Majaji pori kuipoteza CHADEMA kwenye kesi mahakamani

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,345
29,146
Watanzania walio wengi wanakumbwa na tatizo la kujisahau. Nareje sehemu ya maelezo ya hukumu dhidi ya Zombe na Wenzake. Jaji alisema mwenendo wa kesi ulijadiliwa mitandaoni kwa ushabiki na ilikuwa ni kuwahukumu watuhumiwa kabla kesi haijaisha.

Majaji Pori wamejificha nyuma ya keyboards wakijadili mienendo ya kesi na kutoa hukumu kabla Mahakama haijasoma hukumu

Hukumu ndogo ya kesi inayomkabili Mbowe na watuhumiwa wenzake imerejeleza kumbukumbu zangu kwenye hukumu ya Zombe.

Kumekuwa na mijadala tena inayowahusisha manguli wa sheria kuhusu mwenendo wa kesi hii na hasa kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi. Mijadala hii ilikuwa na lengo la kushawishi Mahakama kutoa hukumu in their favor, na Mahakama ilipohukumu tofauti mijadala imeendelea na kosa lile lile la kushinikiza Mahakama kuwa walikuw sahihi.

Ni jambo la wajibu kabisa kuripoti yanayojiri mahakamani hususani mwenendo wa kesi na wajibu huo unapaswa usiingilie haki ya Mahakama katika kutoa hukumu. Upo uwezekano mkubwa baadhi au wingi wa hukumu zisizo za haki ambapo mfumo wa rufaa umewekwa kutoa haki iliyopokwa kwenye hukumu.

Ninapata fadhaa sana kuona CHADEMA inaingizwa mkenge na wasioitakia mema kwa kujadili mwenendo wa kesi zilizopo mahakamani.

Uamuzi wa mahakama unaweza kujadilika kama tunavyojadili hapa. Kwa maoni yangu ni kwamba Jaji hakujikita kwenye kutenda haki bali kutumikia fadhila fulani kwenye kesi hii. Ni mara ya kwanza ninaona Hukumu inasomwa bila kuegemea vifungu vya sheria na badala yake ni maoni tu.

Nyie CHADEMA jifunzeni kudhibiti mihemko mnapokuwa na daawa mbele ya vyombo vya kutoa haki
IMG-20211019-WA0009.jpg
 
pole kamanda,sipati picha kwa sasa uko ktk hali gani.

jana tu umetoka kudemka kwamba mahakama imetenda haki kwa sabaya,leo unashindwa utoe neno gani

pole
Wakiacha kurukaruka kama bisi wakati kesi zipo mahakamani naamini kuna uwezekano mkubwa hukumu zikawa zinatenda haki zaidi.

Kuipangia au kuielekeza mahakama ifuate unachokiamini wewe ni kujiweka kwenye position ya kupata maamuzi against
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom