Majaliwa aipa somo Jumuiya ya Madola, aitaka kuiga Tanzania mbinu za kapamabana na rushwa

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Jumuiya ya Madola inaweza kuiga mbinu ambazo Tanzania imetumia katika kupambana na rushwa, zikiwemo za kujumuisha wadau tofauti kwenye vita hiyo.

Alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Scotland walipokutana kwenye mkutano wa kimataifa uliojadili jinsi ya kupambana na rushwa duniani uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.

“Tanzania iko tayari kushirikiana na ninyi katika kujenga timu hii na ili uweze kupata picha halisi, nakukaribisha Tanzania uje ujionee hatua ambazo tumechukua hadi kufikia hapa tulipo kwenye vita hii dhidi ya rushwa,” alisema Waziri Mkuu ambaye alihudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais John Magufuli.

Alimueleza Katibu Mkuu huyo kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kupambana na rushwa kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwa wananchi. “Wananchi wanafurahia juhudi za serikali, vyama vya kiraia pia vinaunga mkono jitihada zetu na vyombo vya habari vinashirikiana nasi katika vita hii,” alisema.

Waziri Mkuu alitoa wito huo baada ya kuelezwa na Scotland kwamba anataka kuanzisha idara maalumu kwenye Jumuiya hiyo ambayo itasimamia mapambano dhidi ya rushwa na makosa ya jinai.

“Nataka tuwe na idara yenye watu mahiri wa idara za uhasibu, mahakama yenyewe ikiwemo waendesha mashtaka na wanasheria kutoka kwenye nchi kadhaa ili washirikishane uzoefu kutoka kwenye nchi zao.

Ninaamini katika nchi 53 ambazo ni wanachama wetu, sitakosa watu wa aina hii,” alisema. Alisema ameamua kufanya hivyo ili aweze kuendana na malengo makuu matatu ya jumuiya hiyo ambayo ni kupiga vita rushwa, kuhimiza utawala bora na usimamizi wa demokrasia.
 
Jamani jamani et Wawaige Tanzania kupambana na Rushwa wakati waingereza wanajui jinsi uchaguzi wenyewe wa TZ ulivyo bobea kwa Rushwa.
 
Hapa Tanzania hata wabunge wanaomba rushwa, halafu mnakuja na utumbo hapa kwamba Majaliwa awapa somo nchi zingine! Mbona nyie CCM mmechanganyikiwa hivi?
 
Hii habari ilitakiwa iingie kwenye maajabu 7 ya dunia,
Hii Ndio nchi wafanyakazi wa serikali matajiri na utajiri wao hata ukilinganisha na mishahara yao hauendani, hii Ndio nchi wanasiasa watunga Sheria Ndio majizi wazuri, leo hii ndio nchi ya mfano teh teh teh kwi kwi kwi
 
Hahahahah huyo ndio Majaliwa na mkutano wake anasema ulifana sana! Kumtoa Hosea na kumuweka mwingine ndio juhudi kubwa ya kuigw ya kupambana na rushwa? Au ile tumbua majipu bila kufuata sheria ndio waje waige? Sijaona mkakati wowote au hatua madhubuti! Angetutolea mfano mmoja tuelewe! Hajui kuwa hao wazungu wanajua kila kitu kupitia mitandao na balozi zao. Wanajua pia kuwa wana viongozi wa juu ambao hawafuati sheria na hawajui hata diplomasia! Wanajua!!
 
Tanzania imefanikiwa katika mapambano ya rushwa, na sasa nchi za Jumuia ya madola zinapaswa kuiga? maajabu duniani hayataisha.
 
Wakati Majaliwa anayasema hayo wakati ambapo traffic wamekaa barabarani wanachukua rushwa bila hata ya woga. Rushwa ya Tanzania ni ya mfumo
 
Hii nini sasa. Si watawale tu kimya kimya tumewaacha wafanye wafanyavyo badala yakutuzidisha gazab. Yan hao hao tang uhur ni walaj wazur wasl rushwa et tena hao hao toka October 2015 et wanapambana dhid ya rushwa
 
Back
Top Bottom