Majaji wa Tanzania hawajui kiingereza - Tundu Lissu

Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,700
1,086
Salaam wanabodi

Mbunge wa Singida na mwanasiasa machachari Katika siasa za Tanzania ndugu Tundu Lissu ameendelea kuwasakama majaji wa Tanzania kwa kusema hawajui kiingereza.

Akichangia leo bungeni amesema ukisoma hukumu nyingi za majaji wa Tanzania utasikitika 'watu wanahukumiwa vifungo vya maisha na kunyongwa kwa sababu majaji hawajui kiingereza ambayo ndiyo lugha inayotumiwa kwenye sheria za Tanzania,hivyo ameshauri sheria zote ziandikwe kiswahili.
 
Kuna ushahidi mwingi, majaji huwafwata mawakili wawasaidie kuandika hukumu.
 
waosema kiswahili kifundishwe kuanzia chekechea hadi chuo kikuu sijui wana agenda gani. Sasa hebu ona na si majaji tu hata katika maeneo mengi watu hawajui kuongea kingereza. Huo ndio ukweli.
 
salaam wanabodi

mbunge wa singida na mwanasiasa machachari katika siasa za tanzania ndugu tundu lissu ameendelea kuwasakama majaji wa tanzania kwa kusema hawajui kiingereza.

Akichangia leo bungeni amesema ukisoma hukumu nyingi za majaji wa tanzania utasikitika 'watu wanahukumiwa vifungo vya maisha na kunyongwa kwa sababu majaji hawajui kiingereza ambayo ndiyo lugha inayotumiwa kwenye sheria za tanzania,hivyo ameshauri sheria zote ziandikwe kiswahili.
tundu mwenyewe mbwembwe tu hana jipya.yeye anajua kingereza?
 
Kuna generation flani hapa Tanzania ambayo kingereza ni tatizo kubwa. Watu wengi walisoma shule za msingi za serikali(ukiacha Olimpio na Arusha School) kati ya miaka ya 80s hadi sasa hawana backgrond nzuri ya kingereza. Ndio maana utakuta watu wengi wenye umri kati ya around 50yrs kurudi chini hadi around 25yrs hawawezi kuandika/kuongea kingereza fasaha. Kwa bahati mbaya ndio hao watendaji na viongozi makazini serikalini na mashirika binafsi. Baada ya kugundua hilo tatizo wengi kama sio wote wenye uwezo wakawapeleka watoto wao shule za English medium ambazo zilianzishwa miaka ya 90 kama uyoga. Sasa hivi kuna vijana wako vyuoni wanaongea kingereza vizuri sababu wamesoma kwenye shule hizo za English medium. Tutegemee wafanyakazi wanaojua kingereza vizuri huko mbeleni wakishaingia hawa vijana kwenye soko la ajira. Hiyo ni analysis yangu ndogo tu
 
Hivi kweli kwanini hadi leo hukumu zinatolewa kwa lugha ya kiingereza?
 
Sasa ni dhahiri wabunge wa magamba wote wamenywea kwa Lisu. Hapo nyuma kila gamba leo lingesimama kuomba mwongozo wa Spika kwa vifungu vinavyokataza lugha za kuudhi utafikiri yana hata chembe ya soni. Leo magamba wote kimya, Werema niliona kama anataka kujiharishia wakati Lisu anashusha nondo. Bila shaka Werema anajutia hatua yake ya kumpeleka Lisu kwenye kamati iliyomtaka Lisu atoe ushahidi wa tuhuma zake dhidi ya Jaji feki Mbarouk &co. Imesaidia watanzania kujua jinsi tunavyoongozwa na vilaza.
Nimemtumia meseji asisahau na huyu kilaza Mulugo aliyetuaibisha juzi lakini naona kamanda Lisu kaamua kuipotezea.
 
kuna generation flani hapa tanzania ambayo kingereza ni tatizo kubwa. Watu wengi walisoma shule za msingi za serikali(ukiacha olimpio na arusha school) kati ya miaka ya 80s hadi sasa hawana backgrond nzuri ya kingereza. Ndio maana utakuta watu wengi wenye umri kati ya around 50yrs kurudi chini hadi around 25yrs hawawezi kuandika/kuongea kingereza fasaha. Kwa bahati mbaya ndio hao watendaji na viongozi makazini serikalini na mashirika binafsi. Baada ya kugundua hilo tatizo wengi kama sio wote wenye uwezo wakawapeleka watoto wao shule za english medium ambazo zilianzishwa miaka ya 90 kama uyoga. Sasa hivi kuna vijana wako vyuoni wanaongea kingereza vizuri sababu wamesoma kwenye shule hizo za english medium. Tutegemee wafanyakazi wanaojua kingereza vizuri huko mbeleni wakishaingia hawa vijana kwenye soko la ajira. Hiyo ni analysis yangu ndogo tu
wewe una umri gani?mimi ninajua kiingereza,lakini siko fluent simply because sikitumii kiingereza kwenye activities zangu za kilia siku..............nadhani wewe hauzungumzii kujua kiingereza,unazungumzia kuwa fluent.ili mtu aweze kuwa fluent anatakiwa awe na zile core pillars of language;speaking,listening,writing and reading...............huwezi kuniambia mtu mwenye degree hajui kiingereza,labda awe amenunua cheti.................hao watoto unaosema wamesoma english medium walete ushwahilini kwetu halafu uwacheki tena baada ya miaka miwili kama bado wataendelea kuwa fluent.lugha kama vitu vingine inahitaji practices for practice make perfect.............
 
Back
Top Bottom