Majaliwa asema CCM kumpeleka kwa wananchi Rais Samia 2025

Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
5,080
8,219
Dodoma.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mwaka 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampeleka kwa wananchi mtu mmoja, Rais Samia Suluhu Hassan hivyo mawaziri watambue hilo.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 29, 2021 katika ukumbi wa St Gasper jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa mawaziri na naibu mawaziri.

Majaliwa amewataka mawaziri na naibu wao kuwa wasemaji wakubwa wa mafanikio ya Serikali ili itakapofika 2025, Samia Suluhu Hassan (Rais) apite na kusema kidogo tu.

"Wambieni wananchi kuhusu mazuri yanayofanywa na Serikali hii, tambueni msimamo na mtazamo wa Rais ili mkawe wasemaje zaidi yeye akija awe na maneno machache ya kueleza," amesema.

Waziri Mkuu amewataka mawaziri na naibu wao kufanya kazi kwa mashirikiano na kuheshimu kauli za viongozi wakuu kwani siyo kila agizo lazima waandikiwe barua ndipo watekeleze.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kuwa mfano kwa mienendo yao wakianzia na mavazi, kauli na kutojiinga katika mambo yatakayowafanya wajadiliwe.

Amesema katika mitandao ya kijamii wapunguze kuzungumza mambo mengi ili kusudi wanapotamka mambo machache yaonekane kuwa na maana kwa jamii.

Chanzo: Mwananchi
 
Wanasiasa wa hii nchi wamejaa njaa na unafiki tu.

Yani ndo kwanza bado miaka minne mbele mijitu inawaza uchaguzi tu badala ya kuwaza kutatua matatizo ya wananchi.

Huyo Bibi endeleeni kumjaza upepo wa kijinga, wakati sisi wananchi tunaendelea kunoa kichinjio cha 2025.
 
Wana uhakika wa kushinda, hawategemei kichinjio
 
Wanasiasa wa hii nchi wamejaa njaa na unafiki tu.

Yani ndo kwanza bado miaka minne mbele mijitu inawaza uchaguzi tu badala ya kuwaza kutatua matatizo ya wananchi.

Huyo Bibi endeleeni kumjaza upepo wa kijinga, wakati sisi wananchi tunaendelea kunoa kichinjio cha 2025.
Lakini so ndivyo wanavyofanya wrote?!! Si jana tu tumetoka kusikia kuwa mbatia anawaambia wenzake chadema, act na cut waungane ili waing'oe CCM 2025......kila mtu anazungumzia hilo
 
Ni Mambo ya ajabu sana umeingia juzi hata mwaka huna unawaza uraisi wa 2025 tumekuwa watu wapenda madaraka Sana, uchaguzi upo tu tufanye kazi, hata Upinzani wanaweza kushinda hiyo 2025.
TZ yetu wasaidizi ndiyo huwa wanamuharibu Rais, watahakikisha wanaongea kila kitu cha kumpendeza ili waendelee kula vinono...Na awamu hii Majaliwa, Ummy, Msigwa wanaongoza kwa mapambio
 
Wanasiasa wa hii nchi wamejaa njaa na unafiki tu.

Yani ndo kwanza bado miaka minne mbele mijitu inawaza uchaguzi tu badala ya kuwaza kutatua matatizo ya wananchi.

Huyo Bibi endeleeni kumjaza upepo wa kijinga, wakati sisi wananchi tunaendelea kunoa kichinjio cha 2025.
Ndiooo
 
Dodoma.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mwaka 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampeleka kwa wananchi mtu mmoja, Rais Samia Suluhu Hassan hivyo mawaziri watambue hilo.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 29, 2021 katika ukumbi wa St Gasper jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa mawaziri na naibu mawaziri.

Majaliwa amewataka mawaziri na naibu wao kuwa wasemaji wakubwa wa mafanikio ya Serikali ili itakapofika 2025, Samia Suluhu Hassan (Rais) apite na kusema kidogo tu.

"Wambieni wananchi kuhusu mazuri yanayofanywa na Serikali hii, tambueni msimamo na mtazamo wa Rais ili mkawe wasemaje zaidi yeye akija awe na maneno machache ya kueleza," amesema.

Waziri Mkuu amewataka mawaziri na naibu wao kufanya kazi kwa mashirikiano na kuheshimu kauli za viongozi wakuu kwani siyo kila agizo lazima waandikiwe barua ndipo watekeleze.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kuwa mfano kwa mienendo yao wakianzia na mavazi, kauli na kutojiinga katika mambo yatakayowafanya wajadiliwe.

Amesema katika mitandao ya kijamii wapunguze kuzungumza mambo mengi ili kusudi wanapotamka mambo machache yaonekane kuwa na maana kwa jamii.

Chanzo: Mwananchi

Majaliwa? CCM wamekutuma? Au umetumwa na wananchi? Au umejituma mwenyewe?​

Back
Top Bottom