Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,102
- 4,228
Tujaribu kuangalia jambo hili kwa uzuri wake na kwa mawanda yake kwa kuwa limezungumzwa na linazungumzwa sana hta jana tu Mh.Rais Mstaafu Benjamin Mkapa aliligusia.Ni jambo zuri sana ikiwa litajengewa mazingira mazuri na udhati lakini haya yote yanahitaji ushirikishwaji na huenda hili likawa ndiyo swali la msingi sana katika majadiliano"Je sera za kimaendeleo za Nchi yetu zinaruhusu ushirikishwaji?Ili tuweze kujadiliana sharti pande zote za majadiliano zishirikishwe kikamilifu hususani katika upashanaji habari.
Tukiiangalia historia kwa Tanzania Azimio la Arusha la Ujamaa na kujitegemea la 1967 mara tu baada ya uhuru lilikuwa kama msingi wa nyaraka mbalimbali zilizoruhusu ushirikishwaji na kwa lugha nyingine Azimio hilo lilikuwa sera Mama ya Ushirikiswaji lakini hali sivyo ilivyo leo kwa kuwa na tunachokiona leo ni Umma kushirikishwa kwa kiasi kidogo sana na kuachwa katika masuala mengi jambo linalowafanya wananchi wa kawaida kujenga utamaduni wa kunyamaza"culture of sillence"pamoja na Serikali yetu kujitahidi miaka ya karibuni kutaka miradi ya kimaendeleo ishirikishe Umma bado Wananchi wengi wa kawaida wanakosa taarif sahihi na za kutosha kuwawezesha kuingia kwenye majadiliano makini kutokana na mfumo na muundo wa kiupashanaji habari uliopo ambao maamuzi na taarif nyingi hutoka juu kuja chini na walio chini wao hubaki kama watekelezaji tu na waliopo juu wao ni waagizaji"top-down control system"
Tabb(2002)"kinachoshuhudiwa sasa katika Nchi za Kiafrika ni uchumi kushikiliwa na makampuni makubwa ya nje na matajiri wachache wa ndani"..hapo tunaona kuwa nafasu ya Mwananchi wa kawaida ni kama haipo n kama ipo basi ni ya kugeresha na kutokana na hali hii ndiyo maana miradi mingi ya Serikali imekuwa ikizorota kwa kuwa ushirikishwaji umepewa nafasi ndogo sana.
Miongoni mwa raslimali muhimu za ushirikishwaji ni taarifa, taarufa kuhusu raslimali, sera na programu, fursa za kiuchumi, haki na sheria, na mazingira kwa kuwa taarifa ni nguvu n kuw na habari au taarifa ni kuwa na nguvu hivyo basi Umma ukipewa taarifa sahihi na mazingir sahihi unaweza kuingia kwenye majadiliano makini.