Majaji wa Bongo Star Search

🤣🤣🤣 ila wengine hawako serious aisee.

Kuna mmoja alikuwa anaimba uno daaah🤣🤣🤣
 
Ile kazi naona ni ngumu sana. Msichukulie poa kihivyo. Kuna washiriki ni vichwa vibovu.

Halafu mleta mada, Master Jay anaujua muziki.
 
Ila watanzania wengi ni wanafiki sana.Mtu kuambiwa ukweli ndo unaleta thread hapa?
Halafu kumbuka hawa ni binadamu,huenda ukweli wao ukawa msaada kwa watu maana kwa mtu anayeamini ana kipaji atajaribu kuwa prove wrong na kwa kufanya hivyo ataenda mbali zaidi.
Kwa hiyo kama wanahitaji mshindi mmoja unataka wasemeje?

Wengine ni shindano tunslolipenda sana,na nahisi ninyi mnaoandika humu ni wale mashabiki ya wasafi ambao mnamponda Harmonize kujitoa huko.

Acheni unafiki watanzania.Hayo ni mashindano,kama wewe huyapendi na una akili zaidi yao,anzisha yako na wewe ila si kwa kuiga wenzio.
Mmekaa kimajungu majungu tu kukosoa watu waliothubutu. Acheni kuwakatisha tamaa Sie washabiki tunafurahia sana shindano hilo.

Kwangu mimi sijaona shindano linalonisisimua kama bss na ile iliyokuwa tusker project fame.
Haya ya east Africa got talent ,sijui nini, kwangu mimi bado sijayapenda kama BSS
Hongera madam Ritha
 
Sidhani kama Dully Sykes ni Judge mzuri kiivo..kazi yake ni kusema tu Nimependa sauti yako ni nzuri
 
Umejuaje kama majaji ni wazee kama hujawahi hata kuwaza kuangali....
BSS haina mvuto tena majaji wenyewe wazee wa miaka na miaka kwanini wasipishe majaji wapya? Sijawahi wazaga kuangalia upumbavu wa bss
 
kibaravumba, Kuna siku niliangalia moja ya audition zao kupitia youtube na kiukweli ilikuwa dissapointment.

Wanawakatisha tamaa watu kupita kiasi, kuna manzi mmoja mwanza aliambiwa anaimba fine ila hana manjonjo na look ya kistar hivyo akakosa nafasi SERIOUSLY!!!...
 
Hasa Jide ni kama ana chuki na washiriki wa kike,.... na ikitokea wameimba wimbo wa nandy ndo wanafukuzwa kama mbwa
 
Back
Top Bottom