Majaji nao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majaji nao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Foundation, Apr 2, 2011.

 1. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Majaji 12 wapata kikombe kwa Babu Saturday, 02 April 2011 08:56 0diggsdigg

  Na Waandishi Wetu
  MAJAJI 12 ambao ni wakuu wa Kanda za Mahakama Kuu ya Tanzania, jana waliingia katika orodha ya vigogo kufika Samunge, Loliondo kupata tiba ya magonjwa sugu kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila.Habari zilizopatikana jana zimeeleza kwamba majaji hao walifika Samunge wakitokea Arusha ambako walikuwa na semina ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Idara ya Mahakama katika kushughulikia kesi za ukiukwaji wa haki za binadamu.

  Majaji hao, walifika kijiji hapo majira ya saa saba mchana wakiwa wanaongozwa na maofisa wa Serikali wilayani Ngorongoro. Walifika kwa magari ya kukodi aina ya Land Cruiser ambayo ni maalumu kwa ajili ya kubeba watalii.

  Tofauti na viongozi wengine, majaji hao, walikwenda kwa njia ya barabara wakitokea Arusha mjini na mara baada ya kufika nyumbani kwa mchungaji Mwasapila, waliandaliwa eneo maalumu na kila mmoja kupata kikombe cha dawa.

  SOURCE: MWANANCHI
   
 2. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  binadam kama wewe pia.
   
Loading...