Katika historia ya nchi hii haijawahi kutokea Waziri Mkuu aliyeporwa mamlaka yake kama Majaliwa

Kiukweli inasikitisha na pengine inaashiria kuwa na bosi asiyeamini uongozi wa pamoja

Mara nyingi Waziri Mkuu amekuwa na majukumu ya Tawala Za Mikoa ambayo ina maana Wakuu wa Mikoa; Wilaya na Wakurugenzi wanakuwa chini yake pamoja na kuwa msimamizi wa mawaziri na mkuu wa serikali bungeni.

Kwa mwendo tulikua nao Waziri Mkuu angalau alibakia na nguvu kwakuwa ofisi ya Uwekezaji ambayo nayo sasa imepelekwa ofisi ya Rais

Tunasubiri sasa kuona atapewa nini lakini hii ina maana kuwa Majukumu ya Ofisi ya Rais yameongezeka lakini zaidi kutakuwa na mawaziri mfano wa Serikali za Mitaa atakuwa na nguvu kuliko PM

Tumtakie Rais uundaji mwema wa baraza lake!!

Alamsiki!
 
Hajawahi hata siku moja Waziri Mkuu wa Tanzania kuwa na madaraka..
Ndio maana Sokoine alitolewa Uwaziri mkuu akapelekwa Uwaziri wa kawaida kabla ya kurudishwa tena
Same na Msuya.

Waziri Mkuu ni Waziri kama Waziri mwingine
Kazi yake kubwa ni kupokea maagizo ya Rais

Hata akipewa TAMISEMI bado Rais anaweza mpangia kila kitu
 
Ungeorodhesha majukumu ya Mawaziri wakuu waliopita moja na la msingi ni kusimamia Mawaziri wote, haya mengine ni urembo tu.

Kwanza kuwasimamia mawaziri kikazi, kinidhamu na projects zilizo chini ya wizara husika ni kazi nyingi sana kwa Waziri Mkuu.

Sasa hili la investment centre ni katika kujaribu kuongeza Mapato ya serikali kwa kuleta uwekezaji mkubwa na kutoa ajira kwa watu na fedha hizo kwenda kwenye miradi ya maendeleo inayosimamiwa na PM, sasa kama hiyo ni shida utakuwa huitaki mema nchi bali fujo na mlo wako.
 
Unge orodhesha majukumu ya mawaziri wakuu waliopita moja na la msingi ni kusimamia mawaziri wote , haya mengine ni urembo tu .
Kwanza kuwasimamia mawaziri kikazi, kinidhamu na projects zilizo chini ya wizara husika ni kazi nyingi sana kwa waziri Mkuu.
Sasa hili la investment centre ni katika kujaribu kuongeza Mapato ya serikali kwa kuleta uwekezaji mkubwa, na kutoa ajiri kwa watu , na fedha hizo kwenda kwenye miradi ya maendeleo inayosimamiwa na PM, sasa kama hiyo ni shida utakuwa huitaki mema nchi bali fujo na mlo wako

Muwekazaji gani serious atakuja wakati huu wa Magu? Ukiona nchi mpaka wachina wanasita kuja kuwekeza hapo unategemea nini?
 
Hajawahi hata siku moja waziri mkuu wa Tanzania kuwa na madaraka..
Ndo maana Sokoine alitolewa uwaziri mkuu akapelekwa uwaziri wa kawaida kabla ya kurudishwa tena
Same na Msuya.

Waziri Mkuu ni waziri kama waziri mwingine
Kazi yake kubwa ni kupokea maagizo ya Rais..

Hata akipewa TAMISEMI bado Rais anaweza mpangia kila kitu

Sokoine Alienda kwenye Matibabu pamoja na masomo Hungary
Aliporudi tu akarudishiwa u PM
sokoine ni kati ya mawaziri wakuuu waliokua na nguvu ; pengine na Kawawa
 
Back
Top Bottom